25 February 2011

Dowans yatikisa maandamano CHADEMA

*Slaa asema kuilipa ni kuiba fedha za walalahoi
*Mbowe ataka Rais Kikwete achue hatua, la sivyo...


Na Suleiman Abeid, Mwanza

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilifanya maandamano ya amani na mkutano wa
hadhara huku kikiwataka viongozi wa serikali kushughulikia wahusika katika suala la malipo ya Dowans na ukosefu wa umeme nchini.

Moja ya maazimio yaliyotolewa jana na viongozi hao na kuungwa mkono na maelfu ya wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huo uliofanyika jana katika viwanja vya Furahisha mjini Mwanza ni kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha wote walioisababishia hasara nchi kwa kuingia mikataba yenye utata katika masuala ya umeme.

Akihutubia katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe alisema umefika wakati hivi sasa kwa Rais Kikwete kuwawajibisha watendaji wake wote ambao wamebainika kuwa ndiyo chanzo cha matatizo ya umeme katika nchi hii.

Bw. Mbowe alisema baada ya CHADEMA kuanzisha maandamano ya nchi nzima, chama hicho kinataka mara baada ya kumalizika kwa mzunguko huo katika mikoa yote, Rais Kikwete naye awe amechukua hatua dhidi ya wahusika wote vinginevyo wananchi watahamasishwa ili wamchukulie hatua yeye.

Bw. Mbowe alimtaka Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja kujiuzulu mara moja katika wadhifa wake kutokana na kushindwa kuisimamia vyema wizara hiyo na kwamba amekuwa akitoa maelezo tofauti kuhusiana na suala zima la umeme hapa nchini.

“Watanzania tunasema tumechoka sasa, tunahitaji ukombozi wa mara ya pili haraka, tatizo la umeme hapa nchini limegeuka kuwa ‘dili’ la kuvuta fedha kwa viongozi wetu, hapana Watanzania tunasema tumechoka, hatuwezi kukubali kuendelea na mateso tunayoyapata hivi sasa ya mgao wa umeme.

“Rais Kikwete na mawaziri wake wote hawajawahi kuonja makali ya mgao wa umeme kwa vile wao wana majenereta majumbani kwao ambayo yanalipiwa mafuta kwa kodi za wananchi, sasa tunasema awashughulike wale wote waliohusika na matatizo haya, vinginevyo tutawaaambia wananchi na yeye wamwajibishe,” alieleza.

Akizungumza suala la milipuko ya mabomu yaliyolipuka hivi karibuni kule Gongolamboto alisema tukio hilo siyo la bahati mbaya kama ilivyoelezwa na Rais Kikwete alipowatembelea wahanga wa mabomu hayo hivi karibuni na kwamba limesababishwa na uzembe.

Alisema jambo la ajabu, Rais Kikwete alidai kuwa tukio hilo limetokana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu, lakini siku ya pili yake badala ya kushiriki mazishi ya watu waliopoteza maisha kutokana na mabomu hayo alipanda ndege na kwenda Mauritania kusuluhisha mgogoro wa Ivory Cost.

“Kwa kweli Rais wetu ametushangaza sana, anadai kuwa tukio la milipuko ya mabomu kule Gongolamboto ni tukio lilitokana na mapenzi ya Mwenyezi Mungu, na kwamba halitatokea tena, lakini cha kusikitisha, rais anaacha kuzika watu wake anapanda ndege kwenda Mauritania, inasikitisha,” alieleza Bw. Mbowe.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Bw. Mbowe alisema iwapo serikali haitokubali kujirekebisha na kuwasikiliza wananchi kwa kutekeleza yale wanayoyasema, Rais Kikwete asishangae kuona yanatokea maandamano makubwa mengine ya nchi nzima ya kumuondoa katika madaraka kama ilivyotokea katika nchi za Tunisia na Misri.

Awali akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu wa CHADEMA Taifa, Dkt. Willibrod Slaa aliwashukuru wakazi wa jiji la Mwanza kukipigua kura chama hicho na kuwachagua wabunge wanaotokana na CHADEMA pamoja na madiwani wengi na hivyo kuweza kuunda serikali.

Dkt. Slaa alikemea kitendo cha kunyanyaswa kwa machinga waliokuwa wakifanya biashara zao mitaani ambapo aliutaka uongozi wa Jiji la Mwanza kuwashirikisha machinga hao katika kupanga na kuona ni maeneo yapi yanayowastahili wao kuendeshea biashara zao.

Hatua hiyo ilitokana na kelele za wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huo kumkataa kwa nguvu Meya wa Jiji la Mwanza, Bw. Josephat Kanyonyi Manyerere kwa madai aliwasaliti baada ya uchaguzi .

Kutokana na hali hiyo, Dkt. Slaa aliwaagiza madiwani wote katika halmashauri zote nchini zinazoongozwa na CHADEMA kuwa wahakikishe machinga hawanyanyaswi, na badala ya kufukuzana nao mitaani wakae pamoja na kupanga maeneo muafaka kwa ajili ya kuendeshea biashara zao.

“Ndugu zangu naomba muwe na subira, nimewasikia kilio chenu cha kumkataa meya wenu, na yeye nafikiri amesikia, lakini la muhimu ambalo napenda nilitolee agizo ni kwamba tangu sasa viongozi wa halmashauri acheni kuwasumbua ndugu zetu hawa wamachinga, walalahoi, hawa ndiyo wenye nchi.

