14 January 2011

TEFA yatembeza bakuli kuandaa ligi

Na Andrew Ignas

UONGOZI wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Temeke (TEFA), umewataka wadau mbali mbali nchini kudhamini ligi ya wanawake ya wilaya hiyo ambayo mpaka sasa muelekeo wake haujaeleweka.Akizungumza na mwandishi
wa habari hizi Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa TEFA, Peter Mhinzi alisema ligi hiyo ya wanawake kwa wilaya ya Temeke hadi sasa inaonekana kususua kwa kukosa mfadhili.

Alisema wadau na walezi wa mpiwa miguu kwa sasa pia wanapaswa kuelekeza nguvu katika kusaidia ligi ndogo, hususan ligi ya wanawake kwa Wilaya ya Temeke ambayo haujulikani itaanza lini, kutokana na kutokuwa na fedha za kuendesha ligi hiyo.

"Ligi ya wanawake Wilaya ya Temeke, imeshindwa kufanyika kwa kuwa chama chetu hakina fedha za kutosha za  kuendesha ligi hii," alisema Mhinzi.

Hata hivyo alisema kutokana na kuwa mchezo huo wa soka upande wa wanawake duniani kote hivyo imefika wakati wa wadau na wahisani kuwekeza katika ligi mbali mbali za wanawake.

No comments:

Post a Comment