20 December 2010

Wataka mameya wachaguliwe na wananchi

Na Yusuph Mussa, Lushoto

BAADHI ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto wameshauri ili kukabiliana na vitendo vya rushwa kwenye nafasi za mameya na wenyeviti wa halmashauri, kura zipigwe na wananchi wote badala ya madiwani wachache.Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi juzi kwa nyakati tofauti, walisema kama mfumo huu wa viongozi hao kuchaguliwa na madiwani wachache hautabadilishwa, rushwa haiwezi kwisha.

Diwani wa Viti Maalumu, Bi. Husna Sekiboko alisema moja ya vitu vilivyochangia demokrasia kukua ni wabunge kupigiwa kura na wananchi wote, na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikabariki wagombea wao wachaguliwe na wanachama wote."Huwezi kumpata meya, mwenyekiti au makamu wake mzuri kama ataendelea kuchaguliwa na madiwani wachache, kikubwa ni lazima serikali ibadilishe mfumo wa kuwapata kwa kupigiwa kura na wananchi," alisema Bi. Sekiboko.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Madiwani ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Bi. Monica Hizza alizungumzia usawa kijinsia akipendekeza mifumo ya uongozi ibadilike, kama nafasi ya meya ama mwenyekiti inagombewa na mwanaume, makamu wake awe mwanamke."Ni mambo ya kujifunza kutoka juu, si unaona mabadiliko yaliyotokea bungeni, kama Spika ni mwanamke, basi Naibu Spika awe mwanaume, hivyo ndivyo inatakiwa kuwa hata kwenye halmashauri, na hata ile azma ya 50 kwa 50 kwenye uongozi itatimia," alisema Bi. Hizza.

Awali, kwenye semina ya madiwani, mkufunzi ambaye pia ni Afisa Tawala Wilaya ya Lushoto, Bi. Mwanaamani Mtoo aliwataka madiwani kuzingatia sheria na kanuni za halmashauri ikiwemo kutoshawishi ama kushiriki katika kitendo chochote kitakachochangia uongozi mbaya ndani ya halmashauri.

Bi. Mtoo pia aliwataka madiwani kujiepusha na mikataba yenye maslahi, iwe wao wenyewe ama ndugu zao na  hawatakiwi kuwa na uhusiano wa kipapenzi na watumishi wa halmashauri, kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka utaratibu.

1 comment:

  1. Ndi maana tunataka katiba mpya haraka iwezekananvyo ili kuondoa huu upumbavu wa rushwa. tukiwa na katiba mpya mambo yafuatayo yatabadililishwa FOR GOOOOD
    1. Tume ya uchaguzi itakuwa huru haitawajibika kwa Raisi kama ilivyo sasa.
    2. Mbunge hatashika nyadhifa mbili yaaani Mbunge as the same time Waziri. Hii itakoma Mawaziri watakuwa wanateuliwa na Raisi hii itakuwa effective katika uwajibikaji kwa maana kwamba Waziri anawajibika kwa Raisi na pia kwa Bunge. Ilivyo sasa hakuna effectiveness kwa mawaziri only wanawajibika kwa Raisi sio kwa wananchi tu hii imepitwa na wakati.
    3 Wakuu wa Mikoa ( RC ) na D.C watachaguliwa na wananchi ili wawajibike kwa wananchi Maana kwa mfumo wa sasa ONLY wanawajibika kwa Raisi tu huu mfumo umepitwa na wakati.
    4. Mameya kama ilivyoandikkwa hii habari hapo juu nao wachagukiwe na wananchi ili uwajibikaji kwa wananchi
    5. Free of Speech ikaziwe mkazo sana maana serikali inatishia watu pale wanaposema ukweli, kuna mifano mingi waliofanya hivyo HATUNAO TENA wako MAKABURINI sitaki kuwataja tunawajua. So free speech iwepo ili wanahabari na watu wengine wafumue uozo wa serikali bila kuogoma wakolimbwa.
    6. Kuwe na Separation of Executive Branch hii ina maana kwamba serikali na mahakama zile zinawajibika kivyake sio mfumo wa sasa MAHAKAMA kwa sababu wanachagukiwa na Raisi kesi yoyote inayokuja against GOVERNMENT hata kama inaonekana watashindwa mahakama wana rule against it b'se wanaogopa kupoteza UNGA. nilikuwa napendekeza mfumo wa America uigwe which means Supreme court wanakuwa nomineted na Raisi, lakini mpaka wapitishwe na BUNGE ndio wanafanya kazi mpaka wanakufa or Retire which means kwa mfumo huo hawajibiki kabisa kwa Raisi pale wanapokuwa Supreme Court sio kama mfumo wetu huu mbovu.
    7. Mfumo wa kupitisha miswada bungeni nao lazima ubadilike ili kulinda MINORITY kama ambavyo AMERICA In congress wanavyofanya. Mfumo wa hapa miswada inapita kwa majority vote hii sio mfumo mzuri, inatakiwa MSWADA wowote bungeni uwe unapitishwa na 2/3 ya wabunge votes hii itafanya bunge liwe linachangamoto katika kupitisha miswada na kuwawajibisha MAWAZIRI ambao hawafanyi kazi zao kikamilifu. kuliko mfumo wa sasa hauna changamoto yoyote maana its only Majority vyote mswada unapitishwa na kama nyie ni minority hamna SAUTI hata kama mtasusia na kutoka nje msipige kula this maust be stopped.
    Ni haya machahe tu niliyokuwa nayo natumaini tuanze kuyafanyia kazi kabla hali ya hewa haijachafuka mfano KENYA au Ivory Cost tunajua kilichotokea.
    Mdau USA.

    ReplyDelete