*Makamba asema suluhisho la Arusha ni kortini
Na Gladness Mboma
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Yusufu Makamba ameibuka na kusema Meya wa Manispaa ya
Jiji la Arusha Bw. Gaudence Lyimo hataondolewa madarakani kwa maandamano wala sala, bali kwa utaratibu wa kisheria.
Bw. Makamba alisema hayo jana, ikiwa ni siku sita tangu wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waandamane mjini Arusha kupinga uchaguzi wa meya huyo, hatua iliyosababisha polisi kuvunja maandamano hayo na kuua watu watatu kwa risasi, na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.
Kiongozi huyo wa juu wa CCM, alikuwa akijibu madai dhidi yake yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe kuwa ndiye chanzo cha vurugu na mauaji ya Arusha, kutokana na kupuuza ushauri wa Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa.
Hivi karibuni Bw. Lowassa alishauri vyama hivyo vikutane na kukaa meza moja kujadili sakata la umeya ili kuepusha jiji hilo maarufu kama 'Geneva of Afrika', likifananishwa na mji wa Geneva nchini Uswis, unaosifika kwa amani, lakini Bw. Makamba alipuuzia ushauri huo na kutamba kuwa hakuna sababu ya mazungumzoa kwa kuwa chama hicho 'kimeshashinda umeya'.
Vyama hivyo viwili viliingia katika mgogoro wa kiti cha umeya baada ya CCM kumchagua Bw. Lyimo bila kuwashirikisha madiwani wa CHADEMA, huku diwani kutoka Tanga, Mary Chatanda, akiruhusiwa kupiga kura kinyuje na taratibu.
Tayari Diwani wa TLP, Bw. Michael Kivuyo aliyechaguliwa kinyemela kuwa naibu meya amejiuzulu wadhifa huo, akidai hawezi kuongoza eneo ambalo limemwaga damu kwa sababu ya wadhifa huo uliopatikana kinyume cha taratibu.Lakini Bw. Makamba alisisitiza jana kuwa uchaguzi wa meya Arusha haukusimamiwa na CCM na wala haukutangazwa na chama hicho, bali ulisimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha ambayo ndiyo ilitangaza matokeo.
"Mbowe anasema kuwa mimi nilipuuzia ushauri wa Lowassa wa kutaka CCM na CHADEMA wakae meza moja, kwani sisi tuna ugomvi na CHADEMA hadi tukae meza moja! Wanaokaa ni wale wenye ugomvi.
"Kama ni uchaguzi wa meya haukusimamiwa na CCM, bali ulisimamiwa na Jiji la Arusha na ndio waliotangaza matokeo," alisisitiza.Alisema kuwa uchaguzi ukimalizika asiyekubaliana nao au kutoridhishwa na matokeo anatakiwa kwenda mahakamani na siyo kupinga kwa maandamano na kusababisha vurugu na vifo.
"Mbowe na wenzake ndio chanzo cha vurugu na mauaji Arusha na walaaniwe, kwani walikatazwa kufanya maandanamo hawakusikia kwa kuwa walitegemea mauaji na vurugu," alisema.
Bw. Makamba alisisitiza kwamba meya aliyepo sasa, Bw. Lyimo hataondoka kwa maandamano wala sala kama ambavyo wanafanya CHADEMA na watu wengine, bali ataondolewa na utaratibu wa kisheria.
Kuhusu kujiuzulu kwa Bw. Kivuyo wa TLP, Bw. Makamba alimpongeza kwa uamuzi huo na kudai kuwa aliomba mwenyewe kuchaguliwa na ameamua kujiuzulu, ni haki yake.
"Tunampongeza Kivuyo, uchaguzi mwingine utafanyika na atachaguliwa naibu meya mwingine, kwani tunamwamini mkurugenzi aliyetangaza matokeo ya umeya," alisema.Alisema kuwa kama CHADEMA hawakuridhika na matokeo hayo ya umeya wangeenda mahakamani kama ambavyo walifanya majimboni badala ya kuandanama na kuleta vurugu.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Vunjo kupitia tiketi ya TLP, Bw. Augustino Mrema amempongeza Bw. Kivuyo kwa uamuzi huo, na amewataka viongozi wengine wa siasa na serikali waliosababisha vifo na vurugu nao kujiuzulu.Akizungumza kwa njia ya simu akiwa jimboni kwake jana, Bw. Mrema alisema kuwa amefurahishwa na uamuzi wa kijasiri wa Bw. Kivuyo wa kukubali kuwajibika na kusisitiza kwamba hiyo ndiyo demokrasia.
"Ingekuwa viongozi wote wa nchi hii tunaguswa kama Kivuyo ubabe na vishindo vinavyoendelea kwa baadhi ya viongozi visingekuwepo, ninamsifu sana," alisema.Alisema kuwa kulaumiana kwa sasa hakusaidii kitu chochote na badala yake kinachotakiwa ni kuangalia athari za vitendo vya umwagaji damu vilivyotokea na kuwataka viongozi kuona aibu kwa sababu wanaifikisha nchi pabaya."Viongozi waliosababisha mauaji na vurugu wajiuzulu kama alivyofanya Kivuyo, waone aibu wasing'ang'anie madaraka," alisema.
Viongozi aina ya Makamba ni hatari sana. Badala ya kupooza machungu yaliyotokana na maafa yaliyosababishwa na serikali isiyothamini uhai wa raia wake inayoongozwa na chama chake, yeye anachochea moto kwa kutoa kauli zenye maudhi.Matamshi yake mengi yamekuwa na maudhi sana. CCM wasipoangalia, Makamba atachangia sana kukipeleka chama hicho kaburini. Wasifikiri kwamba watatawala milele.Watanzania tumechoka kunyanyaswa.
ReplyDeleteMakamba umekosa staha,heshima,huruma,haya,na udhabiti wa uongozi kwa watanzania.Utawezaje kutamka maneno kama hayo? Ujasiri huo umeutoa wapi? Nani anaendelea kukuweka kwenye wadhifa wako huo? Hata TLP WAMESHTUKIA MCHEZO WENU MCHAFU...mtabaki peke yenu.Haooo! hata aibu hawaoni...kama Laurent Gbagbo tu!Sasa tuone kama mtafanya tena Uchaguzi wa Naibu Meya baada ya kujiuzuru Bwana Lyimo.Tatizo lenu CCM ni kuwa hamsomi alama za nyakati.Hampendwi Arusha....mnataka watu wafanyeje sasa? Mapenzi hayalazimishwi Makamba!!!
