Na Leah Kassopa
MFANYAKAZI wa Kampuni ya kutengenezea Fenicha ya Palray, Bw. Ezekiel Ernest (55) amekufa baada ya kunaswa na umeme wakati anachoma vyuma, eneo la
Keko Mwanga jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Bw. David Misime alisema marehemu alinaswa na umeme gafla wakati akifanya kazi hiyo.
Bw. Misime alisema marehemu ambaye alikuwa mfanya kazi wa kitengo cha uungaji wa vyuma katika kampuni hiyo alipoteza fahamu na kufariki wakati akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Maiti imehifadhiwa hospitalini hapo, na upelelezi unaendelea.
No comments:
Post a Comment