24 January 2011

Mtandao umemomonyoa maadili ya taifa-Wadau

Na Jumbe Ismailly, Singida

WADAU wa kongamano la kujadili Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 wamesema moja ya sababu zinazochangia mmomonyoko wa maadili kwa
viongozi wa serikali ni uteuzi mbaya unaofanywa kwa kuangalia watu waliopo kwenye 'mtandao' wa kambi ya kiongozi mwenye mamlaka ya uteuzi.

Wadau hao kutoka taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na kijamii waliyasema hayo kwenye semina iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA), mjini Singida.

Wadau hao, Bw. Ivo Manyaku, Bw. Emmanueli Misholi na Bw. Eugen Shao waliweka bayana kuwa umefika wakati badala ya kuendeleza tabia ya kutoa madaraka kama takrima, wenye mamlaka waanze
kuangalia watu wenye maadili mema.

Bw. Misholi alibainisha kwamba wakati wa uchaguzi kulikuwa na makundi ya kampeni kwa wagombea wa nafasi mbalimbali, hali inayofanya wenye mamlaka ya kufanya uteuzi wa viongozi kupata na vigugumizi na kutaka kutoa takrima kwa waliowasaidia.

Kusiwe na kutafutiana takrima kwa sababu uchaguzi umeisha, ifike wakati sasa tafuteni watu wenye maadili mema muwape nafasi ambazo ni dhamana kwa
ajili ya taifa hili, ili wautengeneze upendo kwa watu, alibainisha Bw. Misholi.

Bw. Misholi aliweka bayana kuwa siyo rahisi kuhubiri upendo kwa mdomo wakati kwa matendo yao wana mmomonyoko.

Ndiyo maana Nyerere alikuwa anaangalia, wakati mwingine utakuta mwalimu anatolewa wapi huko (asiyefahamika) na kufika mahali watu mnamshangaa.

Halafu anafanya maajabu, lakini sasa hivi mambo yameshakwisha, sasa hivi tunatengeneza network (mtandao) kama mtu haupo kwenye mtandao hauwezi kwenda kokote kule, alisisitiza. 

Alisema kutokana na dhana hiyo ya 'mtandao', viongozi wasiokuwa na maadili wameendelea kupatikana, na hivyo kuhoji endapo mtu akipatikana kwa njia ya rushwa, kitu gani atarajiwe kukifanya akiwa madarakani.

Kwa upande wake Bw. Manyaku alisema kuanzia ngazi ya kijiji, kata, wilaya, mkoa mpaka taifa hakuna maadili, hali ambayo amaesema imesababisha hali ya uchumi wa nchi kuyumba.


Hii imesababisha hata uchumi wetu kuyumba kwa sababu sasa ni suala la wizi, ufisadi, rushwa, utaifa hakuna watu waliopewa mamlaka na dhamana mbalimbali katika nchi hawana utaifa, wana
umimi,รข€ alisisitiza Bw. Manyaku.

Kwa mujibu wa msemaji huyo malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 hayawezi kufikiwa kwa sababu kila mmoja anaona kuwa akipata nafasi
anadhamiria kuanza kujinufaisha kwanza mwenyewe.

Naye Bw. Shao alisema kutokana na ubinafsi uliopo kwa idadi kubwa ya viongozi walipo madarakani, wamekuwa hawatendi haki katika dhamana walizopewa kwa manufaa ya wananchi.

2 comments:

  1. NI KWELI WADAU, KWA VILE WATANZANIA WANAFIRI KWA TUMBO TU NA NDIYO MAANA VIONGOZI WANAPATIKA KWA KUANGALIA MTU ATAKAYEMSHIBISHA AU ALIYEMSHIBISHA RAIS TUMBO WAKATI WA KAMPENI.

    ReplyDelete
  2. HAKIKA TANZANIA NI NCHI YA MADARAKA URAFIKA NA SI UTENDAJI NA USISHANGAE WAZIRI ANA SHAHADA YA KILIMO AKAWA WAZIRI WA KATIBA

    ReplyDelete