22 December 2010

Weakleaks yaihusisha Tanzania na uranium DRC

Na mwandishi wetu

BAADA ya tovuti inayovujisha siri nyeti za Serikali za nchi mbalimbali duniani kuanika siri za Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), mtandao huo wa WeakLeaks umefichua siri nyingine nzito kudai kuwa  Tanzania ni kitovu cha
usafirishaji madini ya uranium kwenda nchini Iran

Kwa mujibu wa taarifa za tovuti hiyo, Marekani inazishutumu nchi mbili katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya na Tanzania kwa kwa madai ya kuwa kitovu cha usafirishaji kinyemela madini hayo hatari.

WeakLeakes ambao ulifichua siri mbalimbali za Balozi  za Marekani, unaitaja Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) kuwa ndilo chimbuko la madini hayo ambayo baada ya kusafishwa hutumika kutengeneza nguvu ya umeme na silaha hatari.

Ilidaiwa kuwa madini hayo ya uranium yanachimbwa na kampuni za kigeni katika Jimbo la Katanga kabla ya kampuni hizo kuyasafirisha kwenda Iran kupitia ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika taarifa za mtandao huo, mwanadiplomasia wa Marekani jijini Dar es Salaam, Purnell Delly  Septemba 2006 anadaiwa kuripoti kwa wakuu wake mjini Washington akisema inafahamika wazi meli zilizosheheni madini ya uranium zimekuwa zikipita katika bandari ya  Dar es Salaam zikiwa njiani kwenda Iran.

Kutokana na taarifa hiyo miaka miwili baadaye Polisi wa Kenya waliamua kuingilia kati kile walichohisi, Uganda kusafirisha madini hayo kutoka DRC na kufanikiwa kukamata vifaa hatari vya milipuko na kutiwa mbaroni wanaume wawili waliodaiwa kununu vitu hivyo kutoka DRC kwa thamani ya sh. milioni 3.9 na walipanga kuviuza mjini Nairobi kwa thamani ya sh. milioni Sh.100.

Mei mwaka huu, Polisi nchini Kenya walifanikiwa kukamata kilo 10 ya vitu  vinavyosadikika kuwa ni madini ya uranium, hali ambayo ilizua taharuki kwa Jumuiya za Kimataifa kwamba nchi hiyo ilikuwa ikitumika kama njia ya kusafirishia madini hayo kutoka  DRC.

Mtandao huo pia ulimnukuu Balozi wa Uswiss akidai kuwa Afrika Mashariki ndiyo njia kuu ya kusafisha madini ya Uranium.

“Kwa mujibu wa mwanadiplomasia mwandamizi wa Uswiss, usafirishaji wa  uranium kupitia bandari ya  Dar es Salaam unafahamika bayana kati ya kampuni mbili za meli kutoka Uswiss,” aliandika  Delly.

“Hans Peter Schoni,ambaye ni Balozi wa Uswiss nchini  Tanzania, alishazungumzia kuhusu tuhuma za madini ya  uranium kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo  (DRC) kupitishwa katika nchi za  Zambia na  Tanzania kwenda  Iran, lakini hakupewa jibu lolote kutoka kwa kampuni husika ama mahali panapodaiwa kupelekwa madini hayo,”aliongeza mwanadipolimasia huyo.

Alielezea kusikitishwa kwake pamoja na taasisi husika lakini haijawahi kuthibitishwa ama kukanushwa ripoti hizo kuhusu meli hizo za  uranium.

Katika ripoti hiyo, Delly ana wasiwasi kwamba huenda mwanadiplomasia wa Marekani mjini Kinshasa, Dpopovich Econoff, ambaye tovuti hiyo ya siri ilimtaja Novemba mwaka  2007 akisema kuwa kuna madini mengi ya  uranium nchini DRC.

“Haifahamiki wazi kama kampuni ya  Malta Forest ama kampuni nyinginezo zilizopo katika Jimbo la  Katanga zinahusika na usafirishaji wa uranium. Mazingira ya kuwepo kwa biashara hiyo yanaonekana lakini ushahidi wa uhakika ndiyo hauonekani,”aliripoti  Econoff na kuongeza;

“Vilevile kuna faida kubwa kutokana na kiwango cha uranium kinachozalishwa na kampuni ya  Malta Forest's Mines hususani tangu bei ya madini hayo ilipopanda kutoka wastani wa  dola 15 mwaka  2004 na kufikia wastani wa dola 135 kwa paundi mwaka 2007,”

Kwa mujibu wa mwanadiplomasia huyo madini hayo yanachimbwa kwa wingi na kampuni zinazomilikiwa na vigogo  ndani ya Serikali ya DRC na kusafirishwa nje ya nchi kwa njia ya panya na mitandao ya rushwa.

Alisema mfano kampuni ya Malta Forest inahusishwa na mshauri wa Rais Joseph Kabila huku kampuni za Uswiss na Finnland zikijipatia faida kubwa kutokana na madini hayo katika Jimbo la Katanga.

8 comments:

  1. Oooh! mafisadi vigogo jiandaeni, weakleaks hiyoooooo inaweka hadharani kweupe, tunasubiri mengine mengi nadhani, sasa shinikizo la damu liko sambamba na nyie. Tusubiri

    ReplyDelete
  2. Udumu Mtandao huu. Mwanzoni niliposoma habari za Marekani tu, niliona kama unaniboa sasa habari za nchi yangu ninayo ipenda sana. Du! huyu jamaa ametumsha okey Wabongo kazi kwetu tupige kelele tuwazomee haooooooo! Wezi wa Kodi zetu. Walaaniwe na wakose amani hadi watubu.

    ReplyDelete
  3. Yaliyoandikwa na Weakleaks, ni ukweli mtupu. kwamba Kikwete hana nia ya kumaliza ufisadi. Huu ni ukwli mtupu. hapa shida siyo ya kikwete ila ni sisi watinzania wenyewe. inawezekana vipi, kiongozi kama huyo, bado tunaendelea kumshabikia? hivi watanzania tunataka ushahidi gani... mpaka tuseme basi??? Tutaimba ya Kikwete na CCM hadi lini? watanzania nchi inauzwa hii!!! Amkeni!!! Raisi hawezi kuwalinda wezi na wabadhilifu wa nchi yetu huku mamilioni tunaendelea kuwa maskini!! Hii nini maana yake? hadi lini mafisadi wataendelea kulindwa?? Ole wenu nyie mnaendelea kuimba ya Kikwete na CCM. Hosea alifichua ukweli mtupu kuwa Kikwete ndiye pingamizi la vita dhidi ya mafisadi. Ni bure tu kuendelea kuongelea swala hili mitaani.. kila mtanzani aone uchungu na nchi yake... tuwakatae viongozi wa namna hii..!! wadumu watanzania wote wenye nia njema ya kuafukuza CCm na Viongozi wao wanaoiua nchi yetu na wadumu wanamapinduzi wa kweli wa Tanzania. wafie mbali wate wanaokubali fulana na kofia za rangi ya kijani na njana bila kujua kuwa wanacheka tu na nyani ambapo matokeo yake ni tanzania kuvuna mabua ya umaskini unaokithiri! Aibu KIkwete!!!! Hoingera Hosea kwa kufichua ugonjwa huu.. Hongera Weakleaks, kwa kutuamsha watanzania!!!

    Ramadhan, Kihonda Morogoro.

    ReplyDelete
  4. Kidonda kinazidi kujichimba kwa Rais Kikwete kwani pia nimesoma sehemu fulani katika mtandao wa Wikileaks unaihusisha kutupiliwa mbali kwa ombi la Spika mstaafu Sitta kuongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni sehemu ya kupinga na kujaribu kuwaziba midomo wabunge watakaokuwa tayari kuanika matatizo anuai ya nchi hususani mienendo ya rushwa miongoni mwa viongozi wa juu wa serikali.
    Subirini mengi zaidi yanakuja kutoka katika mtandao huu.

    Herry, USA.

