LONDON, Uingereza
KOCHA Roberto Martinez, amemtuhumu Wayne Rooney kwa akumpiga kipepsi (kiwiko), James McCarthy na kutopewa adhabu.Martinez alisisitiza kuwa
Rooney alimchezea rafu hiyo mchezaji wake makusudi katika mechi ambayo
Wigan ilichapwa mabao 4-0, dhidi ya Manchester United.
Refa Mark Clattenburg, aliona faulo hiyo na kuamuru kupigwa mpira wa adhabu.
Martinez alisema: "Niliona tukio lile wazi na refa aliona na kutoa mpira wa adhabu ya moja kwa moja.
"Unapotoa adhabu ya mpira wa moja kwa moja ni wazi kwamba itatakiwa kutolewa kadi nyekundu. Ukiangalia marudio, inaonesha wazi kabisa kuwa Rooney alimgonga usoni kwa kiwiko.
"Kama mmoja wa wachezaji wangu angefanya hivyo, ningeweza kusema kuwa alikuwa na bahati kuendelea kubakia uwanjani," alisema Martinez.
Alisema ingawa refa aliona kwa karibu, lakini hakutoa kadi nyekundu.
"Hakutoa kwa kuwa ilikuwa ni Wayne Rooney. Ilikuwa ni bahati mbaya katika mechi. Ndivyo ilivyokuwa."
Kocha wa Mancester United, Alex Ferguson anaamini kuwa Rooney, ambaye aliifungia United goli la tatu timu yake, hana kesi ya kujibu.
Fergie alisema: "Nilikuwa na nafasi ya kuona. Hakuna kitu katika hilo.
Kwa ushindi iliopata united imefikisha pointi 60, baada ya kucheza mechi 27 na inafuatiwa na Arsenal yenye pointi 56, Manchester City kabla ya mechi ya jana ilikuwa na pointi 49 nafasi ya tatu, ikifuati na Tottenham yenye pointi 47 na Chelsea ni ya tano ikiwa na pointi 45.
No comments:
Post a Comment