10 December 2010

Watanzania bado si huru-Shivji

Na Edmund Mihale

MHADHIRI sheria na wanaharakati wa haki za binadamu, Prof. Issa Shivji amesema Watanzania wanasheherekea kutimiza miaka 49 ya uhuru wakati wao
si huru.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Nkrumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana, Prof. Shivji, alisema maana ya uhuru ni uwezo wa kufikiri na kujiamulia mambo mwenyewe, jambo ambalo halipo nchini kwa sasa.

Alisema kuwa suala la kuwa huru liliisha baada ya kufa kwa Azimio la Arusha ambalo lilitetea wanyonge, hali ambayo ilileta heshima ndani na nje ya nchi.

Alisema kwa sasa Tanzania si huru kwa kuwa haiwezi kujiamulia mambo yake yenyewe hadi hapo itakapopewa amri na wakubwa kutoka nje, jambo lililopingwa na Mwalimu Julius Nyerere wakati wa uhai wake hadi kifo chake.

"Misingi ya Azimio la Arusha ilianza kwa Watanzania wenyewe kufikiri na kuamua nini wafuate baada ya Uhuru,  fikra hizo hazikutoka kwa shinikizo kutoka Washington au Uingereza kama ilivyo sasa," alisema Prof. Shivji.

Alisema kuwa hata walipokuwa wakienda nchi za nje waliheshimika kutokana na uamuzi wa kuwa na azimio hilo.

"Tulipewa heshima kubwa na maprofesa wa nje ambao walituuliza kila mara iwapo tunatoka nchi ya Nyerere nasi tuliwapojibu ndiyo, walitupenda na kutupa heshima kubwa kutoka na Azimio la Arusha.

"Hata sasa muulize mtu wa zamani atakwambia Misingi ya Arusha lilirudisha heshima yao na utu wao baada ya uhuru," alisema Prof. Shivji.

Alisema kwa sasa mambo mengi yamekuwa yakiamuliwa kutoa nje hususani bajeti ya nchi imekuwa ikipelekwa nje na kutolewa uamuzi, wakati Mtanzania wa kawaida hajui kinachofanywa na serikali yake.

Alisema serikalia ya sasa imekumbatia sera za mfumo wa kibepari ambazo zimetoka katika nchi za kibepari na hazitaifikisha nchi popote kwa kuwa zimezeeka, hivyo kinachotakiwa mfumo mbadala ili kuifikisha nchi mahali pazuri.

Alisema mfumo huo umejenga tabaka la kundi la wasionacho na kundi dogo la walionacho, jambo ambalo ni hatari kwa mstakabali wa taifa. 

Alisema mfumo huo pia umesababisha serikali kuingia hasara ya kuilipa kampuni ya kuzalisha umeme ya Dowans na maumivu yake yatakwenda kwa wananchi wa kawaida.

Akizungumzia katiba, Prof Shivji alisema kuwa yeye binafsi haoni sababu ya Watanzania kujadili suala la katiba bali wanachotakiwa ni kujadili Tanzania mpya itakayowajali wanyonge.

"Kuna malumbano makubwa tunayasikia kutoka kwa wanasiasa kuhusu katiba, lakini mimi hapa sioni kama kuna jipya suala ni kuitisha majadala wa kitaifa kujadili Tanzania mpya na katiba ije baadaye ,lakini wanasisisa wanataka mambo ya haraka.

"Nakumbuka hata wakati wa kuanzisha vyama vingi tulikaa na wanasiasa, tukasema tuanze mchakato kwanza walau kwa miaka miwili ndio tuingie katika mfumo huo, lakini walikataa wakasema wataka kushika dola, kuingia Ikulu.

"Tanzania hatuna wanasiasa bali kuna wapenda madaraka kwa kuwa wanapenda madaraka, basi wanakimbilia huko nawashauri wananchi kungalia hilo," alisema Prof. Shivji.

Alisema wakati wa Mwaliamu Nyerere walikuwa wakiitisha warsha chuoni hapo naye alihudhuria na kuulizwa maswali na wahadhiri wa chuo hicho.

"Siku moja aliulizwa swali moja la nani anafaa kuwa kiongozi bora, Mwalimu Nyerere alijibu kuwa 'kiongozi bora ni yule ambaye hataki kuwa kiongozi, lakini analazimika kuongoza kwa kuwa hataki wapumbavu watawale'," alisema.