    ReplyDelete
  5. VIONGOZI WA NCHI YA TANZANIA, KIASHIRIO CHEKUNDU KIMEIMULIKA NCHI YETU KWA TUHUMA NZITO ZA USAFIRISHAJI WA MADINI HATARI YA URANIUM, TAHADHALI ZA MAKUSUDI ZICHULIWE ILI NCHI YETU ISIINGIE MATATIZONI NA KUSABABISHA UVUNJIFU WA MAHUSIANO YA KIDIPROMASIA KUTOKA NCHI ZINAZOLAANI DUNIA NZIMA KWANI HAKUNA ANAYEFURAHISHA NA HALI HII.

    ReplyDelete
  6. RAIS KIKWETE UKO MTEGONI,TULIA TULI KUNA WATU WANATAKA UTUMIE MAJESHI NA POLISI KUFANYA MAUAJI,HAYO YA WIKILEAK NI YA KAWAIDA KWA WENZETU, HUKU NDIO KWANZA YAFIKE NA KILA NCHI ILIYOTAJWA WAHUSIKA WAMEPINGA,MWENYE USHAHIDI AKAFUNGUE KESI YEYE NA KATIBA MPYA HIYO INAKUJA BILA SHAKA ITATOA MWANYA WA WATU BINAFSI KENDESHA MASHITAKA

    ReplyDelete
  7. Kwani nani asiyejua serikali yote iliyoko madakani ni ya mafisadi?? Nilishasema tena kuwa acha watanzania wa kizazi hiki tufe kwanza labda kizazi kitakachokuja ndicho kitaweka mambo SAFI. Tulipiga debe sana wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa Octoba kuwa mafisadi wasichaguliwe lakini watanzania wasivyoelewa maaana ya mafisadi walitumbukia kwenye mtego wao. HAYA MAFISADI WANAFANYA MAMBO YAO DAKIKA ZA MWISHO.

    Kimali, BJ

    ReplyDelete
  8. Tunajadili mengi ya mambo tusiyoyajua na kuishia kubwata humu ndani ya mitandao. Tuende mbele turudi nyuma, hawa Wamarekani ni wazushi na wanafiki. Uranium sio kama unga wa muhogo au shenena ya mbao, ambapo meli nzima inaweza kupita kutoka sehemu moja kwenda nyingine pasipo kujulikana ina nini. Sio Uranium jamani! Madini haya ni nyeti kuliko mengine yoyote, sio rahisi wakubwa hawa wasijue meli "nzimaa" imesheheni Uranium inatoka bandari hii hadi ile. Hivi kuna aliyejiuliza hiyo migodi ya DRC inamilikiwa na nani kama sio Makampuni ya Marekani na Ulaya? Madini hayo hayabebwi kwenye viloba au mapipa/madebe, ila kwenye vyombo maalum vinavyozuia yasifanye madhara kwa mazingira, ambavyo ijulikanavyo, ni kampuni chache maalum, tena za wakubwa hao hao ndio zina uwezo wa kutengeneza makasha hayo. Hakuna aliyejua hao wapitisha madini haramu wali walipokuwa wanaayaagiza kwa ajili ya madini ya kujaza mameli mazima mazima? Kwa mapitio ya haraka, utaona msisitizo ulikuwa mkubwa kwenye bandari ya Mombassa - Kenya kuliko Dar es Salaam.

    Niseme hapa, kuna mengi yamefichika na Wamarekani hawataki kusema ukweli. Migodi yao ya DRC wameitelekeza na kuacha madhara makubwa ya mazingura na kufumba macho - acha wajinga hao waafrika wafie mbele. Ingekuwa kwao au kwa wenye kujua HAKI zao, madudu waliyoyaacha huko DRC yangeachwa hovyo kama walivyofanya? Sasa leo ni kama waliokosa mwelekeo na wameparaganyika. Kwa kiwango cha chini kama kilivyoanikwa hadharani na WikiLeaks - Marekani iko hoi, na sidhani kama ina uwezo wa kusimama na wenzao kama China na wengineo. Je haya yametolewa makusudi ili kugonganisha vichwa watu ndani ya nchi zetu, au ni kutokana na uzembe na kushuka kwa viwango kumepelekea kuanikwa wakubwa hadharani?

    ReplyDelete