Na Livinus Feruzi, Bukoba
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kagera imemhukumu Sudi Isimail (20) mkazi wa Kashabo, Manispaa ya Bukoba kutumikia kifungo cha
miaka saba jela na kuchapwa viboko sita, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la wizi wa mtoto.
Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Bw. Wilbard Mashauri baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Awali, ilidaiwa na Mwendesha Mashtaka Bw. Mathias Pastory kuwa Januari 23, mwaka 2009 saa nane mchana huko eneo la Migera katika Kata ya Nshambya, mshtakiwa huyo aliiba mtoto mdogo aliyejulikana kwa jina la Avineth Peter mwenye umri wa mwaka moja na nusu.
Bw. Pastory alidai kuwa kijana huyo alimkuta mtoto huyo akicheza nyumbani kwao, huku mama yake, Bi. Sipelata Adrian (21) akiendelea kufanya shughuli za usafi.
Alisema kuwa Isimail ambaye wakati huo alikuwa jirani na familia hiyo, mara baada ya kufika nyumbani hapo alisalimiana na mama wa mtoto na kisha kutoweka na mtoto huyo bila mama yake kujua na kuelekea kusikojulika.
Alisema kuwa mama huyo alianza jitihada za kumtafuta mtoto wake sehemu mbalimbali bila mafanikio na hakuonekana tena.
Ilielezwa kwamba wakati Isimail akiondoka akiwa njiani baadhi ya watu walimuona akiwa amembeba mtoto huyo.
Je, na aliyeua wanawake wawili na kuiba mabilioni alifungwa miaka mingapi?
ReplyDelete