04 February 2011

Torres aanza kujifua Chelsea

LONDON, Uingereza

FERNANDO Torres ambaye ameweka rekodi ya kusajiliwa kwa ada kubwa zaidi nchini Uingereza kwa pauni milioni 50 kutoka Liverpool, juzi alinza
mazoezi rasmi na timu yake mpya.

Pamoja na mazoezi, pia alitazama nyumba ambayo atakuwa akiishi.

Mchezaji huyo wa ki-Hispania mwenye miaka 26, alikutana na wachezaji wenzake na kuoneshwa sehemu wanapoishi kabla ya kwenda katika uwanja wa mazoezi wa Cobham, Surrey.

Mashabiki wa Liverpool, wameonesha kusikitishwa na kuhama kwa mchezaji akiwemo, Shaun McCormack ( 36), ambaye alibadili jina lake na kujiita Fernando Torres mwezi uliopita. Alisema: "Nililia wakati niliposikia kuhusu kuhama kwake."

Michelle Moore mwenye miaka 31, alisema kuwa ni mchezaji wake kipenzi ambapo aliweka tatuu yake kwenye mkono wake.

Wakati huohuo, kocha wa Liverpool Kenny Dalnglish, amesema timu yake imeanza kuwatisha wapinzani wake hasa wanaofika kucheza Anfield.

"Tunaye Luis (Suarez), Andy Carroll, Raul Meireles na Steven Gerrard. Hawa wanne ni wachezaji wazuri sana ambao wanaweza kuchezeshana vizuri.Kocha huyo alisema hayo, baada ya timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stoke.

Meireles alifunga goli la kwanza na kisha Suarez, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza baada ya kusainiwa kutoka Ajax, alifunga bao la pili baada ya kumzunguka kipa Asmir Begovic dakika ya 79.

Liverpool itapambana na Chelsea katika mechi ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Anfield Jumapili.

No comments:

Post a Comment