“Ninasikitishwa sana ninaposikia viongozi wa serikali kuu wanapoingia mitaani kukimbizana na machinga, akiwemo Mkuu wa Mkoa ndugu yangu Bw. Abbas Kandoro, hii siyo kazi yako, wewe siyo mtawala, wewe ni ‘facilitator (mwezeshaji)’ siyo mtawala, hatutaki mkuu wa mkoa aingilie mambo ya jiji,” alisema.

Akizungumza suala la malipo ya Dowans alisema serikali haipaswi kulipa na kwamba kama ni lazima kulipwa, basi watakaopaswa kutoa fedha zao mfukoni ni Rais Kikwete na waziri wake Ngeleja.

Dkt. Slaa alisema tangu awali alikwisha sema suala la Dowans ni kiini macho, na mhusika mkuu ni mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz na kwamba hata huyo Brigedia aliyekuja nchini juzi, Brigedia Sulaiman Al- Adawi ni wa kuchongwa si muhusika mkuu.

Alisema Bw. Rostam anaelewa kila kitu, hivyo kulipa fedha hizo ni kuiba fedha za walalahoi wa Tanzania waziwazi na kwamba hata kamati ya Bw. Harrison Mwakyembe ilibaini kuwa kampuni ya Richmond ilikuwa kampuni ya kitapeli, hivyo hata Dowans aliyerithi naye ni tapeli.

“Sisi CHADEMA tunasema serikali ya CCM haipaswi kulipa fedha hizi kwa kampuni hii ya kitapeli, ushahidi wote unaonesha kuwa ni mchezo wa kuigiza lakini bado wanang’ang’ania kutaka kulipa, hata kamati ya bunge ilibaini hilo , tuelezwe iwapo akina Mwakyembe (Harrison) walisema uongo, basi tuwawajibishe wao,” alieleza Dkt. Slaa.

Viongozi hao wa CHADEMA leo wanatarajiwa kufanya mikutano katika wilaya zote za mkoa wa Mwanza ambapo kesho watakuwa mkoani Mara kabla ya kuelekea mkoani Shinyanga Jumatatu ijayo.

Amani yatawala maandamano

Kabla ya mkutano huo chama hicho kilifanya maandamano makubwa ya amani nchini yaliyoanzia katika viwanja vya Shule ya Msingi Buzuruga nje kidogo ya Jiji la Mwanza na kuishia katika viwanja vya Furahisha katikati ya mji yaliongozwa na viongozi wakuu wa kitaifa wa CHADEMA wakiwemo Mwenyekiti, Bw. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa na wabunge kadhaa wa chama hicho.

Wananchi wengi waliohudhuria maandamano hayo walionesha utulivu wa hali ya juu kwa kuandamana kwa amani huku wakiimba nyimbo mbalimbali za hamasa kwa kuzunguka mitaa mbalimbali kabla ya kuingia katika viwanja vya Furahisha.

Nyimbo nyingi zilikuwa zikipinga uamuzi wa serikali kutaka kuilipa kampuni ya Dowans, kupanda kwa gharama za umeme, kulaani mauaji ya wananchi mkoani Arusha na milipuko ya mabomu ya Gongolamboto jijini Dar es Salaam iliyotokea hivi karibuni.

Baadhi ya nyimbo hizo pia zilikuwa zikidai kuwa wananchi wamechoshwa na serikali ya CCM iliyopo madarakani ambayo walisema kila siku zinavyozidi kwenda mbele ndivyo maisha yanavyozidi kuwa magumu kwa wananchi wengi wenye vipato vya chini.

Mbali ya hali ya utulivu katika maandamano hayo pia wananchi wengi walifunga shughuli zao za biashara na kujipanga kando kando ya barabara kutoka eneo la Buzuruga hadi viwanja vya Furahisha hali iliyosababishwa kufungwa kwa muda kwa baadhi ya barabara zikiwemo za Nyerere na Pamba.

CHADEMA imeamua kuendesha maandamano ya amani kwa nchi nzima kupinga mambo manne makuu ambayo ni fujo zilizotokea mkoani Arusha na kusababisha vifo vya Watanzania wawili na raia moja wa Kenya ambapo serikali ya CCM imekuwa ikidai fujo hizo zilisababishwa na wana CHADEMA wenyewe madai ambayo viongozi wa CHADEMA wanayakanusha, wakisema zilisababishwa na polisi.

Pili kupinga kitendo cha serikali ya CCM cha kutaka kuilipa kampuni ya Dowans, ambapo CHADEMA inataka fedha hizo kama zipo zielekezwe katika huduma nyingine muhimu za kijamii ikiwemo elimu na afya.

Tatu, maandamano hayo yana lengo la kuwahamasisha wananchi kupinga kwa nguvu zote ongezeko la bei ya umeme nchini ambao umeongezwa kuanzia Januari Mosi mwaka huu kwa kiwango cha asilimia 18.5 hali ambayo CHADEMA wanadai ni kuwaongezea mzigo wa maisha magumu Watanzania, na kusababisha mfumuko wa bei kwa bidhaa zote muhimu.

Na mwisho maandamano hayo yatatumika kushinikiza kumtaka Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa nchini, Dkt. Hussein Mwinyi kujiuzulu katika wadhifa wake kutokana na tukio la milipuko ya mabomu huko Gongolamboto jijini Dar es Salaam, na kwamba ni tukio la pili kutokea nchini akiwa waziri wa wizara hiyo.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Majira jana katika eneo la Buzuruga muda mfupi kabla ya kuanza kwa maandamano hayo, walisema pamoja na kwamba viongozi wa CCM wamekuwa wakidai chama hicho hakiwezi kuondolewa madarakani hivi sasa, lakini muda wao wa kuondoka umefika.

