23 February 2011

Samatta, Ulimwengu kuingoza Vijana Stars

Na Addolph Bruno

KIPA wa timu ya taifa 'Taifa Stars' na Mtibwa Sugar Shaabani Kado, Mbwana Samatha wa Simba na Thomas Ulimwengu anayecheza soka
Sweden wameitwa katika kikosi cha taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 23, 'Vijana Stars' ambacho kitaanza mazoezi leo.

Kikosi hicho hicho kinatarajia kushiriki mashindano ya Afrika ya kuwania kufuzu fainali za Olimpiki mwakani London, Uingereza.

Akizungumza kabla ya kutangaza kikosi hicho Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelo 'Julio' alisema katika uteuzi huo wamezingatia zaidi uwezo wa mchezaji husika ambao wanacheza Ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza zilizomalizika juzi mkoani Tanga.

Alisema wengine wamechaguliwa kutoka katika mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu 'Uhai Cup', yaliyofanyika Dar es Salaam Januari  mwaka huu.

Aliwataja wachezaji hao ni makipa Salehe Malande wa (TSA), Daud Gabriel (Azam FC), mabeki ni Hassan Kessy, Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Salumu Telela (Yanga).

Wengine ni mabeki Louis Tumba, Omary Mtaki (Azam FC), Zahoro Pazi (African Lyoni), Mbwana Hamis (Simba) na Babu Ally (Morani FC) huku viungo ni Ibrahim Juma, Himidi Mao na Salum Abubakar (Azam FC), Samweli Ngassa (African Lyon), Omega Seme (Yanga), Frank Domayo (JKT Ruvu) na Godfrey Innocent (Simba).

Wengine ni Jamal Mnyanje, Cosmas Freddy (Azam FC), Edward Shija (Simba), huku washambuliaji ni Benedict Ngassa (Moro United) na Atupele Green (Yanga).

Wakati huo huo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Boniface Wambura alisema kikosi hicho kitaingia kambini Jumamosi na kitacheza mechi mbili za kirafiki kabla ya kuondoka Machi 23 mwaka huu kwenda Younde, Cameroon kwa ajili ya mechi ya michuano hiyo itakayofanyika machi 26.

1 comment:

  1. Duh Shaban Kado nae yupo under .... acheni kuchakachua umri jamani!!!

    ReplyDelete