08 February 2011

TRL wagoma, safari za treni hatihati

Na Benjamin Masese

WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) jana walianza mgomo hadi Waziri wa Uchukuzi, Bw. Omari Nundu atakapokutana nao kuwapa
uhakika wa kulipwa mafao yao na kueleza hatma ya mwekezaji kutoka India, Kampuni ya RITES.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu jana Mwenyekiti wa wafanyakazi Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Juma Lema alisema kitendo cha waziri kushindwa kutimiza ahadi yake ya kukutana nao Jumamosi iliyopita imeonesha wazi hawathaminiwi katika kampuni hiyo, hivyo ni vema wakasitisha kwenda kazini kwa siku zisizojulikana hadi hapo watakapoitwa.

Sasa tumesalimu amri na kuamua kugoma kufanya kazi na kuitaka serikali itulipe kiinua mgongo chetu tuondoke pia itueleze hatma ya mwekezaji kuendelea kusimamia kampuni, huku kukiwa na mkanganyiko na taarifa zisizo rasmi wakidai tayari mkataba umevunjwa, alisema.

Alisema kuwa kuwa ni muda mrefu kampuni hiyo imekuwa kwenye migogoro lakini serikali imeshindwa kutafuta suluhu na kumwacha mwekezaji aendelee kuleta hasara katika shirika hilo.

Tumejitahidi kwa kila njia ili kunusuru kampuni hii kufa lakini serikali bado imeendelea kumkumbatia huyu mwekezaji hivyo sisi tumekubaliana kugoma na kutaka tulipwe mgawo wetu na kazi iwe mwisho, aliongeza Hata hivyo kitendo cha wafanyakazi hao kufanya mgomo wa usio wa vurugu, baadhi ya abiria wanaotarajia kusafiri leo na treni ya abiria itokayo Dar es Salaam kwenda Kigoma wapo hawajui hatma yao ya safari au kurudishiwa nauli.

Hata wasafiri wanaotarajia kusafiri kesho wanaweza wasisafiri na nauli zao wakarudishiwa kwani hadi sasa hakuna maandalizi yeyote na huu mgomo utakwenda vituo vyote nchini,รข€ alsema mmoja kati ya wafanyakazi .

Kamamnda wa Polisi Kikosi cha Reli, Bi. Ruth Makelemo alikiri kuwepo kwa mgomo usiofahamika katika menejimenti ya TRL na kuongeza kuwa dalili za safari ya leo kutokuwepo zimeanza kuonekana kwa kuwa hakuna maandalizi yoyote yanayoendelea.

Alisema kuwa abiria waliopo katika stesheni hiyo walianza kuhoji kurudishiwa nauli zao lakini kitengo cha fedha hakikuweza kutoa tamko lolote juu ya safari hizo.

Bi. Makelemo alisema kuwa alipojaribu kuulizia juu ya urudishwaji wa nauli, aliambiwa leo watatoa tamko rasmi kama safari ipo au kurudisha nauli na kuwataka abiria hao kuwa na subira.

2 comments:

  1. gomeni tu baba, nchi haina mwenyewe hii.

    ReplyDelete
  2. Si mlichagua ccm fanyeni kazi mnalia nn sasa. Na bado.

    ReplyDelete