“Kwa hali hii kwa kweli siku za CCM kuendelea kubaki madarakani zinahesabika, wananchi tumechoshwa na hali ya ugumu wa maisha, na serikali haioneshi harakati zozote za kutaka kuwasaidia wananchi wake kuondokana na hali hiyo.

Mapema, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Bw. Erasto Tumbo aliwaeleza waandishi wa habari kuwa maandamano kama hayo yataendelea kufanyika leo (Ijumaa) katika wilaya zote za mkoa wa Mwanza, ambapo Februari 26, yatahamia Mara na wilaya zake zote kabla ya kuelekea mkoani Shinyanga Februari, 28 na Machi Mosi mwaka huu.

Bw. Tumbo alisema Februari 2, mwaka huu maandamano hayo yatafanyika  mkoani Kagera na siku ya pili yake yatafanyika katika wilaya zote za mkoa huo ambapo itakuwa ndiyo mwisho wa maandamano hayo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

33 comments:

  1. Saf sana CHADEMA endeelen kuelimisha umma

    ReplyDelete
  2. we usishabikie upuuzi unawajua wanasiasa mlisha ambiwa swala la mbagala lisiwape umaarufu wanasiasa mboe anajipya gani ?tumieni akili na busara sisi tupo nje ya nchi tunafatilia sana maswala hayo lkn tusingependa amani ipotezwe na watu wenye uchu wa madaraka kujifanya wanauchungu wa nchi hiyo ikiwa tu wanatafuta kula sidhani hao hata wakiingia madarakani kunajipya litafanyika mfumo na utaratibu wa nchi utaendelea kuwa ule ule tumeona kenya hata zambia mabadiliko yalitokea kuna nn kipya kimefanyika?tujiulize hilo ukipata jibu utajua au upeo na mtandao mdogo vichwani mwetu?inasikitisha na haiingii akilini kuona watu mnadanganywa ikiwa mnajifanya mmesoma au ndio midomo tu mtu uonekane umeandika kujifurahisha?

    ReplyDelete
  3. wE ndo jinga kabisa, unakula kuku huko kisha unaleta za kwako ulaya, ULAYA! ULAYA! kwani huko mnakunya MANUKATO! nyie ndo walewale mnaoshirikiana kutuibia Mali za taifa letu, kama kuzungumzia ya Mbagala ilikuwa kutafuta umaarufu wa kisiasa sema sasa ya Gongolamboto, nayo ni ya kisiasa? ingalikuwa imetokea huko uliko nini kingetokea? usitufanye wajinga! kuwa ulaya haina maana kuwa una akili saaana kuzidi wale ambao wameshindwa kufika huko, Eee Mungu kwanini yasilipuke tena na Ndugu zake na huyu mshenzi wawe miongoni mwa WAFU? Wafe ndugu zake tu! kisha aseme tena, Wengine hata makaburi hawajajengea yametokea tena, wewe unaleta ushenzi wako katika maisha ya watu, WAFE NDUGUZO!

    ReplyDelete
  4. ..

    Wewe mchangiaji wa saa 11:58 PM Akili yako ndogo kama kazi unayoifanya huko nje ya nch: MFAGIA VINYESI au MALAYA TU. Unathubutu vipi kusema unafuatilia mambo ya Tanzania halafu unatoa upupu kama huo ?

    Huna tofauti na nguchiro Makamba wa CCM anayetoa uozo kila kukicha !!

    .

    ReplyDelete
  5. We anonym wa pili, bibi yenu makinda ndio anajitafutia umaarufu wa kisiasa pale Gongolamgoto.

    Hukuona picha za Mjengwa, spika mzima andjifinya macho na vitunguu swaumu ili yatoke machozi aonekane analia kumbe moyoni mwake ni furaha tele kuwa wameweza kukrieiti nafasi nyingine ya kuuza sura zao ili kuanzaa huruma kutoka kwa wapiga kura.

    ReplyDelete
  6. Matusi, lugha chafu si utamaduni wa Mtanzania. Toa maoni yako yenye kujenga na sio matusi haipendezi, unaweza kuonekana ni sawa na wale wengine walioanza kutoa lugha chafu. Nawatakia siku njema na mtoe changamoto yenye lugha ya kiistaarabu.

    ReplyDelete
  7. Ni kweli Mchngiaji 4:25 AM. Unajua jamaa wanaghadhabika na kutoa maneno ya hasira na matusi kutokana na kuchokozwa na wachangiaji wengine. Kuna watu ambao hawana uvumilivu wa kuona mtu anakejeli ama kuongea uozo. Hivi kweli kwenye uzembe wa kutowajibika, watu wakafa inabidi wanasiasa wasiongee kweli? Alafu lazima utekelezaji wa mambo hapa kwetu na kwingineko, huwezi kutenganisha siasa na utekelezaji kutokana na mfumo. Imekubalika Chama kilichoshinda ndiyo kinasimamisha serikali na kuchagua Mawaziri wanaosimamia wizara. Pia maamuzi/bajeti zinapitishwa bungeni. Hivyo, hao wanaoishi ULAYA wasidhihaki tunaoumia na kukosa la kujiokoa. Nimalizie kwa kusema hivi: Maumivu ya aliyevaa kiatu kinachobana, anayajua yule aliyekivaa.