ReplyDeleteSahihisho:aliyejiuzuru ni Naibu Meya Ndugu Michael Kivuyo wa T.L.P.na si Gbagbo wa Arusha:Gaudence Lyimo wa CCM.
ReplyDeleteMheshimiwa Makamba na viongozi wa CCM wa Arusha chungeni sana kauli zenu,mimi naungana na Tamko la Maaskofu moja kwa moja walilotoa kuhusiana na mauaji na maandamano yaliyofanyika Arusha,kwa mara ya kwanza angalau nimewasikia nao wakiisema Chadema kuwa haiwezi kukosa lawama katika hilo,haya ni matamshi yanayotia moyo sana kutoka kwa viongozi wa dini,maana kauli zao mwanzoni zilitia shaka sana,la muhimu mlitakiwa mtafakari kabla ya kuanza kuwaambia wavue majoho,kwani kauli yao haikua na tatizo,ilikuwa ya kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa raia,ni vyema mtafakari maneno yenu kuliko kuona kulumbana ni jambo jema. Tatizo la Meya Arusha liwekwe wazi,aktiba inasemaje kuhusu wanaoruhusiwa kupiga kura? kisha liamuliwe jambo la msingi. huo ukubwa mnaougombania wanasiasa utamaliza watu
ReplyDeletemakamba umezeeka hata mawazo yako
ReplyDeleteSikio la kufa halisikii dawa. CCM ni sikio la kufa, so dawa zote zinazotolewa kwake sasa ni kazi bure. Tutarajie kifo chake hivi karibuni. Mwenyekiti wake, badala ya kusuluhisha matatizo, tangu mwaka uanze yuko bize na tafrija. Mara mwaka mpya kwa mabarozi, mara birthday ya Msuya etc
ReplyDeleteNaungana na kauli zinazosema waliosababisha vurugu hizo, kwa upande wa serikali na vyama vya CCM na Chadema wajiwajibishe kama alivyofanya naibu meya. Cha kushangaza ni kuwa mbona hakuna anayewanyoshea kidole viongozi wa Chadema? Hawa viongozi vitu wanavyofanya havikubaliki na inabidi vilaaniwe vikali. Haw watu wameonyesha kutokomaa kisiasa tangu uchaguzi uishe. Watanzania wenzangu siyo kila lifanywalo na serikali si sahihi na vyama vya upinzani ni sahihi. Hawa viongozi wa chadema wanaipeleka nchi pabaya. Kwa mfano, ilikuwa na maana gani kwa Slaa kuwaambia watu waende Polisi kuwatoa viongozi waliokamatwa? Alijua aina ya watu aliokuwa anawaambia kwenda kufanya fujo. Ukiangalia kwenye picha utaona wengi wa walikuwa wanaandamana are people who have nothing to loose. Chadema inawatumia hawa watu for selfish gains. It has to do with kuwa na uchungu na nchi. Tunawajuwa hawa ni watu wa aina gani. Hawa watu waliotumwa na Slaa kwenda kuwatoa viongozi hawakwenda kwa amani! Fikiria wewe ungekuwa ni polisi ungefanyaje? Hawa watu walikuwa tayari kuua, polisi nao ni wanadamu wanaoogopa maisha yao. Polisi hawakwenda na kufyatua risasi katik umati wa watu waliokuwa wakinadamana kwa amani. Viongozi wa Chadema (Hasa Slaa) wana kesi ya kujibu. Ni lazima tujenge ustaarabu wa kukemea vyama vya upinzania pia pale wanapokosea, kama maaskofu walivyofanya kwa kusema chadema nao wamekosea. Kwanini hawakuendesha magari yao mpaka uwanja wa kufanyia mkutano kama polisi walivyoagiza? Inawezekana Said Mwema alitumiwa na serikali kama baadhi wanavyodai, lakini pia inawezekana alikuwa na sababu ya kweli kuzuia maandamano. Wakati mwingine ni vizuri kuwapa Polisi benefit of the doubt, maana you never know. polise wana taarifa ambazo sisi watu wa kawaida hatuwezi kuwa nazo. Kwa nini Chadema wanataka kupambana na serikali kwa kila kitu kama sare zao zinavyoonyesha? Chadema wanabehave kama vile nchi haina rais wala serikali. They are not above the law.
ReplyDeleteWe anony January 9, 2011 10:56 PM ; acha kuandika utumbo humu..who is above the law CHADEMA au CCM ?? nani amekuwa akivunja kanuni na sheria zililzopo.?? fuatilia source ya mgogoro ndo uongee sio unakurupuka tuu!! Kama Makamba ambaye akili zake zipo nyuma kuliko umri wake.
ReplyDeleteCCM ndo chanzo cha vurugu na mauaji yote ya Arusha, DAMU ILIYOMWAGIKA ARUSHA IIJUUYAO, HAIJAENDA BURE!! CCM walifanya uhuni kuvunja kanunu=i na uchaguzi wakampachika meya wao.. NAKWAMBIA HII, WALICHOPANDA CCM KWA WANANCHI WA ARUSHA NA TZ KITAENDELEA KIZAZI NA KIZAZI ,LABDA TU WATUPE HAKI YETU!
MADAU, A-TOWN
Inasikitisha kuona katibu mkuu wa chama tawala kutoonesha kutosikitishwa kabisa na mauaji ya raia yaliotokea Arusha badala yake kuendelea2 namalumbano ambayo sidhani kama yanatija kwa Taifa hili...kweli we have a long way 2 go
ReplyDeleteNILISEMA SIKU ZA NYUMA,MAKAMBA HAFAI HATA KUWA KATIBU WA MTAA! UPEO WAKE WA KUELEWA NI MDOGO SANA....MATATIZO YOTE YA NCHI HII NI MAKAMBA KUANZIA CCM MPAKA SERIKALINI...ENZI ZA PHILIPO MANGULA KULIKUWA HAKUNA UJINGA WA NAMNA YA MAKAMBA.
