03 February 2011

Tosamaganga wamtaka Waziri Kawambwa

Na Eliasa Ally, Iringa

WANAFUNZI wa Sekondari ya Tosamaganga  Wilaya ya Iringa Vijijini wamemtaka Waziri wa Elimu
nchini Dkt. Shukuru Kawambwa kufika
shuleni hapo ili kutatua matatizo ambayo yanaikabili shule hiyo.

Matatizo hayo ni ukosefu wa maji kubomoka kwa bweni la Mandela ambaloa linahatarisha maisha kwa kulala nje ya mabweni kuhofia usalama wao

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana baadhi ya wanafunzi wa sekondari hiyo walisema kuwa kutokana na ukosefu wa maji unaoikabili shule hiyo kwa muda mrefu hadi sasa wanafunzi zaidi ya watano wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa kutokana na kuumwa matumbo.

Waliongeza kuwa pamoja na mkuu wao wa shule Mwalimu Julias Shalla kujitahidi kurekebisha baadhi ya kero zilizokuwepo lakini shule hiyo kwa sasa imekuwa kama gofu na kuondoa sifa ya kubwa la shule hiyo.

Walisema baada ya kuona vioo vya madirisha ya shule hiyo vyote vimeharibika na kuzibwa kwa kutumia maboksi alikarabati kwa kuweka vioo vingine.

Walisema pia ameboresha taaluma nidhamu, michezo, uzalishaji wa mali na umakini katika utunzaji wa mazingira kwa kupanda na kutunza miti kuzunguka shule hiyo ambapo bado shule hiyo.

Waliongeza iwapo juhudi zikaongeka za kurabati mabweni  yangekuwa msaada mkubwa kwa vijana wa kizazi cha leo ambao wanajitokeza kusoma kwa bidii na maarifa.

Waliongeza kuwa ni aibu kwa shule kongwe kuachwa kabisa na serikali na kushindwa kutunzwa kwa ajili ya kumbukumbu ya vizazi vijavyo.

Shule hiyo ilianzishwa 1922 ikiwa chini ya Kanisa Katoliki ambapo serikali baada ya uhuru kutoka kwa wakoloni ilichukuliwa na serikali.

Mwalimu Shulla alikiri kuwepo kwa matatizo na kero hizo ambapo alisema kuwa zipo ambazo zimeanza kushughulikiwa ambapo zingine zinahitaji msaada mkubwa wa serikali

No comments:

Post a Comment