    ReplyDelete
  8. kumbe hata matahira wapo ulaya. yaan hana tofauti na mapimbi wa ccm kama kikwete,makamba,msekwa na ngeleja. huyo alifkaje ulaya? labda alisafrishwa na wafirajji wa kizungu na sasa amefirwa m,paka akil imepooza.rud nyumban tukuombee upone

    ReplyDelete
  9. huyo wa ulaya atakuwa ni kimada wa akina kikwete ambaye amekodishiwa chumba hoteln il aweze kumliwaza kwa safari zake nyingi za ulaya. hayo anayooongea ni masimuliz ya ktandan na kikwete wake kwan hayana tofaut na hotuba za kikwete zilizojaa pumba na upuuz huku maisha ya watanzania yakielekea kaburn. we mbwa usitutishe na ulaya yako rud nyumban ujue maisha halisi ni yap na si maisha ya ukimada

    ReplyDelete
  10. ni matahira wachache tu ndio wanaeza aminishwa kuwa chadema ni chama cha udn. mm n mwislam na kamwe sikubaliani na propaganda hz chaf za ccm. shime waislam na wakristo tukiunge mkono chama hk tukfu kwa maslah ya taifa na tuachane kabsa na kna shehe yahya n lwakatare walionunuljiwa na kuwasaliti wanyonge. shme bakwata amken tuungane na wakatolk kuupnga ufsadi

    ReplyDelete
  11. damu ya wanyonge wa taifa hl itawalilia viongoz wote wa dn wanaoungana naccm kueneza propaganda za udn kuhsu chadema chama cha wanyonge.mm n mwislam msom na kamwe huez nidanganya na pumba za mashehe na baadhi ya maaskofu ambao baada ya kuhongwa wametusahau kondoo zao tunaoteketea kwa maisha magum. mmunghu atawalaan mpaka kiyama na historia ya nchi hii itawahukumu milele. mungu ibark chadema amin

    ReplyDelete
  12. Pamoja na madai ya kutokuilipa Dowans, mi naona waongeze pia madai ya kudai CCM iachie ngazi

    ReplyDelete
  13. Matusi si muhimu. Cha maana ni kuandamana na kumtaka Kikwete na CCm yake wajiuzulu. Wameshindwa kuleta umeme wanajishughulisha na utapeli wa kila aina. tuwashinikize viongozi wakuu na familia zao waondoke nchini kama wanavyofanya waarabu. WaTanzania wanaenda ulaya hawajifunzi lolote wao ni kufungua matawi ya CCM ulaya. Wakati watu wanatimua viongozi wasiofaa duniani kote

    ReplyDelete
  14. very hot watanzania. siamini!!! siamini hata. labda naota tu. unajua watanzania wenzangu tusilifumbieni macho kabisa hili swala. serikali ya CCM jamani inatutia aibu mwishowe tutakuja kuonekana matahahira kama mchangiaji wa kwanza anayejifanya anaishi ulaya. tusilifumbie macho hasa kwa vijana ambao muda huu tunahitaji kujijenga kifamilia jamani. tusimame kwa sauti na kauli moja tuseme CCM inatosha. tusiwaachie tu mbowe na dk slaa wale tayari ni wakombozi ambao wametufungila njia, tuifate njia kwa pamoja mpaka ikulu tukaseme kwa kikwete inatosha.
    tusipofanya hivyo, tusubirie disaster inakuja jamani.. maisha ya tanzaniai takuwa ni heri moto wa jehanamu coz yatakuwa magumu. nawasilisha hoja wajameni....

    ReplyDelete
  15. Wachangiaji mnatia kichefuchefu. Mnaongea ugoro mtupu. Ningekukuwa mhariri wa majira ningefunga ukurasa huu.

    ReplyDelete
  16. Watanzania wenzangu,hebu tujifunze kutafakari kabla ya ku-act kwa mambo ambayo yanaweza kuja kutufanya tukajuta. Nasema hivyo kutokana na jinsi wananchi mnavyojiingiza kwenye ushabiki huu wa CHADEMA bila kujua uhalisi kuhusu viongozi hawa wa CHADEMA.
    NEVER STOP THINKING!!
    Nukta ya kwanza:
    MAANDAMANO YANAYOFANYWA NA CHADEMA.
    Ni jambo la kidemokrasia watu kuandamana as long as process zote zimetekelezwa.Hakuna mtu mwenye akili atapingana na hili.Kuandamana kwa amani mwanza,ndicho kilichotakiwa hata Arusha.Lakini viongozi wa CHADEMA NDIO WALIOSABABISHA UPOTEVU WA MAISHA YA WATU WASIO NA HATIA.lakini hawataki kusema ukweli.Polisi hawakuwanyima kuandamana,CHADEMA walipewa route ya kupita kutokana na miundombinu ya Arusha kutokuwa ya kutosha(barabara),ili wasiathiri utendaji wa watu wengine wanaotumia barabara hizo.Wao wakakataa kwamba lazima wapite barabara zote wanaotaka wao.Polisi wakakataa.Walipopita barabara hizo kwa nguvu polisi wakazima maandamano yale.Kibaya zaidi ni kwamba waliandamana kuelekea kituo cha polisi walikokuwa viongozi wengine wa CHADEMA,eti kwenda kuwetoa..Can you imagine!! Sasa hili hawalizungumzi,wanaeneza uongo nchi nzima eti mauaji ya arusha,mauaji ya arusha,...kila kukicha.Dr Slaa ndie wa kulaumiwa kwa kusababisha wananchi wale wapoteze maisha kwa sababu yeye ndie aliyewahamasisha watu wandamane kwenda kituo cha polisi kuwatoa kina MBOWE.Na alijua kuna watu watapoteza maisha kwa sababu katika hali ya kawaida polisi hawawezi kuruhusu watu wapeleke maandamano polisi,what do you expect??
    Ninachosema,itoshe kusema kuwa,Dr Slaa alijua kuna watu watapoteza maisha kwenye maandamano yale,na of course ndio walichotaka ili wapate cha kuongea majukwaani..Imagine,watu wanatafuta umaarufu majukwaani kwa cost ya maisha ya watu wengine..kuna ubinafsi,unyama na ukatili kama huu..?? Do you think watakuwa wakatili kiasi gani hawa watu wakiingia madarakani?Jifunzeni kufukiri watanzania!! Do you think watanzania tunawahitaji watu walioichoka amani kama Mbowe na Slaa? Lengo la CHADEMA ni kuingia madakani kwa gharama yoyote ile,hata kama watu watapoteza maisha kiasi gani,damu zitamwagika kiasi gani..is that what we want? Mbowe na Dr Slaa ni watu hatari sana wasiojali uvunjifu wa amani katika nchi yetu.watanzania tunahitaji mabadiliko,tunahitaji kuing'oa CCM madarakani,lakini sio kwa style hii wanayoitaka CHADEMA,hatutaki siasa za chuki na za kichochezi zinazoenezwa na CHADEMA,hawa ni watu wenye uchu tu wa madaraka,hawana lolote..labda CHADEMA wabadili approach,lakini sio hii wanayoitumia ya ku-create tatizo then wapate umaarufu majukwaani kwa kuikashfu na kuilaumu serikali iliyoko madarakani..
    Nukta ya pili ntakuja baadae..

