13 January 2011

Sara, Mashaka kukimbia Marathon Mali

Na Amina Athumani

WANARIADHA Sara Kavina na Mashaka Masumbuko, wanatarajia kuondoka nchini Januari 21 mwaka huu kwenda Bamalo, Mali kushiriki mbio za marathon Januari 23, mwaka huu Akizungumza Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa
Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui, alisema wanariadha hao tayari wameanza maandalizi ya mbio hizo ambazo zitashirikisha wanariadha kutoka nchi mbalimbali.

Alisema mashindano hayo yameandaliwa na Benki Kuu ya Afrika (BOA) na yatashirikisha wanariadha kutoka nchi zote zenye matawi ya benki hiyo.

"Mashindano haya yatatambulika kwa jina la BOA na yameandaliwa na kudhaminiwa na benki hiyo, hivyo kwa upande wetu tutapeleka wanariadha wawili ambao wanatoka JKT na JWTZ na tayari wameshapata vibali kutoka kazini mwao kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo," alisema Nyambui.

Alisema mashindano hayo ni ya siku moja na wanariadha hao wanatarajia kurejea nchini Januari 25, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment