LONDON, Uingereza
MCHEZAJI wa zamani wa Tottenham na Wolves, Dean Richards amefariki akiwa na umri wa miaka
36, baada ya kuugua kwa muda mrefu.Wolves ilipanga
kutoa heshima za mwisho kwa mchezaji huyo, kabla ya mechi yao ya Ligi Kuu jana dhidi ya Spurs.
Taarifa ya klabu hiyo ilisomeka: "Kila mmoja katika Wolves amasikitishwa kwa kifo cha Dean Richards, aliyefariki asubuhi hii (juzi) akiwa na na umri wa 36 baada ya kupigana na maradhi kwa muda mrefu."
Richards, ambaye alicheza mechi nne akiwa na timu ya taifa, chini ya umri wa miaka 21, alianza kucheza soka akiwa na timu ya Bradford na pia aliichezea Southampton.
Aliachana na soka mwaka 2005 kutokana na kulalamika kujisikia kusinzia na maumivu ya kichwa.
Mwishoni alifanya kazi ya kuinoa timu ya watoto ya Ligi Daraja la Pili ya Bradford, iliyopo katika mji aliozaliwa.
Taarifa ya Bradford ilisomeka: "Klabu kweli imesikitishwa kusikia kifo cha mchezaji wake wa zamani na mpenzi, Dean Richards."
Taarifa ya Spurs imeongeza: "Kila mmoja katika Tottenham Hotspur amesikitika kusikia kifo cha mchezaji wetu wa zamani Dean Richards.
"Tunatoa rambirambi za dhati kwa familia ya Dean Richards katika wakati huu wa majonzi."
No comments:
Post a Comment