13 January 2011

Dzeko aipitia filamu ya Man City

LONDON, Uingereza

MSHAMBULIAJI Edin Dzeko, amesoma filamu ya Manchester City ya masikitiko ya kutotwaa ubingwa katika miaka iliyopita na ameahidia neema kwa kwa siku zijazo kwa mashabiki wa timu hiyo.City ilimsaini mshambuliaji
huyo wa Bosnia akitokea klabu ya Ujerumani, Wolfsburg kwa ada ya pauni milioni 27 kwa matumaini kuwa anaweza kuisaidia kutwaa ubingwa baada ya kupita miaka 43.

Jumatatu Dzeko mwenye miaka 24, aliangalia filamu mpya ya timu yake 'Blue Moon Rising' kuhusu majaribu na mateso ya mashabiki wa City.

Alisema: "Niliiangalia na ilikuwa ni filamu yenye hisia sana na niliona mambo mengi yaliyotokea katika miaka ya hivi karibuni.

"Filamu pia ilionesha watu kuishi kwa ajili ya klabu ambacho ni kitu cha kusisimua.

"Wakati nilipoona kiasi gani walivyo na upendo kwa klabu na bado hawajatwaa  ubingwa kwa muda mrefu, utii wao ni wa kusisimua.

"Na mimi nataka kuwafanya watu hawa kuwa na furaha. Nilitwaa ubingwa wa Ujerumani nikiwa na Wolfsburg kwa mara ya kwanza katika historia yao na sasa ningefurahi kupata mafanikio hayo hapa"

Dzeko alisema anafahamu upinzani uliopo dhidi ya Manchaster United, lakini anataka timu yao kupata mafanikio na kuwafurahisha mashabiki.

Alisema anaifikiria mechi kati yao ambayo itakuwa Februari 12 mwaka huu.
Dzeko anajua umuhimu wa kufunga katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, kama alivyofanya akiwa na Wolfsburg msimu uliopita katika Ligi ya Mabingwa.

Uchezaji wake ndiyo ulimfanya akatoka kucheza soka Bosnia na kuhamia Jamhuri ya Czech na Ujerumani na kufunga mabao 123 katika michezo 236.

Akiwa na Wolfsburg alifunga mabao 26, na kusaidia 10, katika mechi 32 ambapo walitwaa ubingwa wa Bundesliga msimu wa 2008-09.

Alikuwa mfungaji bora wa Ujerumani msimu uliopita akifunga mabao 22 na alifunga magoli 17 kwenye mechi 31 katika timu ya Bosnia-Herzegovina.

Dzeko alisema: "Nataka kufanya ubora wangu kuonesha watu kwamba mimi nina thamani ya fedha hii, mimi najua ni mengi lakini nina mtu ambaye anahisi shinikizo.

Kocha wa City, Roberto Mancini awali alikuwa akimtaka mchezaji huyo kuanzia majira ya joto yaliyopita, alisema anatumaini atakuwa mchezaji muhimu sana kwa klabu kwa siku zijazo.

Alisema anatumaini mchezaji huyo anaweza kushirikiana vizuri na wachambuliaji wenzake, Carlos Tevez na Mario Balotelli.

Kocha huyo alisema ni mchezaji mwenye ubora, uzoefu na anaweza kucheza katika mfumo wowote na kumwelezea kuwa ni mmoja kati ya washambuliaji wazuri waliopo Ulaya kwa sasa.

Jumamosi City itacheza na Wolves, ambapo mashabiki wa timu hiyo wanaweza kumshuhudia kwa mara ya kwanza Dzeko akicheza.

No comments:

Post a Comment