LONDON, Uingereza
HARAKATI za uhamisho wa mchezaji, David Beckham kuichezea Tottenham zimerejea baada ya Spurs kuanza upya harakati za kuhakikisha wanamnyakua.Mchezaji huyo wa kingereza, bado anajaribu kupata ruhusu
kutoka katika timu yake ya LA Galaxy kwa ajili ya kuicheza Spurs, wakati ambapo msimu wa Ligi Kuu ya Marekani (MLS) ikiwa imesimama.
Wakati kocha, Harry Redknapp alipowasili White Hart Lane Jumapili alisema walikuwa wamekata tamaa kwa asilimia 99, kwamba nyota huyo hawezi kujiunga nao.
Lakini baada ya kuzungumza na Mwenyekiti, Daniel Levy kabla ya mechi yao ya FA, mzunguko wa tatu dhidi ya Charlton, imeonekana kuwa Redknapp ameanza tena kumwinda mchezaji huyo.
Alisema: "Inaweza kutokea. Mazungumzo yanaendelea."Becks mwenye umri wa miaka 35, leo atapimwa afya katika uwanja wa mazoezi wa Spurs karibu na eneo la Chigwell na kesho atafanya mazoezi rasmi.
Moja ya kizuizi kwa Tottenham, ilikuwa ni bima ya mchezaji huyo kwa kucheza mechi.Tatizo jingine kwa Tottenham, kumsaini Beckham ni idadi ya wachezaji wake wa kucheza Ligi Kuu.Idadi inayotakiwa ni wachezaji 25 na majina hayawezi kubadilishwa tena, baada ya Januari 31 mwaka huu.
Hii ina maana kuwa kama Spurs itamjumuisha Becks na kurejea Galaxy katika kipindi ambacho Ligi ya MSL inaanza Machi, italazimika kuwa na wachezaji 24 kwa kipindi kilichosalia.Kwa sasa Galaxy inasisitiza kuwa Beckham, lazima arejee Marekani ifikapo Februari 10, mwaka huu.Hiyo ina maana kuwa kama atasainiwa basi ataweza kucheza kama mechi tano kwa Spurs.Italazimika kumlipa mshahara wa pauni kama 65,000 na Galaxy pia inaweza kutaka kulipwa fidia.
Pia Spurs italazimia kuomba kuchapa na kuuza jezi zenye jina la Beckham.Lakini Redknapp alisema: "Si kumsaini kwa sababu ya jezi ni kuhusu soka."Beckham alisema: "Ninamshukuru Harry Redknapp kwa kunipatia nafasi ya kufanya mazoezi pamoja na timu yake hadi mwezi ujao."
No comments:
Post a Comment