    ReplyDelete
  17. Kweli kabisa bora ukurasa huu ungefungwa watu wanashabikia siasa tu,mbona hawajiulizi kwa nini wamachinga wanamkataa meya wa chama chao walichokichagua? hata Slaa hana mpya cha kuwadanganya machinga kwani hata ccm inawapangia sehemu maalum lakini machinga hawataki,hizo ndio siasa za tz na africa,hiyo ndio picha halisi kwa vyama vyetu pindi wanapopata madaraka,siasa ni ATM ya kuckua pesa.wanasiasa ni waongo na wamepata watu wa kuwadanganya

    ReplyDelete
  18. huyu jama mpumbavu kwanza hayupo nje kama hayupo dabaga huko iringa basi atakuwa upcountry flani,amekosa uzalendo na hajui njaa ya msingi ya watanzania walio wengi,unaleta u ulaya hapa watu mlo mmoja hata town hajafika halafu kuna watu wachache wanatafuna kodi zetu.we kaa huko huko ulaya,labda iko siku kilio chetu kitasikika.

    ReplyDelete
  19. Watanzania wezangu mnazungumuza kwa uchungu tunajua kweli mnauchungu na yanyotokea nchini mwetu hivi sasa.nawaombeni tutoe maoni yetu bila jazba na matusi mazito kwa viongozi,pamoja na namna moja au nyingine kweli wanausika.

    ReplyDelete
  20. Fursa ya kuzungumza na ya kutoa maoni ni HAKI na UHURU wa kila mtu. Kufunga makala hii siyo suluhisho.

    Jua kwamba Hata maji ukiyaziba kwa ukuta yatabomoa tu !! Swala ni watu kuwa "responsible" kwa yale wanayoandika. Na naamini wanaoandika hapa sio watoto wadogo. Ni watu wazima wenye uchungu na nchi yao na wanaotaka mabadiliko.

    Inapotokea kwamba wananchi wanashindwa wafanye nini ili kukomesha MAFISADI na WASHIRIKA WAO hasa hasa VIONGOZI wa CCM na SERIKALI YAKE wanaoendelea kuiba rasilimali za watanzania,basi LUGHA kali mnazoziita "matusi" zinatumika kama jukwaa la uwafikishia hawa WEZI ujumbe kwamba "Wenye-nchi WANA HASIRA" na "WAMECHOKA KUVUMILIA" na pia kuwastahi viongozi wao !!

    Hivyo basi: Usibaki kushangaa tusi na kupendekeza kufunga hii makala. Jiulize ni kwa nini Watanzania wamefikia hatua ya kuwatukana viongozi wao matusi ya nguoni ??? Je nini suluhisho ?

    Shayo

    .

    ReplyDelete
  21. Shayo asante kwa mawazo mazuri.

    Miaka 50 ya uhuru bado tuko maskini kuliko kipindi cha mkoloni. Bado tunaongozwa na katiba ya kikoloni. Jeshi la polisi linafanya kazi kwa manufaa ya WAKOLONI MAMBOLEO = CCM NA SERIKALI YAKE. Mali zetu zinapelekwa nje badala ya kupelekwa kwa wananchi. Wawekezaji wa nje wanathaminiwa kuliko wananchi wa Tanzania.

    Mashule hayana vitabu wala waalimu. Wanafunzi wana-feli mitihahi kidato cha nne bado serikali haichukui hatua yoyote ya msingi. Mbagala mabomu yanalipuka, wananchi wanakufa, bado hatujifunzi lolote.

