10 January 2011

CCM: Tuna madiwani 16 Arusha

Na John Daniel

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimedai kuna taarifa za uongo zinazosambazwa kuhusu idadi ya madiwani wake katika Manispaa ya Arusha na kueleza kuwa chenyewe ndicho kinachoongoza kwa kuwa na jumla ya madiwani 16 wakiwemo
wabunge watatu.

Chama hicho pia kimesisitiza kuwa kama kingeshindwa kisingeweza kugombania kiti hicho cha umeya kwa kuwa sera na ilani za uchaguzi zitakazotekelezwa na kiongozi huyo bado ni za CCM na si vinginevyo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumulumba, Dar es Salaam jana, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda, Bw. Tambwe Hiza alisema ni aibu kwa watu wanaojiita viongozi kudaganya wananchi kuhusu idadi ya madiwani bila kuona aibu.

"Kuna taarifa za uwongo zinazoenezwa kwamba CCM imepora umeya Arusha, ukweli ni kwamba CCM ndio ina madiwani wengi kuliko CHADEMA, tuna madiwani 10 wa kuchaguliwa, watatu wa viti maalumu na wabunge watatu, jumla 16.

CHADEMA wana madiwani wanane wa kuchaguliwa, viti maalum watatu, wabunge wawili wa viti maalum na mbunge moja wa kuchaguliwa jumla 14, jamani hapo nani ana madiwani wengi?" alihoji Bw. Tambwe na kuongeza:

"Kwanza CCM hatuwezi kugombani umeya wa Arusha maana sera na ilani ya uchaguzi inayotekelezwa ni ya CCM, asilimia 90 ya fedha za maendeleo za halmashauri zote ikiwemo Arusha zinatoka serikali kuu ya CCM, sasa hata meya akitoka chama gani atatekeleza mipango ya ilani ya CCM, lakini kilichopo Arusha ni ukweli kwamba tulishinda umeya," alisisitiza Bw. Tambwe.

Alisema anasikitishwa na CHADEMA kuhoji uhalali wa  Mbunge wake wa viti maalumu, Bi. Mary Chatanda, kuwa mmoja wa wajumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo wakati sheria ziko wazi kuhusu eneo gani mbunge wa viti maalumu atawakilisha.

"Tarehe 10.12.2010 CHADEMA wenyewe walimwandikia barua Mwanasheria Mkuu wa serikali kuomba ufafanuzi wa kisheria kuhusu wajumbe wa halmashauri kisheria na katika majibu yake kupitia barua yenye kumbukumbu na. JC-A.130-74 ya 16.12.2010 aliwapa ufafanuzi kuwa ni maamuzi ya chama husika kuamua mbunge wake wa viti maalumu atawajibika halmashauri ipi.

"Na hii waliuliza baada ya wao CHADEMA kuamua wabunge wake wawili, Bi. Grace Kiwelu na Bi. Lucy Owenya wawakilishe Halmashauri ya Hai na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo kuwakatalia, lakini baada ya ufafanuzi huo wale wabunge waliruhusiwa, sasa wanachohoji ni nini kama si kupotosha tu wananchi kwa makusudi ili wajitafutie umaarufu bure," alisema Bw. Tambwe.

Alisema kwa mujibu wa sura ya 287 ya kifungu cha 35 1 D wabunge wa viti maalumu wanatokana na idadi ya kura za chama husika, lakini ni wapi wafanye kazi zao ni uamuzi wa mamlaka husika ya chama kilichowateua na kutoa mfano kuwa kwa upande wa CHADEMA kazi hiyo hufanywa na Kamati Kuu.

"Sisi tunasema kama CHADEMA wanadai kuna ukiukwaji wa sheria waende mahakamani badala ya kuchanganya watu, mbona wanadai wameshindwa kuhoji ushindi wa rais eti sheria inawazuia kwenda mahakamani, ndio maana wanataka katiba mpya mbona hili la meya wanaruhusiwa kwenda mahakamani lakini hawaendi kama wana haki," alihoji.

Alikana CCM kutaka kufanya mazungumzo yoyote na CHADEMA kuhusu suala hilo na kusisitiza kuwa chama chake kiko sahihi, hivyo hakina sababu wala nia ya mazungumzo.

