08 March 2011

CBE lawani kwa kusimamisha mitihani

Na Rehema Mohamed

WANAFUNZI wa Chuo cha Biashara (CBE) Dar es Salaam wameulalamikia uongozi wa chuo hicho kwa kusitisha mitihani bila ya kuwapa maelezo ya
msingi.

Wanafunzi hao ni wa mwaka wa pili ngazi ya shahada ambao jana walitakiwa kufanya mitihani ya kumaliza mhura wa tatu.

Mmoja wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jina la Bw.Chales Mwita alisema, kusitishwa kwa mitihani hiyo ni kutokana na baadhi ya walimu wa chuo hicho, Dodoma kugoma kusimamia mitihani hiyo kutokana na kutolipwa mishahara yao.

Bw.Mwita alisema wanadai mitihani hiyo ifanyike ili wasiharibu utaratibu wa bodi ya mikopo ambao hulipa kulingana na mihura hivyo kama watachelewa watakosa fedha za mahitaji ya shule.

"Kutokana na hali hii wenzetu wa Dodoma wanataka kila chuo kifanye mitihani yao ili kama wengine kuna mgomo,wengine tuendelee na mitihani kama kawaida"alisema Bw.Mwita

Aliongeza kuwa taarifa kutoka kwa Mkurugezni wa mafunzo ambaye aliwapa taarifa za kusitishwa kwa mtihani huo zimesema mitihani hiyo itaendele baada ya kupata hatma ya walimu waliogoma chuo cha Dodoma.

Hata hivyo Ofisa Habari wa CBE, ambaye hakutaka kutaja jina lake alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo alikanusha kuwepo kwa mgomo na kusema kuwa kusitishwa kwa mitihani ni jambo la kawaida.

No comments:

Post a Comment