14 comments:

  1. Huyu Prof. anampigia debe marehemu! Na basi ampigie kura kama yule bibi wakati wa uchaguzi aliogoma kupiga kura hadi aone jina la nyerere! Huu si wakati tena wa kuturudisha nyuma! Si kila jambo lililosemwa au kuamuliwa na nyerere lilikuwa bora, mabaya yapo mengi tu, hata hilo azimio la arusha halikuwa na manufaa makubwa kwa wengi, kama nyerere aliliona bora basi si watanzania wote liliwafurahisha! Hivyo nakushauri Prof. Shivji uanze kampeni ya kumtakatifisha nyerere kwa papa, maana keshakufa na azimio la arusha halitorejeshwa! enzi za unyerere zimepita, hakuna tena unafiki!

    ReplyDelete
  2. Hivi wewe Said. mbona unapinga kila siku vitu vya ukweli au nawe fisadi?

    ReplyDelete
  3. Tukubali, tukatae, Jina la Mwalimu Julius Kambarage Nyerere litakuwa mioyoni au tumboni mwa watanzania kwa muda mrefu. Kuna watu wanamnung'unikia hata Mungu kwa baadhi ya mambo. Kwa hiyo pamoja na mabaya ambayo yatakuwa yalifanywa na Nyerere lakini kwa upande wangu alikuwa kiboko cha Mafisadi. Sio kwa nyakati hizi ambapo Mafisadi yanatamba mchana kweupeee! kwa rasilimali zetu wote wakati wengine tunaugulia katika lindi la umaskini. Hapa ndipo penye tatizo kubwa.

    ReplyDelete
  4. Issa Shivji, Professor, hata wewe unayo mabaya mengi na mazuri mengi, uongo?. We learn through mistakes. Hii mambo ya kukosoana ki-siasa isiwe kama vile kuna fumbuzi zilizo jificha ambazo wewe unajua zilipo.
    Pole pole, kuna chama kitakuja okoa hii nchi, iwe isiwe, lakini si kwa pupa kama unavyo fikiri. Vile vile kama unaona hapa TZ hapakufai, usiwapotoshe watu, hii issue ipo hata huko kwa mababu zako India, Pakistan au sijui Bangdesh.Waweza kuamua kwenda zako mzee, isiwe taabu sana. Sisi siyo wajinga, tunajua tunacho kifanya. Hata hao wa TAA, TANU, CCM wanayo masikio, wanayo macho, na wanazo akili, watajua na wanajua watafanya nini. hata ikibidi kukabidhi madaraka ya nchi kwa chama kinacho wafaa wananchi. Hivyo basi, wapewe muda wa kuondoka madarakani kwa amani na wajao waje madarakani kwa amani, msitupotoshe tuanze kulumbana kila kukicha na kisha tuanze kuumizana sisi. Hatukuozea ubabe huo. Anne Tikche, nisamehe lakini umenikera ndiyo maana nimekujibu japo ulifundisha chuoni miaka ya 80's, lakini kwa hili sikubaliani nawe kamwe.

    ReplyDelete
  5. WE KIPROFESA ACHA HIZO KATIBA MPYA NI LAZIMA HAKUNA KULALA HADI KIEELEWEKE

    ReplyDelete
  6. watanzania njaa zinawasumbua mpaka zimewatoa akili,huyo professor naona hata hamumuelewi anachozungumza kwa sababu mumekoseshwa elimu tokea kindergatten na hiyo ndio inayomuinua mtu na msingi mzuri kiendana sambamba na lishe bora na malezi bora, lakini watanzania yote mumeyakosa masikini watanzania, hamuna uwezo wa kufikiri hata upeo wa masaa wachilia mbali huko anakozungumzia Shivji, mimi naona huyu profesor hana kazi, kwa sababu hiyo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaaa, poleni watanzania mutaendelea kukaa barabarani kumsubiri rais mumpigie makofi maisha yenu, poleni sana.

    ReplyDelete
  7. Naomba yeyote anayejua historia ya Shivji wakati wa utawala wa Nyerere anisaidie kunielewasha. Swali ninalotaka kujibiwa ni je, Shivji alikuwa anamuunga mkono Mwalimu na mfundisho kama anavyofanya sasa hivi? Sasa hivi kuna watu wanajijengea umaarufu kwa kuongelea enzi za Nyerere. Ila tukubaliane kuwa, pamoja na kwamba Nyerere ni shujaa wetu na baba wa taifa letu, kuna makosa yaliyofanywa huko nyuma ambayo matokeo yake bado yanaonekana leo. Shivji asitufanye watoto wa jana. Tujaribu kutatua matatizo tuliyonayo leo, lakini siyo kuturudisha enzi za Nyerere. Nyerere hautuachia nchi tajiri. Ni baadhi ya siasa zake mbaya zimetufikisha hapa tulipo!!!!!