    Juzi Gongo la mboto wananchi wanau-awa tena kwa mabomu bado swala hili linachukuliwa kama siasa na siyo kwa kuwalinda raia na mali zao.
    Mahosipitalini hakuna dawa. Maskini hawezi kununua dawa hata ya kufunga kidonda !
    Nchi iko kwenye giza, umeme hakuna. Mikataba mibovu ya madini, umeme, rich-mond, etc etc

    Hii ndiyo miaka 50 ya UHURU ???????

    ..........Wote tunamjua adui wetu ni nani : CCM na serikali yake, ila basi ..........

    .........Tukipiga kura, kura zetu hazihesabiwi kihalali bali zina-chakachuliwa !! Tufanye nini kama siyo kuanzisha vita na wengine basi wanaishia kutoa matusi mazito ??

    Paul

    ReplyDelete
  22. Nawapongeza wachangiaji wote hapo juu isipokuwa wale anaotukana tu. kutoa maoni ya kuelimishana ndio njia ya uhuru zaidi inayotakiwa katika safu hii. Hata hivyo katika mambo ya itikadi kuna kutofautiana lakini tutofautiane kwa Hoja siyo matusi. Mchangiaji mwenzangu wa sa 11.25PM ameeleza mambo mengi sana hasa kuhusu Arusha. Huyu ndio lile kundi la Mh. Pinda ambao mnatoa taarifa kwa watu bila kuzifanyia utafiti. Suala la route Arusha halikuwepo na Chadma walifuata ruti moja tu tatizo lilikuwa taarifa za kiintelejensia walizopata Mwema kutoka kwa Mkuu wa Mkoa na fake Meya Lyimo zilileta rabsha. Si kusudi langu kurudia mambo ya Arusha maana ukweli unaeleweka na ndio maana Mh. Lema alipotoa kauli ya uongo waPinda ambao ni kama huu wa Kwako Spika Makinda aling'aka na kumtisha Mbunge Lema kumsimamisha vikao, lakini alivyothiisha hayo Spika aliyeyusha kujifanya atashughulikia yeye. Wananchi tunataka ushahidi utolewe hadharani ili ukweli ujulikane. Ndugu yangu wewe najua ni wa CCM hata mie ni mwana CCM lakini inapofika Chama kinapoteza mwelekeo na kinakuwa ni BMW - Baba, Mama, Watoto hatuna budi kusema ukweli. Nakushauri ujitahidi kufatilia mambo ili utoe michango yenye tija na si kuwalaumu Chadema pekee. walioua ni Polisi. Marehemu wale walipigwa risasi hawakuuawa na mawe ya waandamanaji utasemaje kuwa Chadema wamesababisha mauaji kama siyo UAKI - Upungufu wa Akili Kichwani mwako.
    Haya nguvu ya umma ilianzia Tunisia, ikaja Misri leo ipo Libya na huenda kesho ikaja Tanzania. Usishangae waliokufa Tunisia, Misri na Libya ni mashujaa wa ukombozi. Kama kufa ni kufa mbona watu wasio na hatia wameeuawa kule Mbagala na Gongolamboto? kwani hawa hawakuhitaji kuishi. acheni kutisha watu na amani ya watu wachache ambao ni viongozi pekee.

    ReplyDelete
  23. Watanzania wenzangu,lets try thinking critically.
    Time management.
    Think about idadi ya siku na masaa watakayotumia CHADEMA kuzunguka nchi nzima kunadi ujumbe huo wanaotaka kuueneza.. Katika kipindi hiki ambacho kwa kiasi kikubwa teknolojia imeenea,kuna haja ya kupoteza muda kurudia na kueleza ujumbe ambao umeshawafikia wananchi? Nlidhani maandamano eneo moja ilitosha kufikisha ujumbe maeneo mengine,..
    Hiyo idadi ya maelfu ya watu walioandamana mwanza multiply by vituo vyote watakavyohutubia,multiply by masaa watakayotumia kuandamana,unajua tungeweza kuyatumia kuzalisha kiasi gani??? Think scientifically you people!! Mtabadilika lini watanzania kujua muda ni function muhimu katika maisha yetu??
    Mwisho nawaasa kutumia kuhamasisha watu kuchukua hatua za kuiondoa serikali madarakani kwa njia ya maandamano,eti kama kule Misri,Tunisia na kwingineko..Mnataka kuwafikisha wapi watu nyie watu wenye ufinyu mdogo hivi wa akili,mnaochukulia mambo ya siasa kama ushabiki wa timu za mpira?
    How far are you sure kwamba hata kama mtaiondoa serikali hiyo kwa maandamano nchi itakuwa cool kama ilivyo Misri hivi sasa? Then what,mkishawatoa,ndio madarakani wakae akina Slaa na Mbowe,hawa wenye uchu wa kuingia madarakani kama fisi? Tolerance ya watu ambao,walishaendelea,demokrasia yao ilishapanuka is quite different from us men!!Kulinganisha Misri na Tanzania ni sawa na usiku na giza.. Our level of poverty has transformed the way we think and the way we react with matters like this you people.! Misri waliandamana zaidi ya wiki mbili bila kufanya kazi,lakini hakuna damu iliyomwagika,na baada ya Mubarak kuondoka nchi imebakia kwenye amani hadi sasa,do you think tanzania igekuwa hivyo?? Think criticaly!!

    ReplyDelete
  24. Ndugu uliyenitangulia hapa juu February 26, saa 4:15AM mawazo yako ni finyu kama ya Makamba. Unathani una hoja kumbe ni upupu.

    Soma hoja zilizotolewa hapo juu na wachangiaji kama Shayo na Puaul zitakusaidia ujue nchi yetu inakoelekea na ni ni kwa nini watu wanahasira na nini cha kufanya...... usikubali kuwa na wawazo finyi kama nguchiro !!!