ReplyDeleteULAANIWE MAKAMBA UKOSE AMANI KABISA TENA HUNA SIKU NYINGI CCM TUTAKUTEMA TU UNAFURAHIA WATU KUFA DAMU YAO IWE JUU YAKO MAANA UNAPINGANIA NA SERIKALI YAKO MWENYEWE WEWE WA OVYO SANA
ReplyDeleteTUMESIKIA MENGI KUTOKA KWA MAKAMBA, NA JUMLA YA KAULI ZAKE NI KUWA ANAHITAJI MSAADA WA MUNGU.
ReplyDeleteMimi ni Muislamu safi tena wa suala tano. NInamwomba Makamba asitumie kitabu Kitakatifu cha Biblia kulaani mauaji yakiyotokea Arusha. Kwanza mwenzangu Makamba ni Muislamu mwenzangu. Sasa ninamwuliza kwa nini asitumie Koran kulaani na badala yake anatumia Biblia? Huu ni uchokozi fika. Makamba huna uchungu na uhai wa wananchi. Mbona wewe ulionewa huruma ulipomchakachua mwanafunzi wa kike wa shuleni kwako enzi zile? Au umesahau?
ReplyDeleteNdiyo Tanzania aliyotuachia Mwalimu Nyerere hii, nchi ya kuuana, Ubabe, dhuluma, Unyanyasaji ukabila, udini, na maovu mengine mengi. Issue hii ya Arusha Makamba anaona kabisa ina msukumo wa Kidini kwa sababu tu Maaskofu wamekemea ili hali yeye si dini yake!
ReplyDeleteWapo Mashehe wanaumia, hawalali kuona kwa nini Tanzania tumefikia hapa?! Wanakemea na kumlaani mtu yeyote yule kama Makamba lakiniwao pia kama maaskofu wana imani serikali itaingilia kati kwa hekima kuliangalia hili kwa mapana ili lisitokee tena.
Makamba hawezi waambia Maaskofu kuwa Meya hataondolewa kwa sala. Hii ni kukebehi dini ya wenzako. Na Tanzania hatujafika huko. Sisi kizazi kipya hatutaki kuona Mtu kama Makamba na wenzake ssrikalini waanaisaidia Serikali kutupeleka huko kwa uvivu wa kufikiri na kuamua na hasa maslahi ya chama na ubinafsi.
Maaskofu kama viongozi wa kiimani hawawezi kujitenga wanapoona maovu, mauaji na utovu wa sheria ukisheheni wakakaa kimya. Sisi kama waumini tutawashangaa na pengine hata watanzania wote kuwadharau kwa kushindwa kukemea maovu ndani ya Nyumba ya Mungu. Tanzania ni nyumba ya Mungu ambayo Viongozi wetu wa Dini zote wamekabidhiwa kuihifadhi, wakiwemo viongozi wa serikali.
Wahenga walisema ukikosa la kusema kukaa kimya nako ni busara!
Ukweli ni kwamba kwa matamshi ya Makamba ya kudai CCM imeshinda umeya Arusha na ambaye hajaridhika aende kotini sio kuandamana ni wazi kabisa pasipo na shaka kwamba zile sababu za kiitelenjesia IGP Mwema alizozitumia kupiga marufuku maandamano alizipata kwa Makamba. Inasikitisha kuona Mbayuwayu (IGP Mwema) kupewa ushauri wa kipumbavu na kong'ota (Makamba)bila ya kuchanganya na akili yake akabamiza mdogo wake kwenye mwamba. Hivi Mwema si bora angejiuzuru kuliko kutekeleza ushauri wa kijinga wa kuzuia maandamano kwa kutumia vyombo vya habari? kila mtu nchini anamheshimu sana Mwema kwakuwa ana sifa za kimataifa (interpol) hivyo kuonekana msomi na mweledi kuliko IGP aliyepita, kilichomshinda kutumia akili zake kunusuru maisha wa watanzania wenzake, wadogo zake, wapwa zake, shemeji zake na hata wototo wa rafiki zake ninini? Makamba atakuwa chanzo cha vita nchini tumchunge sana kuanzia leo na kuendelea
ReplyDeleteEeh! Hapa sasa ndio tunaona umuhimu wa Phillip Mangula! Kwa kumuacha mangula CCM walichemka sanaaaa! Unajua Uzee ni hekima na busara, na sasa nimeamini sio kila mzee ana busara! Ni bora mhe Makamba angekaa zake kimya kuliko kuongea kwa jazba tu bila kutafakari ya siku zijazo! Eee mwenyezi Mungu Mpe hekima mzee wetu huyu aweze kutafakari kabla ya kusema! Amen
ReplyDeleteWe unayejiita Dr.Anderson we dr wa kuuza mandazi au wa kusukuma mikokoteni? maana unarukia hoja tu bila kuwa na trend ya suala zima la Ars.Kauze mandazi huko usituletee usiku!
ReplyDeleteHivi mlikuwa wapi pale jeshi la polisi lilipowauwa wapemba zaidi ya 21 kwa sababu zinazolingana?
ReplyDeleteInaniwia taabu kuamini kama kuna harufu ya udini lakini kukurupuka Maaskofu kulaani kitendo cha fujo na vurugu na kukaa kimya walipouliwa wapemba, inanipa wasiwasi.
Hivi ni kwa sababu wakati ya mauaji ya Pemba Rais alikuwa Mkristo na sasa Rais ni muislamu?
Tuepushe shari. Na njia bora ni kuwa Mbowe na Slaa wajiuzulu kwa kuwahadaa wafuasi wao na kuwaingiza kwenye matata kiasi cha baadhi kupoteza roho.
Nchi tunaipeleka pabaya. Hatari mti na macho
nyie Chadema kwa mtindo huu mtaua watu wengi sana,kwanza mnadanganya watanznia kuwa mnauchungu sana ni uongotu,nyinyi ni wakabila chama chenu ni ukabila tu,kwanini fujo hizo Arusha tu igini mifano mizuri ya Zitto kabwe,hashabikii kumwagika Damu za watu mnataka umaarufu kwa kumwaga damu tabia hiyo ni mbaya sana msirudie tena Sisi watanzania wa ukweli hatutaki,ingawa kidogo mmefanya vizuri kidogo kumchukua mkenya na kumwingiza kwenye maandamano ili awe chambo ilia msirudie tena
ReplyDeleteharafu we padre nikatta wa jimbo kuu la Songea mbona unafurahia sana Damu za watu kumwagika harafu unajiita mtumishi wa Mungu siyo vema hata kidogo,mkumbuke mauaji ya kimbali kule Rwanda kanisa katoliki lilihusika na tumeshuhudia Mapadre na maaskofu wakifungwa katika mahakama ya kimataifa ya aicc Arusha haujifunzi Padre wewe usiye na haya?
