10 January 2011

Rwanda, Misri zachanua U-17

KIGALI, Rwanda

WENYEJI wa michuano ya Afrika kwa vijana wenye miaka chini ya 17, Rwanda imeonesha malengo yake ya kutwaa ubingwa huo baada ya kuichapa Burkina Faso mabao 2-1, katika michuano ya tisa ya vijana hao iliyoanza kuchezwa
kwenye Uwanja wa Amahoro mjini Kigali, juzi.

Misri, katika mechi nyingine, ilitoka nyuma na kufanikiwa kuiangushia kipigo cha mabao 2-1, Senegal, katika mechi ya Kundi A.

Hiyo ni michuano ya pili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kufanyika nchini Rwanda, baada ya kuandaa fainali za vijana wenye miaka chini ya  20, miaka miwili iliyopita.

Washindi hao, watakuwa wanaangalia mechi itakayowakutanisha Jumanne, ambayo itatoa jibu la kinara wa kundi lao.Zikiwa timu nne katika kila kundi, ushindi mara mbili utaiwezesha kusonga mbele hatua ya nusu fainali na kujihakikishia kucheza fainali za Kombe la Dunia zilizopangwa kufanyika nchini Mexico, Juni.

Vijana wa Rwanda, walipata bao la kwanza dakika ya nne, lililofungwa na Faustin Usengimana na kuongeza bao la pili dakika 47, kupitia kwa Tibingana Mwesigwe.

Burkina Faso, washindi wa tatu katika michuano iliyofanyika miaka miwili iliyopita nchini Algeria, walicheza vizuri na kupata bao lao dakika ya 55, lililofungwa na Faical Ouedraogo.

Ni ushindi mzuri kwa mechi ya kwanza, ingawa naweza kusema penalti waliyopata Burkina Faso, haikuwa sahihi, alisema Kocha wa Rwanda, Richard Tardy.

Hapa hatuangalii nyuma, tunapeleka mawazo yetu kushinda mechi mbili zilizobaki katika kundi letu, aliongeza.Kocha wa Burkina Faso, Rui Manuel Pereira, alisema inasikitisha, wakati wakijipanga kusawazisha, wakafungwa bao la pili.

Tulicheza vizuri kipindi cha pili, lakini hatukufanya jitihada zaidi za kusawazisha,alisma.

Senegal ilitawala kipindi cha kwanza katika mechi yake, walipata bao lao dakika ya 21, lililofungwa na Ibrahima Ndiaye.Lakini, Misri ilikuja juu kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 61, kupitia kwa Mahmoud Abdelmonen. Mohamed Rasham, aliihakikishia ushindi Misri kwa kufunga bao la pili dakika ya 83.

Tumekuja hapa kubeba kombe na hakuna cha kushangaza, tutafurahia kombe hili,¡± alisema Kocha wa Misri Mohamed Omar.Tutahakikisha tunaendelea kushinda kama tulivyofanya, haijalishi kama mechi inayofuata tunacheza na wenyeji,¡± alisema.

Tulitumia nguvu nyingi sana kipindi cha kwanza na kuiruhusu Misri kututawala kipindi cha pili na ndiyo matokeo yake haya,¡± alisema Kocha wa Boukouta Cisse.Tulianza vibaya, lakini asilimia 100, tutawabana Rwanda na Burkina Faso ili tusonge mbele,¡± alisema.

No comments:

Post a Comment