Na Mwandishi Wetu
HATIMAYE Mchungaji Ambilikile Masapila 'Babu' amelegeza msimamo wake wa kukataa kuhama katika Kijiji cha Samunge ili kupata sehemu ya wazi ambako atatoa huduma bila
msongamano na sasa amekubali ombi la kutoa tiba katika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo.
Hatua hiyo ambayo imepokewa kwa shangwe na wakazi wa Dar es Salaam na mikoa jirani, imekuja baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Babu na viongozi wa serikali, kutokana na maombi ya kumtaka mchungaji huyo ahamie sehemu ambayo itakuwa rahisi kufikika ili kuepuka maafa zaidi.
Tangu Babu aanze kutoa huduma hiyo mwishoni mwa mwaka jana, viongozi wengi wa serikali wamekuwa wakimiminika kijijini Samunge kupata kikombe na kutumia nafasi hiyo ama kumshauri kuboresha mazingira au kuhamia sehemu nyingine ambayo ni rahisi kufikika.
Kwa muda mrefu, katika kijiji cha Samunge na maeneo ya jirani ambalo foleni ya magari inapita kwenda kwa Babu kumekuwa kukiripotiwa vifo vya watu wengi, wanaopoteza maisha kabla ya kumfikia mchungaji huyo kutokana na msongamano.
Hata hivyo, Mchungaji Mwasapila amekuwa akishikilia msimamo kuwa hawezi kuhama eneo hilo hadi Mungu atakapomwonesha sehemu nyingine ya kutolea huduma, jambo ambalo limetokea jana.
Msemaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa katika maandalizi ya Siku ya Wajinga inayoadhimishwa duniani kote leo, alisema kuwa huduma hiyo itatolewa tu kwa wale watakaokuwa kwenye foleni kuanzia saa 12:30 hadi saa 4:00 asubuhi.
"Wa kwanza kufika atakuwa wa kwanza kupata kikombe. Hakutakuwa na ruksa ya kuchakachua foleni. Mnajua kuwa Babu hapendi, na wanaofanya hivyo hawaponi," alisisitiza.
Akizungumza na Majira jana, wakati anapanda helkopta iliyokodishwa kutoka Kenya tayari kwa safari ya Dar es Salaam, Babu alisema Mwenyezi Mungu amemruhusu kutoa tiba katika Uwanja wa Jangwani ili kunusuru maisha ya watu wengi wanaoshindwa kumfikia na wengine walioko mbali na Loliondo.
"Nadhani uamuzi huu utasaidia kuondoa msongamano hapa Samunge hasa kutokana na miundombinu mibaya. Unajua hata ile wiki moja niliyotoa kwa serikali imeisha bila miundombinu kutengamaa, hivyo nimekubali kuhamia Jangwani," alisema na kuongeza kuwa baada ya hapo atahamia Tabora na Mbeya ili kuonesha tofauti baina ya dawa yake na nyingine zinazotolewa huko.
Babu Masapila aliwaomba wakazi wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi na kuwahi, bila kujali kuwa leo ni Siku ya Wajinga.
NI SIKUUUUKUUUU YA WALIWAOOOOO WAJIIIINGA
ReplyDeleteleo ni sikukuu ya wajinga hatudanganyiki ngoooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteSi muende nyie paparazi huko alikowaambia kuwa atatoa tiba babu, hakuna mjinga
ReplyDeleteusinge mention sana neno siku ya wajinga ungepata wengi lakini umekosea kurudia siku ya wajinga, alafu wakenya wanahusikaje na kutoa helikopta?
ReplyDeletePeo.
poa ni sikuu ya wajinga ila wakazi wa dar babuu watamweka wapiiiiiiiiiiiiiiiii?
ReplyDeletewe nyewe tu bila ugeni msongamano, dala dala mwenge kwenda posta maasa matatu babu je akija siitakuwa masaa sita kukaa kwenye dala dala ambayo bila foleni ni dakika 10.
kama kunaviongozi wanaoshauri babuu ahamie dar wafikirie kwanza msongamano uliopo dar jumlisha msongamano wa babu kisha watapata jibu.