ReplyDeleteMakamba mnamuonea bure! Kama busara iwapi ile ya viongozi wa CHADEMA wanapokataa mazungumzo na Serikali. Hili mlio wengi halioni kwa vile hamtaki Viongozi wa CHADEMA wabebe lawama.
ReplyDeleteCHADEMA wanabeba lawama kwa kuwatowa muhanga wananchi waliouwawa. Kwani si tunajuwa Sheria za nchi zilivyo? Si tunajuwa maamuzi wa maasari wetu wanapotekeleza sheria hizo? hivyo matokeo kama ya Mwembechai , Pemba na Unguja hayakutosha kuweka tahadhari kwa viongozi wa CHADEMA?
CHADEMA walifanya kwa makusudi kuwatowa muhanga watu ili wawe na njia ya kuipressure Serikali lakini karata haikuwa kama walivyotegemea.
Mnataka busara kutoka kwa Makamba na mnasahau kuwa kanisa linakosa busara kuingilia mambo ya uchaguzi. Kanisa lina haki ya kulaani vurugui na mauwaji ya Polisi lakini halina haki ya kujiweka upande mmoja wa mgogoro kwani kufanya hivyo ni kusababisha kuambiwa ukweli (kuvua majoho)lakini kinageuzwa na kuonekana ni matusi. Nini unategemea unapoingia katika vita na kusaidia upande mwengine huku ukitegemea upande wa pili kukupongeza. Makamba yuko sahihi na anaewzea kupinga hoja zake afanye hivyo kwa hoja si kumtukana.
Makamba tunakuheshimu kiongozi kama wewe huwezi sema naneno kishenzi kama hayo naunajua watu wameuwawa tumia akili kama mwanasiasa aliye komaa kisiasa mimi ni mwanaccm damu,Lakini kauli zako si za busara naomba chama changu cha ccm kiangalie swala hii kiundani ilisije likatupeleka pabaya.Huyu makamba kila siku mojungu tu badala ya kuendeleza chama nimwakati wakutafuta mapungufu ya chama na kujenga nchi,Sisi wanaccm nikipindi cha kujiuliza wapi tumekosea tulekibishe si wakati wa malumbano.Makamba acha ujinga
ReplyDeleteKwanini CCM wanaogopa maandano kuliko mahakama? Jibu ni rahisi, mahakama zetu sio huru, anayeteua majaji woooote nchini ni mwenyekiti wao wa CCM taifa, hivyo ni sawa na kesi ya nyani kula mahindi kumpelekea ngedere akaamue. Maandamano yanaogopewa na serikali zote kandamizi duniani, maana ni maandamano nyenye nguvu ya kukusanya watu iliwaende wakakusanyike pahala ili wajulishwe ukweli halisi wa mambo, matukio na ubaya wa watawala.
ReplyDeleteKamwe msikimbilie mahakamani, hamtapata kitu huko, kimbilieni maandamano na mikutano ya hadhara sio mahakamani, ona kesi ya mgombea binafsi ya mch. Mtikila ilivyoamuliwa na mahakama ya juu, ona dowans, ona kesi ya mzee wa vijisenti ya kuua, ona, ona, ona,.........
Ndiyo maana makamba na wenzake wanataka muende mahakamani ili mkakatwe shigo zenu kwa panga butu la wateule wa mwenyekiti wao wa CCM.
Maandamano ndiyo mwiba wa madhalimu, andamaneni hadi mfe wote, sio kwenda mahakamani mtavuliwa kwa nyavu zenye rangi ya kijani huko.
HIVI HAWA WATU WANAONONGONA KUHUSU MAASKOFU NDIYO KWAMBA MJI WA ARUSHA UNATAWALIWA NA DINI YA MAASKOFU?AU NI UJINGA WA KUTOONA MBALI NDIYO MAANA WANADHANI SERIKALI INAENDESHWA KAMA TOYO?TUMIENI AKILI,KUNA USEMI UNASEMA YA MUNGU MPE MUNGU YA KAISARI MPE KAIZARI ,WALIOANDIKA HAYO SIYO WAJINGA KIASI HICHO MNACHOFIKIRI NYIE.HAO MAASKOFU WENU NI WA DINI YENU SIO WATAWALA WA NCHI HII.HAYO MAMBO WANAYOFANYA WANATAKIWA KUFANYIA HUKO HUKO KANISANI NA SIYO KWENYE VYOMBO VYA HABARI KAMA VILE WANASIASA WALE AMBAO HAWANA BUSARA.UWEZI KUSEMA ETI UMTAMBUE MEYA.WEWE ASKOFU TANGU LINI AKACHAGUA MWANA SIASA MPAKA USEME UMTAMBUI?KAMA WANGEKUWA NA BUSARA WANGEJUA HAKI MARA NYINGI INAPATIKANA MAHAKAMANI NA SI KUCHOCHEA WAUMINI WAO KUFANYA VURUGU KWA KUWA ETI MTU WAO WANAOMPENDA MAASKOFU WAKISAHAU WAO NI WACHUNGAJI WA WAUMINI NA SI WASEMAJI WA SERIKALI,AU WANA SIASA.
ReplyDeleteFANYA YA KANISANI WACHA YA WANASIASA WAFANYE WANASIASA.
Mh.Makamba akapimwe kichwa chake,nina wasi wasi anaugonjwa wa akili.Je?angekuwa January ameuwauawa je?asingelaani mauaji hayo?Mungu amsamehe kwa maana hajuwi alitendalo.Ninaomba sana Mh.JK mpeleke makamba akapimwe kichwa ambacho kimeharibiwa na madaraka ya CCM.Istoshe CCM haitatawala milele.Hakuna marefu yasio na ncha na kila kitu kina mwanzo na mwisho.Ninaamini Mh.Makamba atalipwa hapa duniani kwa kashfa zake za kipumbavu.
