Na Mwandishi Wetu
BAADA ya kufungwa mabao 2-0 juzi na Yanga, uongozi wa timu ya Polisi Tanzania umesema utakaa na Kocha Mkuu wake, John Semkoko aeleze
sababu ya kupoteza michezo mitatu mfululizo hadi sasa.
Polisi Tanzania imeanza raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara kwa kuchapwa mchezo wa kwanza mabao 2-0 na Toto African na baadaye ikafungwa bao 1-0 na Mtibwa kabla ya kubandikwa tena Yanga juzi.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Leonard Kijagwa alisema baada ya kupata matokeo ya mchezo wa juzi dhidi ya Yanga uongozi wa juu wa Polisi utakaa na Simkoko ili awape sababu za msingi zilizosababisha kupoteza mechi hizo.
Alisema uongozi haujaridhika na mwenendo wa timu yao kwa kuwa waliwajibika kuipatia huduma zote muhimu kujandaa na raundi ya pili, lakini wanashangaa kuona wakifanya vibaya michezo waliyoanza kinyume na matarajio yao.
"Huu ni mchezo wa tatu sasa tumepoteza, hivyo tunatakiwa kukaa na kuona ni sababu gani hasa inayosababisha sisi kufungwa hivyo kinyume na matarajio yetu na kwa kuanzia uongozi utatakiwa kupata sababu za msingi kutoka kwa kocha kwanza," alisema katibu huyo.
No comments:
Post a Comment