23 February 2011

Vyama vyasuasua kujiandaa All Africa Game

Na Amina Athumani

VYAMA vya michezo nchini ambavyo vitashiriki mashindano ya mataifa ya Afrika 'All Afrika Game' bado inasuasua na maandalizi ya michuano
hiyo.

Akizungumza jana kwa njia ya simu, Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Henri Lihaya alisema wataviita vyama hivyo hivi karibuni ili kuzungumza navyo kwa ajili ya kujua michezo iliyopewa dhamana ya katika michuano hiyo.

"Tungekuwa tumeshakifanya kikao hicho, lakini kuna baadhi ya mambo yaliingiliana hapa katikati na ndiyo maana hadi leo hii, bado hatujakifanya lakini tutaviita vyama vyote vinavyotarajiwa kushiriki michuano hii hivi karibuni, ili kuongea navyo," alisema Lihaya.

Vyama vitakavyokwenda kushiriki michuano hiyo ni pamoja na Chama cha kuogelea Tanzania (TSA), Shirikisho la ngumi za Ridhaa (BFT), Chama cha Riadha (RT) na Chama cha Netiboli (CHANETA).

Michuano hiyo ya Afrika inatarajia kufanyika Maputo, Msumbiji mwishoni mwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment