22 December 2010

Tevez akubali yaishe Man City

MANCHESTER, England

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Carlos Tevez amefuta barua yake ya maombi ya kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo, hivyo kurejesha hali ya utulivu ndani ya City inayofukuzia ubingwa wa nchi hiyo.Manchester City ilitangaza
jana kuwa mkataba wa Tevez, ambao umebakia muda wa miaka mitatu na nusu, haujabadilika na kwamba mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina ameshaeleza azima yake ya kuitumikia klabu hiyo.

Juzi Jumatatu, Tevez alirejeshewa nafasi yake ya unahodha katika mchezo dhidi ya Everton na kupokea mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki wake wa nyumbani, lakini jambo hilo halikuweza kuzuia timu hiyo, isiambulie kichapo cha mabao 2-1 ambacho kimeiacha timu hiyo ikiendelea kushika nafasi ya tatu, huku ikiwa nyuma kwa pointi mbili dhidi ya vinara wa ligi hiyo, Manchester United.

Kipigo hicho kinadaiwa kuondoa ile hali iliyokuwepo ndani ya  Eastlands, baada ya kupata taarifa mapema za kwamba Tevez, ambaye ni mpachikaji mabao anayeongoza pia ni kwa kulipwa fedha nyingi amebadili mawazo.

Taarifa hiyo ilikuja baada ya siku tisa za tafrani kutokana na mchezaji huyo kudai kutaka kuondoka, akidai mahusiano yake na baadhi ya maofisa wa ngazi ya juu yalikuwa yamevunjika.

Mbali na madai hayo, mshauri wa Tevez, naye pia alidai kuwa mchezaji huyo hafurahishwi na kitendo cha timu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu.

No comments:

Post a Comment