21 comments:

  1. CCM wauaji, walafi wa madaraka, mafisadi lakini kila kitu kina mwisho wake. Ukweli utasimama tu.

    ReplyDelete
  2. mimi nafikiri hili suala lingekwenda mahakamani ndio ingekuwa sahihi maana kila upande ungewasilisha hoja zake za madai na utetezi ambapo wananchi wote kwa ujumla tungekuwa na nafasi ya kusikiliza na tungekuwa pumba na mchele. Maana wanasiasa wote watambue historia itawahukumu hapo baadae. Vurugu hazijengi zikianza kumalizika ni kazi na pia huwa zinachukuwa muda mrefu na pia madhara ni makubwa kwa manufaa ya wachache tuuuu.

    ReplyDelete
  3. AAAAGGGRRRH!! WANA KILL SOME 1 RIGHT NOW!! HATE SISIEMBUUUU, WAFISADI WWATUPE SHEZXXXXXX..DAMEE!!GOH!

    ReplyDelete
  4. NA DIWANI WA TANGA ALIFIKAJE KWENYE UCHAGUZI? SIO KUONGEA ONGEA TU HOVYO.

    ReplyDelete
  5. Ningependa sana kuona mijadala hii inaendeshwa kwa hoja badala ya hisia binafsi. Hili la wabunge wa viti maalum naona binafsi nimefunguliwa macho zaidi. Mwenye data zaidi naomba aziweke hapa

    ReplyDelete
  6. CCM TUMEWACHOKA NA UNAFIKI NA UZANDIKI WENU. BADO KITAMBO TU DUNIA YOTE ITAJUA MLIVYO. MNANG'ANG'ANIA MADARAKA KAMA WAKOMUNISTI WA URUSI. LAKINI NA WAO WALIPOROMOKA BAADA YA MIAKA 70 TU. MMETUMIA POLISI KUUA, MNADANDAYA WANYONGE, MNANUKA RUSHWA KILA KONA - AU MMESAHAU KURA ZENU ZA MAONI NA WAKATI WA UCHAGUZI MLIVYOKUWA KICHEKESHO NA AIBU, HAMKUBALI MAKOSA, NANI ASIYEWAJUA??? MNA MAADILI KWELI NYIE?? SHAME ON YOU!! KWA KWELI WAPERNDA HAKI NA AMANI WAMECHOKA. HAMNA KAZI ZINGINE ZA KUFANYA? KILIMO KWANZA KINAWAHITAJI, MBONA MNANGANGANIA KUTAWALA WATU WALIOWACHOKA?? HAMNA TOFAUTI NA ZIMBABWE, GGABO, NA MADIKITETA WENGINE. MNATUMIA UNYONGE WA WTZ KAMA MTAJI WENU WA KISIASA MTU AKIWASIFIA MNAFURAHI HATA NI SIFA FEKI, AKIWAKOSOA MNAMPA LABEL YA KIDINI AU UKABILA. CHEAP THINKING!!

    ReplyDelete
  7. Kwenda mahakamani au kutokwenda hakuondoi haki ya CHADEMA kuandamana, bado walikuwa wanazo haki zote mbili kikatiba za ama kwenda mahakamani, kuandamna ama vyote viwili, ni nani amezuia haki ya CHADEMA kuandamana? nguvu iliyotumika kutawanya maandamano yale ilikuwa kubwa kuliko nguvu ambayo ingetumika kuyalinda maandamano yale fanfanyike kwa amani. Hakuna mtu yeyote atasema chochote kuhalalisha mauaji ya Arusha tukamuelewa sisi wananchi. Tuache porojo za kisiasa

    ReplyDelete
  8. kwa simple mathematics kama ya sobibo, wananchi wa arusha wanapaswa tuwajua polisi walioua. wanapaswa kujua meya anakaa wapi. wanapaswa kujua wake/waume zao na watotot wao wanapatikana wapi. hawana budi kupata misiba kila mtu kwa wakati wake. people's power.

