08 February 2011

Wananchi waua viongozi wa kijiji

Na Moses Mabula, Urambo

MWENYEKITI wa Kitongoji cha Zugimlole, Bw. Mkenzi Magida na Mtendaji wa Kijiji hicho Bw. Yasin Mkwabi wameuawa na wananchi wenye
hasira ambao wanaishi katika Msitu Hifadhi ya Taifa kinyume na sheria wilayani Urambo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, Bw. Liberatus Barlow, tukio hilo limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika Kijiji cha Zugimlole, wilayani Urambo.

Katika tukio hilo, viongozi hao na mgambo mmoja waliuawa papo hapo na wananchi wanaodaiwa ni wavamizi wa msitu wa hifadhi wa Ugalla Kaskazini huku mgambo mwingine akifariki dunia Jumapili kutokana na majeraha makubwa aliyopata baada ya kupigwa wananchi.

Waliouawa papo hapo ni Mtendaji wa Kijiji cha Zugimlole, Yasin Mkwabi, mwenyekiti wa kitongoji katika kijiji hicho, Makenzi Magida na mgambo, Emmanuel Gabriel. Mgambo Ally Mlangila alifariki dunia baadaye juzi.

Kamanda Barlow alisema watu wanaodaiwa kuwaua viongozi hao ni wale waliovamia msitu wa hifadhi wa Ugalla Kaskazini ambao hawaruhusiwi kuwemo ndani, ambao mifugo yao ilikuwa inashikiliwa na uongozi wa kijiji hicho.

Alisema watu hao waliwavizia viongozi hao walioenda kuangalia mifugo ambayo inakombolewa kwa kulipiwa faini kulingana na sheria zilizopo, ndipo walipoitana kwa ishara maalumu na kuwazingira kisha kuwaua.

Kamanda Barlow alisema watu sita wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo lakini majina yao yalihifadhiwa kuepuka kuvuruga uchunguzi.

1 comment:

  1. Jamani kama wakubwa wa serikali ya nchi kama RAIS hawafati sheria je wanchi mnategemea tutafata sheria? kule arusha polisi waliua raia kwa makusudi kwa sababu serikali ilivunja sheria ya vipengele vya uchaguzi wa MEYA,huko mbarali wameua huko babati police wanakimbiza raia wanaodai haki yao. Nafikiri hapo ndipo CCM ilipotufikisha tutaanza kunyongana kama kuku hasa kura zikiibiwa 2015.Watendaji wanaosimamia tutamalizana wakichakachua na police atakaejihusisha kutupiga tutamalizana kwani wote tunawajua kwani wapo uraiani,tutafuta mmojammoja tunamalizana kama ilivyofanyika kwa hao ndugu zetu walioenda kutafuta kula jasho la wengine

    ReplyDelete