LONDON, Uingereza
KOCHA Arsene Wenger, amesisitiza kuwa hataki kununua wachezaji wenye majina, wakati akiwa kocha wa Arsenal.Alisema Gunners, haitaweza kujiweka kwenye hatari ya madeni muda mfupi, baada ya kuanza kuonesha mafanikio kwa
kupata faida ndogo.
Wenger ambaye amekuwa akilalamikiwa na mashabiki wa Arsenal kwa kukataa kutumia fedha kusaini wachezaji wenye majina makubwa katika soka, baada ya misimu mitano ya ukame wa makombe alisema: "Unaangalia katika klabu ambazo zinapoteza pauni milioni 100 au 150 na kama sisi tutafanya hivyo tutakwisha.
"Tunaweza kulipa pale tunapoweza. Ninashangazwa na watu wanaoshangaa kwa nini hatufanyi hivyo."Mkuu huyo wa Gunner, alisema hayo kwa kulinganisha na timu za Chelsea na Manchester City, ambazo zinamilikiwa na mamilionea.
Aliongeza: "Tunakabiliana na wapinzani ambao hawaheshimu ushindani wa haki wa kiuchumi. Badala ya sisi kulaumiwa, watu wanatakiwa kuwaangalia wengine."
No comments:
Post a Comment