ReplyDeleteKWA KAURI ZA CCM, VITA SASA VIMETANGAZWA RASMI
ReplyDeleteNdugu yangu Makamba, achana na mambo ya kuropoka, ni vyema ukatafiti kujua chanzo cha tatizo ndio uzungumze. Nilitegemea kutokana na umri ulio nao utumie ushawishi, hekima na busara kufanya utatuzi. Hivi na nyie CCM hamuoni hilo? au ni walele. Makamba umeshindwa kupigania haki za watanzania na sasa unabwatuka maneno yasiyokuwa na mvuto! Unadhani ukatibu mkuu wako utakupeleka mbinguni? Wako wapi leo waliokuwa wanatafuta mali kwa ubabe? wa kina Mabutu, Jonas Savimbi, John Ngarang? Makamba Mungu akuponye ugonjwa wa akili tena uenda wazimu ulionao...
ReplyDeletekwa sasa mimim nimekosa imani na chama cha mapinduzi, kuanzia kwa mwenyekiti wake hadi kamati na halmashauri kuu ya CCM. Siwezi kuamini kinachofanyika sasa kwenye CCM. Haiwezekani watu wanauawa na polisi halafu katibu mkuu wake anashangilia. Makamba siyo tu sasa amezeeka, bali akili imechoka na ameshakuwa mwendawazimu, Haiwezekani mzee mzima ambaye tulitegemea angekuwa na busara, lakini tunashuhudia kuwa hamna kitu ndani mwake anaropoka maneno yasiyokuwa na hekima hata kidogo. Na sielewi anajiamini nini. Dhambi inayoendelea kuifanya CCM nina uhakika muda mfupi ujao Watanzania wataanza kuona. Malipo watayapata hapahapa. Kumbuka walikuwepo akina Idd Amini na Mobut Sesesko walikufa kwa aibu. Makamba na viongozi wengine wanaofanana na hao mtapata adhabu hapahapa duniani.
ReplyDeletemapadiri wa katoliki muone aibu sisi waumini wenu tunaona ni sahihi kuhubiri badala ya kuwashabikia wanaotaka watanzania kupoteza amani iliyojengwa kwa muda mrefu vinginevyo vueni magwanda ya kanisa mje majukwaani kwenye siasa nakuomba kadinari wetu kemea hilo kama kweli unampenda mungu nasi waumini wa kanisa tuwe na imani nanyi uchaguzi umeisha na ccm ndio mshindi tufanye kazi ch
ReplyDeletembowe na wenzako mnapaswa kujiuzulu kwani mauwaji hayo bila wewe na viongozi wenzako wa chadema kukiuka taratibu na sheria za nchi yasingetokea ni kweli mbowe umewahi kugombea hata urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania hujui kama huridhiki na mwenendo wa uchaguzi unapaswa kwenda mahakamani? na sio maandamano?umeona sasa umepoteza maisha ya watu bila sababu mimi charles mhagama
ReplyDeletendugu yangu mbowe nilifuatilia sana mdahalo wenu kati ya CUF na Chadema ndugu hamadi Rashidi alisema namnukuu"mimi ni mwanasiasa mkongwe usinijalibu napia Cuf ilikwisha poteza watu 26 katika machafuko pemba yaonesha kauri hiyo ilikukwaza sana hivyo umeamua kumwaga damu za watu 3 ili mkikutanatena kwenye mdahalo kama ule uwe na hoja ya kujibu.kuwa wewe Chama Chako kimepoteza watu nakushukuru kwa kuonesha wewe ni mkatili kwa vitendo
ReplyDeletenampongeza katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Bi Mery Chatanda kwa kuwapa ukweli maaskofu wa kanisa katoliki kwani tulizani ni viongozi wa dini kumbe ni wanasiasa wenzetu waliojificha chini ya msalaba nawakumbusha ya kwamba yatakapotokea machafuko mtajikuta nanyi mnafikishwa kwenye mahakama ya kimataifa kama wenzenu wa Rwanda au hamjui, pamai
ReplyDeletenanyie CCM acheni kulalamika nayi nendeni makanisani mkavae majoho muanze kuhubiri mapadre na maaskofu wao waache tabia mbaya za ufuska,chuki,ukabila,udini na mengi mabaya watawaelewa tu
ReplyDeleteKauli ya maaskofu kuwa hawamtambui Meya si sahihi. Hawakupaswa kutoa kauli hii. Hii ni kushabikia upande mmoja. Ukiangalia Arusha CCM wana madiwani 16 na Chadema wana madiwani 14 kwa hizi hesabu inaonyesha CCM wanapaswa kutoa Meya. Chadema walijua hilo ndiyo maana walianza kuvuruga ili ionekane walionewa na kuamua kutoshiriki. Sasa mlitaka mkurugenzi afanyeje? Chadema wameonyesha kutokomaa kisiasa. Wanataka kuingia madarani kibabe. Leo hii hata uchaguzi ukirudiwa lazima atachaguliwa meya kutoka ccma sababu wana madiwani wengi. Sasa maaskofu wanapoamua kutomtambua meya wanaamini madai ya chadema au wamefanya utafiti. MAKAMBA YUKO SAHIHI SWALA LA UHALALI WA MEYA WA ARUSHA LITAAMULIWA NA MAHAKAMA. CHADEMA WANAPASWA KWENDA MAHAKAMANI SIYO KUANDAMANA. NYIE MNAOWATETEA CHADEMA SIWAELEWI. SASA BAADA YA KUANDAMANA NINI KINAFUATA? Naomba mnaotetea njia hiyo mnijibu. Nyinyi mnaotetea vitendo vya chadema siyo wastaarabu. Mbona mnatukana wengine? Au ndiyo aina ya watu wanaoshabikia chadema? Msitukane toeni hoja. Na viongozi wenu wako kama nyinyi ni kutukana na kupambana. Wewe angalia hata mavazi yao, ni ya kijeshi. Siasa siyo mapambano, ni kujadiliana na kufikia muhafaka. Gazeti la Majira limetupa ukurasa huu kuchangia mawazo siyo kutukana wengine. Kwa nini mnavyofikiri nyinyi ndiyo mnaona tu ni bora kuliko mawazo ya wengine. Mnaongea kama vile wafuasi wa chadema ndiyo uma wa Tanzania. Kumbukeni pia CCM ina wafuasi wengi. Wakiamua nao kuja mitaani kweli tutakuwa na nchi? Kama alivyosema Dr Anderson, Slaa ana kesi ya kujibu. Kwanini aliwatuma vijana kwenda polisi kuwatoa viongozi wa chadema? Hii kweli ni sahihi? ANACHOSEMA MAKAMBA NI SAHIHI SULUHISHO LAZIMA LIPATIKANE MAHAKAMANI SIYO MITAANI. CHADEMA MKIENDELEA KUPELEKA WATU MITAANI BILA UTARATIBU WATAKUFA WENGI. POLISI WAPO KWA AJILI YA KULINDA USALAMA WA RAIS WENGINGE. YEYOTE ANAYEFANYA UHUNI HATA KAMA NI KWA JINA LA SIASA ATASHUGHULIKIWA.
