Na Patrick Mabula, Kahama
MWENDESHA pikipiki mmoja wilayani Kahama ameuawa kinyama kwa kukatwa shingo na kitu chenye cha kali na watu wasiofahamika na kisha
kuporwa chombo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Diwani Athuman alimtaja mwendesha piki piki huyo kwa jina la Bw. Burugu Batromeo (23) mkazi wa Kijiji cha Mhongolo kilichopo nje kidogo ya mji wa Kahama.
Siku ya tukio mwendesha pikipiki hiyo alikodiwa na mtu asiyefahamika usiku huo na alionekana siku iliyofuata mbali kidogo na kijiji akiwa amekatwa na kitu chenye icha kali upande wa shavu la kulia na sehemu ya shingo ya yake.
Mtendaji wa Kata ya Mhongolo, Bw. Ally Matisho alisema kijana huyo alikodiwa na watu hao ili awapeleke kitogoji cha Lubela kilichopo kijiji jirani cha Nyashimbi, walipofika katikati ya mbuga walimchinja na kumyang’anya pikipiki yake.
Panga walilotumia lilikutwa katika eneo la tukio na walichukua pikipiki yake aina ya SANLG iliyokuwa na usajili wa namba T812 BNK na kwenda nayo kusikojulikana.
Wakati huo huo, vijana watatu wakazi wa mjini Kahama waliotambulika kwa majina ya Bw. Emmanuel Magembe (28) , Mrisho Ibrahimu ( 26 ) , Joseph Daud (25) wamehukumiwa na mahakama ya wilaya ya Kahama kwenda jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa pikipiki kwa kutumia nguvu.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Bi. Lilian Rugarabamu baada ya kulidhika pasipo shaka na upande wa mashtaka uliotolewa mahakamani hapo kuwa walitenda makosa hayo na kuwatia hatiani kutumikia kifungo hicho.
Awali, ilidaiwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka ulioongozwa na Mwendesha Mashtaka Bw. Felix Mbise kuwa watu hao walitenda kosa hilo Aprili 4, mwaka jana saa mbili usiku katika kijiji cha Nyang’wale wilayani Kahama, walipomvamia Francis Donald na kumpora kwa nguvu pikipiki yake aina ya SANLG nyenye namba usajili T 404 BES.
No comments:
Post a Comment