    ReplyDelete
  9. CCM wanafikiri siasa za ubabe zitawasaidia kumbe zinazidi kuwazamisha kwenye shimo refu ambalo hawataweza kutoka maana Wananchi wmeshachoka na vituko vyao

    Tambwe Hizza wacha usani na ukuwadi maana nymbo hizo umeziimba sana ulipokuwa CUF na sasa unaziimba CCM ili mkono uwene tumboni

    CCM kwisha kwisha kwisha

    ReplyDelete
  10. Hivi Tambwe Hiza hajiulizi maana ya neno "Propaganda"? Hiyo nafasi aliyowekwa haoni kuwa ni nafasi ya watu "Vilaza" wasio na uwezo wa kufikiri wazungu wanasema "outside the box" - Ningekuwa namfahamu binafi ningemshauri aachane na hiyo idara maana jina tu la idara hiyo inatosha kumfanya mtu adharaulike hata kama kasema kitu chenye point - Aachane kabisa na masuala ya Arusha, cha msingi ambacho ningemshauri afanye ni kuwashauri wenzake watoe pole kwa wanafamilia waliopoteza ndugu zao...thats all! More than that itakuwa ni CRAP!

    ReplyDelete
  11. Hiza umenena. Mbumbumbu wataendelea kupiga kelele. Kwa wao ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa.
    wametawaliwa na udini. Thumun buq'mun humyun....

    ReplyDelete
  12. wanaoshabikia udini ni heri wakajiuliza kama kweli udini ukiingia nchi hii ni kundi lipi litanufaika na lipi litapoteza. Tusikurupuke kutaka vitu ambavyo vitatugarimu. Eh Baba wa Taifa Mwal. J.K. Nyerere rudi haraka umwadabishe Kikwete uliyemkataa hadharani. Amedhamiria kuua wananchi kwa ulafi na uroho wa madaraka. Rudi baba, rudi. Huku saas hivi kuna kila dalili ya Kikwete kushamirisha udini akisaidiwa na Makamba. Wote hawa hawakuwa chagua lako wakati ule CCM kikiwa chama chenye weledi. Ikulu imejaa watu wasio na udhu wa kufanya kazi huko. Lugha zao ni matusi, kashfa, kebehi, dharau, n.k. Ule utakatifu uliouuhubiri sana, umetoweka. Rudi Baba, Rudi!!!!

    ReplyDelete
  13. Sawa Sasa kama CCM ina uhakika kuwa ilishinda kihalali kwa nini isikubali huo uchaguzi ukarudiwa na wakaendesha hii manispaa kwa amani bila manunguniko yeyote? Unafikiri uchaguzi ukiwekwa hadharani kuna haki itapotea tukiachana na ushabiki wa makamba na hawa wengine wanaotaka sifa. Makamba na ubabe wake akumbuke hii ni Tanzania ya amani sio Iraq. Hawezi kutawala watu ambao hawampendi kila siku kutakuwa na malumbano ambayo hayatakwisha.
    Mnasema kuna vyombo vya sheria, mahakama nk, je tujiulize hawa polisi wao wanafanya kazi kwa ajili ya nani na hiyo mahakama itafanya kazi kwa ajiliya nani. Je hapa kuna haki itapatikana kama polisi wameweza kuvamia maandamano na ya amani kutumami silaha kali, na nguvu kumba kupita kiasi. Sasa tunajua tupo kwenye maombolezo hata watu liwapite masikioni na machoni wao badi ni siasa tu.
    Mimi ninashangaa huyu Rais yupo au kiti chake kamwachia makamba. Kwa sababu ninaona hoja za serikali wanajibu watu ambao hata hawahusiki. Mf Chitanda au Makamba wasingeweza kujibu ile hoja ya maaskofu na mashehe kwa dharau namna hiyo. Wao waliuliza serikali hawaja uliza CCM.