ReplyDeletemaaskofu mnaacha kushughulikia maadili ya kanisa mnaingia kwenye siasa mbona mapadre wengi wana watoto na matokeo watoto wa mitaani ni wengi hamchukui hatua kwa nini?nataka mnijibu haraka
ReplyDeletekweli nimeamini wahuni ni wengi CHADEMA
ReplyDeleteBURE MNATOANA MACHO.TOKA LINI MCHAGA AKASHANGAA MTU KUFA AU KUUA KWA AJILI YA MALI? UGOMVI HAPO NI BIASHARA YA KUKAMATA HAZINA YA SERIKALI KATI YA CCM NA WAFANYABIASHARA WAKE NA SLAA NA WACHAGA WAKE. AMKENI. SLAA,MBOWE,NDESAMBURO,SELASINI NI WATU WA KUPELEKWA MAHAKAMA YA KIMATAIFA KWA KUCHOCHEA VURUGU MPAKA WATU WAKAPOTEZA MAISHA,NA NYIE MANAOSHABIKIA WATU HAWA MSIFIKIRIE MAHAKAMA YA KIMATAIFA NI KISUTU AMBAO WANAMUANGALIA SLAA AKIVUNJA SHERIA YA KUCHUKUA MKE WA MTU NA KUTAMBA NAYE KWENYE VIWANJA,HUKO HAMNA ASKOFU WA KUIKEMEA CCM SAA ZOTE HUKO NI SHERIA TU.HAWA WACHAGA WANAUA BABA ZAO ILI WAPATE MALI SEMBUSE HAO WALIOKUFA ARUSHA? HATA NYIE MAASKOFU CHUNGENI KAULI ZENU SANA MSIJE MKAJIKUTA KAMA YALIOWAKUTA RUANDA.NA WEWE KIMADA WA SLAA UNAMTANGAZIA NANI KWAMBA WEWE NI MJA MZITO,UNAFIKIRI NI SIFA HIYO KUZAA NJE YA NDOA? YANAYOKUFIKA NI LAANA YA MUMEO NA BADO YATAKUFIKA MENGI,HATUTAKI KUWA NA FIRST LADY WA TYPE YAKO.
ReplyDeleteNdugu wapendwa wafiwa na wote waliopatwa na matatizo ya kupigwa risasi na waliojeruhiwa kwa namna moja au nyingine ninawapa pole na mungu atawasaidia.
ReplyDeleteKwa hali ilivyo CCM ni ngumu na inaonyesha jinsi kila mtu anavyojichukulia sheria mkononi. Huyu Chitanda anaewadhalilisha maaskofu sijui anajiamini nini? Akumbuke hicho ni cheo tu na kina mwisho lakini unawasumbua watanzania wengi kulika kumfurahisha Makamba na wakumbwa wako. Akumbuke huyu Askofu ameweka mkataba maishani mwake milele kutokana na dhamira yake ya maisha yake.
Mchunguzeni huyu Chitanda inawezekana hata hilo jina analotumia sio la kwake. Kama angekuwa ni muumini mwenye imani asingesema hayo maneno makali hivyo. Ninachotaka kumwambia huyu mama eti hayo mavazi anayoyaona ya kuwa yanamkera aliyatumia huyo tunae mwamini na alitumia mavazi hayo hayo kuleta amani duniani. Ndio maana wakristo wanatumia na waislam wanatumia.
Lengo la maaskofu lilikuwa ni nzuri na nguvu yake ni kuleta amani kwa pande zote mbili kwa kweli. Sasa kama CCM ina uhakika kuwa ilishinda kihalali kwa nini isikubali huo uchaguzi ukarudiwa na wakaendesha hii manispaa kwa amani bila manunguniko yeyote? Unafikiri uchaguzi ukiwekwa hadharani kuna haki itapotea tukiachana na ushabiki wa makamba na hawa wengine wanaotaka sifa. Makamba na ubabe wake akumbuke hii ni Tanzania ya amani sio Iraq. Hawezi kutawala watu ambao hawampendi kila siku kutakuwa na malumbano ambayo hayatakwisha.
Mnasema kuna vyombo vya sheria, mahakama nk, je tujiulize hawa polisi wao wanafanya kazi kwa ajili ya nani na hiyo mahakama itafanya kazi kwa ajiliya nani. Je hapa kuna haki itapatikana kama polisi wameweza kuvamia maandamano na ya amani na kutumamia silaha kali, na nguvu kubwaa kupita kiasi. Sasa tunajua tupo kwenye maombolezo .
Mimi ninashangaa huyu Rais yupo au kiti chake amemwachia makamba. Kwa sababu ninaona hoja za serikali wanajibu watu ambao hata hawahusiki. Mf Chitanda au Makamba wasingeweza kujibu ile hoja ya maaskofu kwa dharau namna hiyo. Wao waliuliza serikali hawaja uliza CCM.
Ndugu uliyozungumzia mpenzi wa Makamba wa zamani ukisema wewe ni muislamu wa sala tano, kumbuka kwamba uislamu haukubali kashfa ya aina hiyo kutangazwa Na ukitangaza sharti ulete mashahidi wanne ambao wameshuhudia zinaa ikitendeka.Ni wazima kwamba haiwezekani kuwapata mashahidi wanne au na wakipatikana ni tukio nadra. Hii inamaanisha kwamba matamshi ya aina hiyo yanachukiwa kidini. Usipokuwa na ushahidi kama huo,ole wako. Naona watu wengine hata wanamshambulia Mbowe kwa mambo kama hayo.Hii si tabia nzuri au jambo la kujadiliwa na watu wazima; ni mambo ya soni - hivyo yanafaa yafichwe. Hii ni kazi ya mahakama na wala sii shughuli ya waandishi. Kwa jumla,jamani nawasihi tuache matusi na tujadili mada zote kiungwana. Mohamed Mwendapole
ReplyDeleteIssue hapa ni kuwa Slaa na Mbowe wanataka umaarufu kwa kumwaga damu ya raia! Period!