    ReplyDelete
  8. Mimi ni yule yule Mzanzibari Halisi,mwana mageuzi Hafidh kutoka Zanzibar.

    Napenda kuchangia hoja hii katika mtazamo wa Prof Shivji na wanataaluma wengi amabao wanajikita katika kuishinikiza kwa njia moja ama nyengine Taifa la Tanzania lirudi katika Siasa za Kikoministi !

    Kwa mtazamo wangu kwa dunia ya leo hakuna taifa lililosimika hasa falsafa hii mwelekeo wa kikoministi mana hata hao waasisi wa mrengo huu basi wamebadilika kifikra ila kimuundo wanajiita wakomenisti. hebu tuaangalie kidogo mana naona ntawaacha watu katika giza, nina mana hii ya kua ukiwaona China wanasema wakomenisti kimrengo wa kisiasa lkn kimatendo sio ukoministi ule tayari wametoka halikadhallika Urusi na nchi zote zilizokua na msimamo huu so mabadiliko yanakuja kutokana hali halisi ya dunia inavyokwenda.

    Tuiangalie Tanzania ilipokua chini ya Uongozi wa Mwalimu hali ya biashara ilikuaje?! ilikua hakuna uhuru wa biashara na bidhaa zilikua adimu sana kwa huku kwetu Visiwani tulikua tunanunua mchele,sukari , unga kwa misururu ya foleni tena kwa wiki mara moja au mbili chini ya usimamizi wa Balozi ! lakini tulipoamua kuondokana na fikra hizi hatua kwa hatua naona mabadiliko yamekuja , Mzee Ruksa alifungua milango ya biashara anaeweza alete, haya ni mafanikio maana kutakua na ushindani wa kibiashara na hiyo ni fursa kwa wanunuzi amabao ni wananchi walalahoi.
    Huo ni mfano mmoja tu ipo mingi.na mzee wangu Prof SHIVJI ajue kwamba hakuna kitu chenye faida lakini kisiwe na side effects.

    Cha msingi ni kuondoa mianya mibovu ya watu wachache wabinafsi na kuiziba ili taifa zima liwe na manufaa.inawezekana kwa hili.

    Zipo nchi tele duniani hazifati mrengo wa ukoministi na sasa ni nchi zinazojiweza kimaisha bila ya msaada wowote. Tanzania inawezekana kabisa ikiwa tu tutakua tayari kupata mageuzi ya ukweli.

    Nataka niwambie tuu Zanzibar tunaanzisha safari hii na mda si mrefu kwa uwezo wa Mungu mambo yatakaa sawa ili na ndugu zetu watanganyika muelekee safari hii ya pamoja.

    ReplyDelete
  9. Jambo la msingi alilosema Prof. ni "Tanzania hatuna wanasiasa bali kuna wapenda madaraka kwa kuwa wanapenda madaraka",

    ReplyDelete
  10. Ah minaona huyu mzee kaishiwa kweli,sisi watanzania hatutaki tanzania mpya,tunataka Tanyanyika na katiba yake,rais wake,na baraza la kutunga sheria,Pia na bajeti yetu,tunataka tujue mabo ya muungano na sio ya muungano ambayo tuwe na usawa,tanganyaka tufaidike na zanzibar pia wao wafaidike,Pia tujea jinsi gani serikali ya muungano inavyo wafaidisha watanzania baina ya zanzibar na tanganyika,kama hakuna faida tuuvunjilie mbali.

    ReplyDelete
  11. Ningependa kumsikia Prof.Shivji atuambie kama kila kitu cha Nyerere kililijenga Taifa hili la Tanzania.Nataja makosa makubwa machache ya Nyerere na akina Shivji wake wa siku zile: 1.Kuhamishia watu kwenda " vijiji vya ujamaa".Mpaka sasa Jamii ya Watanganyika hawajatulia kutokana na hili kosa.
    2. Uamuzi wa kwenda Dodoma. Leo hii unalighalimu Taifa kwa kiasi cha kulimaliza nguvu kiuchumi. Tuna makao Makuu sehemu tatu, Magogoni Dar-es-Salaam. Dodoma. Na Zanzibar.
    Kutaifisha misingi mikubwa ya Uchumi. Na halafu baada ya kushindwa,kuibinafsisha kwa bei ya shilingi moja!!!
    3.Kukijenga Chama chake CCM kuwa na kiburi cha kidikteta kama alivyokuwa yeye mwenyewe. Tusimshangilie Nyerere bila kufikiri!!

