Na Mwali Ibrahim
KAIMU Katibu Mkuu wa Yanga, Mwesigwa Selestine amesema baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo, atahakikisha haipi nafasi migogoro inayoendelea na
badala yake ni kuangalia njia za kuindesha kisasa klabu hiyo kongwe nchini.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Selestine alisema matatizo yaliyopo Yanga si makubwa na tayari yameshapatiwa ufumbuzi na sasa kilichobaki ni yeye kufanya mambo ya utendaji.
"Uongozi uliopo kwa sasa madarakani umenihakikishia kwamba kuna hali nzuri ya kiutendaji, hivyo nitahakikisha kutumia nafasi hiyo vizuri kwa manufaa ya chama.
Alisema matatizo hayo si makubwa kiasi cha kuifanya klabu ishindwe kuendelea na taratibu nyingine za maendeleo na viongozi wamemhakikishia kwamba ufumbuzi utapatikana hivi karibuni.
Katibu huyo alisema, klabu hiyo ni kubwa na ina wapenzi wengi na pia ina mafanikio makubwa na hiyo ni moja ya changamoto atakazokabiliana nazo katika kipindi hiki.
Ndugu yangu Selestine usipoteze muda wako, Yanga hakuna uongozi wa mpira, cha msingi ujiunge nao tu kujinufaisha au uachane nao.
ReplyDeleteMpenzi wa Yanga soka anayekerwa na mwenendo wa timu.