ReplyDeleteCCM inatukana mpaka viongozi wa Dini. Chama Kisichomuogopa hata Mungu Kinaweza kumfanya mtu chochote wakati wowote. ni chama cha kukikwepa kama ukoma. Huyo Mary Chitanda sijui ni dhehebu gani? isijekuwa kachakachua majina tu
ReplyDeletetunamwomba Makamba atuachie Dini yetu ya Kikristo. Yeye aendelee na Dini yake sisi hatuna ugomvi na Dini ya Mtu.
ReplyDeleteTunamwomba aache kutumia Biblia na kutukana
Ukristo.
Atumie kitabu cha Dini yake.
Kwa kweli kutokana na maoni hapa nimeamini ya kuwa sisi waislamu hatuwapendi wakristo. Tunawakashifu sana kiasi kwamba wanafikiria kama vile wanatabia ya kufungia mabomu kiuno na kufundisha watoto ugaidi kama wenzetu wa afghanistani. Sasa sisi tumeanza kuongea na kuwakashifu, hawa wakristo wakianza kujibu hapa TZ patakalika kweli. Wewe unaemuona mwenzio hafai je wewe unafaa kwa lipi, labda kukesha kwenye mdundiko. Sisi tunapenda kuwafuatilia sana, kuiga na kubadilisha kinyume kila wanachofanya hatuwezi kubuni. Na ndio maana kuraani yetu tulikopi kwenye biblia na kubadilisha kinyume chake. Kama inafaakutumia kwa nini makamba anapenda kutumia biblia zaidi kuliko kitabu chetu. Kwa hiyo haifai. MOHAMED HUSSEN.
ReplyDeleteWote walaaniwe CHADEMA na CCM maana ukisema CCM pekee unakosea, CHADEMA wanalazimisha mambo ili waonekane watetea haki za watu, Wao viongozi mbona kwenye mkong'oto huwa hawaonekani? siku zote nimekuwa natizama maandamano naona wanaoathirika ni wavaa kandambili maskini wasiojua wakilala mahabusu watoto wao nyumbani watatakula nini. MBOWE NA SLAA wao wanakula shavu tu wanataka watembelee mabenzi ya Ikulu kwa kupitia kwa wavaa kandambili? SHIDA YAO NINI? WANATAKA URAHISI TU? au ndio wanataka kulindwa na kufunguliwa barabara wanapokuwa wanapita kwa ving'ora barabarani wasipate tabu. Mimi sioni hiyo haki wanayopigania ni haki gani wote WASANII, wakishapata huo uongozi wa nchi WANANUFAIKA WAO NA FAMILIA ZAO. Huyo Mbowe au SLAA unadhani akiwa Rais atakusaidia hata shilingi mia? Angalia Maalim Seif sasa hivi hata akienda Buguruni ulinzi wa kufa mtu amekula shavu katusahau sisi wavaa kandambili. ...... JAMANI TUACHENI HIZO NJAA ZENU MBOWE NA SLAA HAZITATUFKISHA POPOTE, MAUAJI YA ARUSHA WOTE MNAUSIKA.
ReplyDeleteMzee Makamba naona unakoenda kubaya. Sasa Meya haondoki kwa maandamano wala sala, basi nadhani wewe sio muumini wa dini yoyote na wala huamini kwamba Mungu yupo. Kama hivyo ndivyo sisi tutaendelea kukuombea kwani umechanganyikiwa sasa. Huoni hayo Madhehebu ya Waislamu na Wakristu wala huthamini michango yao katika jamii. Mungu apishie mbali unakotupeleka siko. Sasa Mzee unapotupa mifano yako mingi kwa kutumia vitabu vitakatifu unatusanifu sio???? Mwenyezi Mungu mwingi wa REHEMA akusamehe na akupe muda wa toba, naamini ulikurupuka na hukujua kama umetamka maneno hayo
ReplyDeleteBwana Mohamed Hussen - ninashuku kwamba wewe ni muislamu ( kushuku pia ni dhambi !). Jina lako la pili spelling umekosea ! Pili, sijasikia maisha yangu muislamu akisema maneno uliyotaja. Haifai, na kusema kweli ni dhambi kubwa, kuleta fitina baina ya waumini wa dini mbali mbali.Tanzania tupende au tusipende tutaishi pamoja tukiwa na dini mbali mbali. Mpaka sasa tumeishi vyema licha ya kwamba tuna imani tafauti.Mimi binafsi, nina marafiki wa dhati kwa hali na mali ambao ni wakristo. Hata katika nyumba moja huenda wakawepo ndugu wenye dini tofauti. Tusiruhusu siasa kutugawanya - ikiwa tutaitikia mwito huo basi tutakuwa wapumbavu.Huwezi kugeuza itikadi ya mtu; waweza tuu kumshawishi. Kila dini inafaa iheshimiwe. Qurani inasema: " Nyinyi fuateni dini yenu, na sisi tutafuata dini yetu". Yani pawe na suluhu. Mgogoro ni wa nini.Pana yeyote aliyopewa hela au madaraka kwa sababu ni muislamu au ni mkristo ? Hamna ! Wako, Mwendapole
ReplyDeleteHivi hakuna taratibu zozote zinazoonyesha ni nani ana haki ya kupiga kura kumchagua Mayor?kama zipo hakuna mwandishi wa habari anayeweza kuinukuu na kuziweka hadharani?