    ReplyDelete
  25. Yaelekea mchangiaji wa mada ya tarehe 25 Feb. 11.22PM na wa mada ya 26 Feb. 04.15AM ni mtu mmoja aliyetumwa au mhusika ndani ya serikali hii ya kifisadi mwenye nia ya kutetea uozo uliopo.
    Katika Mada yake ya awali anaitetea serikali kwa yaliyotendeka Arusha akitumia nadharia za waongo na wazushi wakubwa, wasio na hata chembe ya haya; kina Saidi Mwema, Chagonji, Pinda na wahuni wengine. Kuhusu Arusha kila mtu mwenye akili timamu anafahamu ni Polisi ndiyo walio-provoke Chaos kwa kutumia risasi za moto kuwaua walipaji wa mishahara yao (a.k.a walipa kodi) waliokuwa wakiitumia haki yao iliyowekwa na Katiba ya kuandamana ili kueleza hisia zao!
    Si kweli kwamba waliojeruhiwa na waliouwawa walipita njia zilizozuiliwa au "Kuteka" kituo/vituo vya Polisi kwani ushahidi upo waziwazi kwamba miongoni mwa waliojeruhiwa na kuuwawa walifuatwa mpaka majumbani na baadhi nyumba za ibada kama makanisani. Labda kama mchangiaji huyu atatuhakikishia kwamba kulikuwa na vituo vya polisi kule. Hii inafafanua kwa nini serikali inagwaya kuunda tume huru kuchunguza uharamia uliofanywa na askari polisi wanaolindwa na kutetewa kwa hali na mali na serikali corrupt hii ya wahuni wa CCM. Mimi naamini siku haziko mbali utawala unaowajibika utaingia madarakani na kuyaweka yote yaliyotokea Arusha wazi na wahusika kuchukuliwa hatua. Hivi inaingiaje akilini kuona kikundi cha watu waliokabidhiwa dhamana ya kulinda mali na maisha kutenda kinyume chake, (yaani kuwaua,kuwapora na kuwajeruhi) kisha kuachwa wakizurura na kutembea vifua mbele kama kwamba wameua mende kabatini? Ni kweli hakuna mantiki hapo ya kuwakamata wahusika,kuwazuia hadi kukamilika kwa uchunguzi? Kuna mantiki gani kwa kitengo cha Upelelezi kukabidhiwa kazi ya kuupeleleza uhalifu uliofanywa na wao wenyewe, kisha kupeleka matokeo ya uchunguzi kwa mhalifu mkuu - Saidi Mwema ambaye kwa ndoto zake za mchana mwenyewe alizoziita za "kiinteligensia" mamia walijeruhiwa baadhi wakipoteza maisha?
    Nakubaliana na mchangiaji huyu katika jambo moja, nalo ni kwamba Mbowe na Slaa ni "Watu Hatari". Ndiyo, ni hatari sana, si kwa wananchi bali kwa CCM na mafisadi na vikaragosi wao kama huyu jamaa anayetaka kutupotosha kwa faida ya mafisadi na CCM. Maana bila ya Slaa uhalifu mwingi unaofanywa na CCM usingejulikana.
    Kuhusu "Time management" ni utumbo mtupu, kama yuko sincere basi aanza na kumshauri Kikwete anayezurura duniani kote kama Sindbad na safari zake zisizokuwa na tija wala mwisho. Kwangu mimi safari hizo ndizo zinazoliingizia taifa letu hasara kubwa kwa vile Kikwete huambaatana na msururu wa ndugu na marafiki zake kwa gharama za nchi!

    ReplyDelete
  26. Slaa anazeeka vibaya. Hii yote ni laana ya kuacha upadre. Anaongea bila kutumia busara. Chadema kimekuwa chama cha genge la wambea. Wamepoteza mwelekeo na kuanza kusema ovyo ili mradi kutafuta umaarufu kwa gharama yoyote ile. Wanajichimbia kaburi come 2015. Kuna fisadi yeyote katika TZ kama Mbowe na Ndesamburo? Jamani nyie acheni tu. Sisi wengine tumenyamaza tu. Mkitaka kujua true colors of chadema fanyeni analysis ya wabunge wao wa viti maalumu: wangapi? wanatoka wapi? na wanahusiana na nani? Hawa tunawajuwa waache kabisa lugha ya kusema eti wana uchungu na nchi. It is a gang of liars looking for cheap popularity. It is really a shame

    ReplyDelete
  27. Kuahidi si kutenda,ukiwa nje unaona unaweza kila jambo,ukiingia ndani mambo ya moto leo yameanza kujitokeza Meya wa Chadema anazomewa na waliompigia kura,na ahadi ilikuwa wamachinga mtafanya kazi zenu bila kuingiliwa,hata Slaa sasa anawaambia madiwani wa Chadema wawatengee machinga sehemu maalum tofauti na kauli za mwanzo kuwa mtafanya shughuli zenu bila bugdha,hizo ni sura za wanasiasa wanageuka kama kinyonga na Watz mnapiga makofi

    ReplyDelete
  28. nchi hii si ya chadema peke yake.

    ReplyDelete
  29. nchi hii si ya chadema peke yake, wala ccm peke yao, wala cuf, nccr.

    Maovu yakemewe lakini: KUSEMA KUWA TUTAANDAMANA ILI TUMUONDEWE ALIYECHAGULIWA KWA DEMOKRASIA, RABDA CHADEMA WAFANYE HIVYO ILI BAADAYE WAO WAPATE UONGOZI WATUONGEZE.

