Na Kassian Nyandindi, Mbinga
MCHUNGAJI wa Kanisa la Yehova la mjini Songea mkoani Ruvuma amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na kosa la wizi wa vifaa vya umeme.Hukumu hiyo ilitolewa dhidi ya mchungaji huyo na
mwenzake, katika Mahakama ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya hiyo, Bw. Frank Mahimbali.
Awali Mwendesha Mashtaka, Inspekta Saana alidai mbele ya hakimu huyo kuwa tukio hilo la wizi lilitokea Agosti Mosi mwaka huu katika Shule ya Sekondari St. Luise iliyopo Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga.
Inspekta Saana alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Issaya Mwakalinga (32) mkazi wa Songea mjini na Denice Masetti (28) mkazi wa Namabengo Wilayani Namtumbo.Alidai kuwa watuhumiwa hao waliiba vifaa viwili vya kuzalisha umeme jua, yenye thamani ya sh. milioni mbili, mali ya shule hiyo.
Hukumu hiyo ilitolewa baada ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kuthibitisha kwamba mchungaji huyo na mwenzake walipanda juu ya paa la jengo la shule hiyo na kuiba vifaa hivyo.
Check hizo mvua, 7!! Chenge? faini, tena laki 7 tu.
ReplyDeleteKisa wa kwanza kaiba solar panel, wa pili kaua watu wawili!
UNJUST LAW IS NOT LAW AT ALL!!