ReplyDeleteMuheshimiwa makamba heshima yako inanashuka, sasa furahia maafa yalitokea Arusha kwakauli yako chafu, na kuongea kama siyo kiongoz, kama umechoka mbabu achia ngazi wenzako, mbona bado tuna viongoz wazuri tu katika nchi hii jamani????????????/
ReplyDeleteNIMEFUATA MAONI YOTE KWA MAKINI. Yangu ni kuwa Makamba ni mwanadamu na hakuna aliyekamili. Lilibora ni kuwa kwa sasa naamini neema ya Mungu itatosha kurekebisha kauli hatarishi. Mheshimiwa Chatanda pia napenda kuamini hamasa za wadhifa zimemfanya ajisahau. Lakini atambue kuwa wakuu wetu wa DINI ZOTE NI WAPAKWA MAFUTA WA MUNGU na wana wajibu wa KIROHO, KIMWILI NA KIJAMII (SOCIAL RESPONSIBILITY) kwa WATANZANIA WOTE. Kwa mujibu wa MAJUKUMU yao hawawezi kukaa kimya pale panapohitajika kauli zao HAWANA BUDI KUZUGUMGUZA, KUSHAURI na KUKEMEA bila kuengemea UPANDE WOWOTE. Hawawajibiki kumtambua kiongozi kwa kuwa tu anatoka chama tawala.KAMA KUNA NAMNA FULANI ya manung'uniko lazima wanene ili vyombo husika virekebishe malalamiko kuona YANAPASWA KUFUATILIWA siyo kuachilia WANASIASA KUTEKA HOJA. Pia swala la hisia na chuki binafsi ya kidini ISIPENYEZWE KWENYE JAMII YA WATANZANIA kwa KUFANINISHA VIONGOZI WA DINI NA YALIYOTOKEA RWANDA AMBAYO MAJIRANI ZETU wanaendelea kuyaponyesha kwa gharama kubwa ya maridhiano, na hata KUSAMEHEANA.Kauli ya utengano imekuwa ikitolewa.Sisemi Watanzania tulikuwa hatulaani mauaji ya Pemba.Jambo hapa ni kuendelea kuyaepusha.Watanzania hatuko tayari CCM ile ile ililumbana sana na CUF iingie tena kwenye MJADALA WA KISIASA na CHADEMA wa upatanisho jambo tusilotaka....litokee na kuturudisha kabisa nyuma. Umaskini upo nchini si siri na vingozi wanaunafuu wao mkubwa YET lazima tuwe na viongozi..lazima walindwe haiwezekani wawe na nafasi ya kuitisha party ya chakula au kugawa fedha kwa wapiga kura. Hapa lazima tulenge tatizo...uchaguzi wa umeya...na chuki ya chama tawala kupoteza ubunge kwa wapinzani kwa upande na Chadema kujiona inayo haki ya kuona uchaguzi wa umeja unaendeshwa kwa haki. Kama hili lilionwa mapema na kufanyiwa kazi hasa baada ya polisi kumpiga vibaya na kujeruhi Mbunge maandamano yasingehitajika na damu isingemwagika. Lazima tuone ukweli kuwa wapiga kura walipaswa wafahamishwe yaliyojiri Mbunge wao apigwe na polisi..kazi ambayo viongozi wa Chadema walipaswa wawafahamishe.Ishara za nyakati zikidharauliwa lazima wanaodai haki yao watachukua hatua bila kujali kuwa ni Chadema yao(siyo CCM) kwa sababu kiko madarakani hivyo kila kitu kwake kinaonekana shwari kwa mgongo wa chupa. KAMA tunaitakia nchi yetu AMANI YA KUDUMU CCM inayotawala ijichunguze na kuangalia dalili za nyakati wananchi wameamka wana macho ya kuona SIYO WAJINGA. Haki za kisiasa hazipatikani MAHAKAMANI ila kwa mazungumzo, kumtanguliza Mungu..Hili kama viongozi watawala wataendelea kupuuzia au kufumbia macho kwa masilahi yao..tunaowaomba wasitupeleke pabaya (sisi viongozi tunaokulia hatutaki ndugu zetu polisi waishi kwa kupewa amri wasizopenda ..za kuua ..kumwaga damu za kaka...dada...baba..wajomba zao na wengine wanaotegemewa na taifa kwa maendeleo). Viongozi watawalao sasa wajifunze somo kutoka TUNISIA wanapaswa kushughulikia HAKI ZA RAIA NA HASA KUPIGA VITA UMASKINI.
ReplyDeleteViongozi wa dini ni sehemu ya jamii wajibu wao ni wa kiroho, kimwili na kijamii (social responsibility) hivyo wanapaswa kuTOA MAONI, KUSHAURI na KUKEMEA bila kujali sura ya mtu..au kongozi wa kisiasa. Ni wote wa dini zote ni WAPAKWA MAFUTA WA MUNGU. Ninachojua viongozi wotw wanaapa kwa Vitabu vitakatifu kujua yaliyomo ndani KITANZI KWAO ili kuwa wacha Mungu. Maneno ya wanasiasa kusema waache kazi za kiMungu na kuingia siasani wajue wanaweza ila wanasiasa hamuwezi kuingia kwenye viatu vyao. Wanasiasa wanapaswa kuwa wakweli na ketekeleza wajibu wao wakiisikiliza sauti ya Mungu iwaongoze na siyo sauti ya ushabiki wa siasa na kwa mabosi wao. Inabidi viongozi wasome ishara za nyakati hizi ili kuepusha MIGOGORO ya siasa TUSIYOSTAHILI KUBEBA GHARAMA TENA kama ule wa CCM na CUF ulipoteza roho nyingi za watu. CCM hii inayotawala kuona mambo yamekuwa shwari (ombi letu la siku nyingi)na CUF Zanzibar isitupekee tena kwenye mgogoro mwingine na CHADEMA. Tangu Mbunge wa ARS Mjini polisi alipompigwa na kumizwa vibaya (CCM) haikuona kuna jambo liepushe hasira ya wana Chadema. Vyombo husika vilipaswa kurejea uchaguzi wa umeya kujiridhisha na mkakati mzima. Tukubali tusikubali lazima tuwe na viongozi wawe CCM, CUF au CHADEMA haiwezekani wasilindwe, haiwezekani wakaandaa party au kugawa pesa kuwashukuru wapiga kura. Watanzania hatuna watawala wa dini, kabila wala wafanyabiashara. Kuwanyooshea vidole kina Mbowe, Mchaga, mfanyabiashara ni kosa. Msemaji wa kauli hiyo hauko sahihi idadi kubwa ya viongozi tulio nao ni wafanyabiashara wakubwa tena wa kimataifa..funguka macho. Haki ya kisiasa haiko mahakamani...siyo jinai. Viongozi walioko madarakani wanapaswa washughulikie umaskini...la sivyo wanaoitwa wa kanda mbili watawatoa madarakani..Tujifunze toka TUNISIA ni nani walimtoa rais madarakani.
ReplyDelete