    ReplyDelete
  12. Jamani nakuombeleni mumuelewe vizuri prof hicho alicho ongea hapo ni sawa ingawa kama bibinadamu kuna mapungufu lakini ni ya kibinadamu lazima muweze kumuelewa alicho kikusudia sidhani kama ameongea baya ndani yake lakini inawezekana mumemuelewa vibaya ama hamukumuelewa kabisa.hakukataa katiba mpya ila amesema kwanza tujenge tanzania mpya ndio badae ije katiba.na ushauri alio utoa kw mfumo wa vyma a ingi lakini wanasiasa wakawa na haraka na ndio hayo sasa yanawakuta wengine wasusua matokeo na kupelekana mahakamani ma matokeo mengi tu mabaya kwa chaguzi zetu hizi za vyama vingi .mi nadhani ushauri wake sio mbaya hata kidogo

    ReplyDelete
  13. Prof Shivji hajakosea hata kidogo. Mwanzoni tu amesema hatuko huru kwasababu hatujuwi nini tunachokitaka. Ndio unakuta mtu anasema wewe kiji prof, wewe muhindi, sijuwi wewe mpakistani, wewe unayesema hivi, tambua huo ni ubaguzi, huo ni ujinga.

    Usimjadili mtu, jadili kile alichosema au kuandika. Ndio maana waliokuwa na maarifa na walio soma, hukubaliana kuto kukubaliana au huamua kukubaliana kwa baadhi na mengine wakatafautiana na hapa ndivyo inavyotakiwa.

    Mimi si mfuasi wa Mwalimu Nyerere na wala si mfuasi wa ujamaa, lakini kwa baadhi ya mambo Mwalimu Nyerere tunaweza kusema ni kiongozi shupavu. Anapozungumza unajuwa kwamba unamsikiliza kiumbe mwenye akili timamu. Si uongo Mwalimu anaposimama UN na kuzungumza, basi si sawa na anavyozungumza Kikwete na kusikilizwa au Mkapa, au sijuwi hawa maraisi uchwara wa Afrika. Anaposimama Mwalimu kuzungumza kitu basi huonekana kwa wakati wake ni sawa na Nelson Mandela.

    Tanzania ni kweli usiopingika kuwa imepoteza mwelekeo wa kuwa huru. Kuna kila sababu haya mambo kuzungumzwa kwa upana kabisa. Wasomi, watu wa dini na watu mashushuru wanapaswa kukaa chini na kuaangalia tuenako na kuangalia tutokako. Jee huu ndio uhuru tulio pigania? Nadhani baada ya kutoka hapo, tunaweza kuwa na katiba safi tunayoitaka sisi wenyewe wa Tanzania.

    ReplyDelete
  14. Mimi ni yule yule mwanaharakati mwanamageuzi kutoka visiwa vya amani Zanzibar - Ni yule yule Hafidh.

    Napenda kufatilia hoja za msingi na vipi watu wanaweza kujenga mhimili ya hoja zao.

    Niliwahi kutoa mchango katika mada hii na ntaendelea kutoa mchango wa mada hii pale ntakapoaana panahitajika kutoa.

    Mara hii naona wachangiaji wengi wanakubaliana na Prof Shivji Kua bado Taifa letu la Tanzania bado sio huru !! mimi binafsi namkubali Prof Shivji lakini si kwa kila kauli anayotoa ntakubaliana nayo,haiwezekani - kuna mchangiaji mmoja anasema kua ati wachangiaji na wanaomkosoa Shvji hawajamuelewa na kumfahamu ! Ndugu yangu napenda nimuambie Prof alizungumza suala hili kwa kiswahili fasaha kwa hiyo waliowengi wamemuelewa vizuri anachokisema na alichokusudia labdakama wapo ni wachache tu .

    Hebu napenda niwaulize wale wote wanaomkubali Prof Shivji kwa hili kua bado watanzania sio huru !!

    Hebu jengeni hoja za msingi - ili watanzania wawe huru wanatakiwa wawe vipi? kati ya sasa na hiyo ya vision ya Shivji?

    Unaposema tunataka Tanzania mpya ! mna maana gani hapo? mnataka kufata mfumo wa Zanzibar Mpya ya sasa? au mna mfumo mwengine ambao ukifikiwa ndio tutajua kua sasa tuna Tanzania mpya?

    Katiba mpya mnasema sio suluhisho kwanza tuwe na tanzania mpya ndio ije katiba mpya !! hebu fafanua kwa undani kifanyike nini na nini ?

    Mwisho napenda kutoa ombi kua wanaopenda kuchangia ni bora wakaweka majina yao mana ukitaka kujenga hoja kwa mchangiaji fulani au kumjibu mchangiaji fulani itakua vizuri kumjibu kwa jina lake.

    Asante.

    ReplyDelete