    ReplyDelete
  30. yaonekana KUNA JAMBO HAPA SI KUKEMEA UOVU TU; IKIWA KIONGOZI MKUU WA CHAMA SASA ANAFIKIRIA 'MAPINDUZI'; KUNA JAMBO HAPA CHADEMA HEBU TUELEZENI........

    ReplyDelete
  31. eng. mwakapango,E.P.AFebruary 27, 2011 at 5:56 PM

    ndugu zangu hili la matusi limefanywa makusudi ili watu waache kuchangia hoja za msingi. watu wanaotoa matusi wametumwa na watu wanaolinda maslahi ya watawala ili kuonyesha kuwa wanachofanya CHADEMA si cha msingi. napenda kuwa taarifu ndungu zangu sasa hivi sio muda muafaka wa kujibu hoja za CHADEMA wanaCCM na hasa walioko madarakani kukinusulu chama wanatakiwa waongeze bidii kutafutia ufumbuzi wa baadhi ya mambo ambayo ni kero kwa wananchi mfano huu mfumuko wa bei is not a real situation unaweza kuthibitiwa vitu vinatoka china ambako ni bei rahisi zithibi hizi bidhaa zishuke ili kupunguza makali. bei za vyakula ongeza ruzuku kwenye pembejeo za kilimo ili kushusha gharama za uzalishaji na bei za vyakula zitashuka na vilevile ongeeni na watu wa songas na dowans kupunguza makali ya umeme acheni kushiriki kwenye porojo hizi. hivi rafiki yangu William Ngereja unafanyaje kazi kutumia magazeti watu wanataka positive things na wewe usiwe chanzo cha kufa kwa CCM ukiona yamekufika shingoni jiuzulu sisi vijana tupo tele kukupokea kijiti. CHADEMA wametimiza matarajio ya upinzani wakipigwa mabomu wanawazidisha umaarufu wao ni bora CCM ikatekeleza yaliyo mazuri

    ReplyDelete
  32. jamani hebu nitoe takwimu na ushaidi, Tz ni nchi ya 147 kt ya nadhani 156 kwa umasikini duniani, ni nchi ya 47 kt ya 53 africa kwa elimu, kwa vifo vya malaria kwa mwaka wanakufa watz 60 hadi 80 elfu,rejea hotuba ya rais ya 2005 dec, ahadi alizotoa na hali halisi,rejea rasilimali za nchi kuibiwa na mafisadi na wawekezaji feki, vyote hivyo vinapita kwenye baraza la mawaziri na rais ni mwenyekiti, jua rais ana mamlaka ya kuwakamata na kuwaweka ndani ata viongozi waliopita ila wanaleana, hakuna ahadi iliyotimizwa, udini umechomekwa na viongozi wadini na serikali ya ccm baadhi ili kuhalalisha udhaifu wao na kutugawa ili waongoze,mimi ni mwahasibu, watz wenzangu, kodi inayokusanywa nchini ni asilimia 30 tu ingine yote kwa mafisadi. utalii tunaibiwa we wacha tu, wageni wanaokuja kutalii tz wameshalipia kwao! Mtz acha kuwa na ubinafsi kwa kuwa wewe unauwezo, hebu tembelea vijijini ndio utaona jinsi watu wanavyobigika, kuweni na huruma. niwaulize nani kt yenu au kwa familia kwake umeme safi? maji safi? elimu safi? makazi safi? kwa miaka 50! kuna mabadiliko au mwelekeo wowote? serikali ya cc inatugawa kwa manufaa yao. misri na egypty wamekufa wa c zaidi ya elfu 2, wakati malari imeuwa watu elfu 60 wastani wa watu elfu 5 kwa mwezi, je hii si kama mauwaji tu? kumbuka tuna dhahabu, almasi, tanzanite(Tz tu inapatikana), mbuga za wanyama. hivi umujiuliza pamoja na risilimali zote hizo ukienda benki kuu hatuna hata akiba yoyote ya dhahabu, almasi, tanzanite isaidie kwenye mifumuko ya bei na thamani ya mali za nchi.zikiisha hatuna cha kumbukumbu. cha msingi ni katiba mpya kuwaokoa wanyonge na kumaliza ufisadi. mi cna chama ila tuangalie hali halisi. tusitete serikali kwa udini au chama. tafakari

    ReplyDelete
  33. Wewe mchangiaji 11:22 ni kikaragosi ulietumwa kuleta propoganda hapa,kawaambie tuko macho na bundi hatui katika bati.Hii porojo ya kudai chadema wana uroho wa madaraka si kweli!!Mbona huwasemi CCM wanatumia nguvu kubwa kuchakachua matokeo WAKITUMIA TUME YA UCHAGUZI,JWTZ,POLISI NK ili wabaki ikulu???Huu sio zaidi ya UROHO NA UCHU WA MADARAKA!!
    CHADEMA kama nilivyo mimi tuna uchungu na maisha yetu yanayorudi nyuma badala ya kuboreka
    nawe 7:41 tuachie slaa na mbowe wetu kabisa,usiwaguse!!!Ohooo!!!Ukitaka kujua nguvu ya mlevi mwaga pombe yake!!!Ukitaka kutujua nguvu yetu wasemee vibaya viongozi wetu!!Ole wako
    kuna mtu safi,mwadilifu,msomi,mzalendo nk kama hawa.

    ReplyDelete