    ReplyDelete
  14. Mimi nafikiri hata Jeshi la Polisi liache kujidhalilisha kwa kufuata kila kitu wanachoamuliwa na Mabosi wao!!!! Wanahitaji kutumia akili zaidi na maarifa waliyonayo tukiamini kuwa wamesoma kwa vile wapo askali tuliosoma nao hadi chuo kikuu?. Ni aibu na ni ukatili kuamulishwa kuua kwa makusudi na kuvunja mali za raia. Wanainchi wengi tumeanza kuaamini kuwa askali hamtumii akili. Mfano unadhihilika kwa mauaji mliyofanya Arusha na kuvunja vioo vya magari bila kutumia akili. Kumbukeni ninyi pia ni raia, mna watoto mtaani, mtaziweka hatarini familia zenu, endeleeni kufanya kazi bila akili. Mkuu wa jeshi la polisi ujue pia wewe un familia na ndg pia siku watu wakiamua utakumbuka na kujutia matendo yako!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. kama ccm inasema ina madiwani wengi mimi sidhani kama kuwa na idani kubwa ya madiwani ndo ushindi utapatikana kwao. swala pia sio wote watampa kura huyo wao watu wanaangalia utendaji pia. so huyo tendwa naona anaporojo tu. mwisho wao 2015 coz imefika mahali watu wachache wamefanya hii nchi ni yao wakati ni ya wananchi wote

    ReplyDelete
  16. wamesahau kilichofanyika jimbo la hai. walifungana kuwa na madiwani 11 kwa 11 then akashinda chadema ambapo ccm mmoja alimpigia chadema. watu wanaangalia wapi kuna ufanisi zaid

    ReplyDelete
  17. Mimi hapa ndipo wanaponishangaza wanasiasa.Chadema walisikitika kuhusu katiba hairuhusu kuonga matokeo ya urais mahakamani ndo wanataka,ila ya umeya si inaruhusu?Tatizo liko wapi?Suluhu ni kwenda mahakamani tu ndugu zangu,sisi Zanzibar tulikuwa tunaona vurugu ndo kupata haki now tumepatana nyie ndugu zetu ambao tulikuwa tunawategemeeni kwa kujifanya mnajua siasa mnatupeleka wapi?Wananchi msikubali kutumiwa kuwa ngazi ya mafanikio na wanasiasa,kuna mda lazima tutumie akili,maandamano ndo yatasaidia nini kubadilisha matokeo ya umeya?Hivi nyie watu wa Arusha mnafikiria lakini?

    ReplyDelete
  18. Nyie mnaosema CHADEMA iende mahakamani mnajua mahakama itachukua muda gani mpaka kesi kuisha unaweza kwenda mahakamani na kesi kuja kusikilizwa 2015 hii unakuwa umefanya nin na hiyo kesi itenda kwa kukata rufaa kila upande na muda ukiyoyoma na je muda wote wa kusubiri kesi inamaana hakutakuwa na ushirikiano katika shughuli za maendeleo ni bora njia zinazochukuliwa na CHADEMA kwani zitaleta suluhu kwa muda mfupi na hatimaye watu waendelee na shughuli za maendeleo kwa kushirikiana. Jaman tutumie busara katika kufuatilia huu mgogoro na kujua chanzo hasa ni nini na nani chanzo cha mgogoro.Wewe unayesema wananchi wasikubali kutumiwa kwan hao viongoz wanwatumikia akina nani si wananchi na kama wananchi hawakutaki utaongozaje na kumbuka hao viongoz wa CHADEMA wameshinikizwa na wannchi kwenda kwenye maandamano kwan hao wananch pia walishinikiza maandamano kupinga matokeo ya urais lakin ni busara tu za viongoz wa CHADEMA zilizookoa.

    ReplyDelete
  19. ACHENI USHABIKI JIBUNI HOJA ALIYOTOA HIZZA KUHUSU SHERIA. NA MAASKOFU WA ARUSHA JIBUNI HILO,MUACHE KUWACHANGANYA WAUMINI WENU.

    ReplyDelete
  20. mtu anaposema tukiingiza udini eti kundi litafaidika kwa kufikiri wao wengi suala la imani ni baya sana kwani imanini moja mtu inawedhuru mia. maaskofu wavue mahoho wa hubiri siasa. mbona CUF maandamano yao ya kuwasilisha katiba yalisambaratishwa na polisi kwa mabomu lakini maaskofu hawakutoa tamko lolote ila CHADEMA ikiguswa kidogo tu Maaskofu wanakuja juu kama moto wa kifuu ni kwanini? tuache fitina hatutasalimika hata kidogo.

    ReplyDelete
  21. Mbona uchaguzi wa Spika ulifanyika Bungeni....si lazima CCM wawapigie CCM! CHADEMA (14) + TLP (1) + CCM muasi (1)= 16!
    Uchaguzi lazima.

    ReplyDelete