16 December 2010

Wajawazito watakiwa kupima afya mapema

Na Lilian Justice,morogoro

WITO umetolewa kwa akina mama wajawazito kupima afya mapema kubaini endapo wamepata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili wasaidiwe na wataalamu wa huduma ya afya kwa kupatiwa dawa ya kuzuia maambukizi  kwa mtoto.Wito huo ulitolewa hivi
karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa HDT Dkt. Peter Bujari wakati wa kampeni ya kutokomeza maambukizi ya virusi vya IKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto .

Aidha Dkt. Bujari alisema kuwa kampeni ya kutokomeza maaambukizi ya VVU ina lengo la kunga mkono jitiada za kitaifa za kuhakikisha hakuna mtoto anambukizwa VVU kutoka kwa mama.

"Kampeni hii itahusisha vyama vya kiraia ,kiuchumi,kimila na desturi pamoja na kisiasa hatimaye CEPA itajenga mtandao wa ushawishi ambao utasaidia ufuatiliaji na wajibikaji wakati wa miadi ya kuzuia maambukizi na matibabu vinaongezewa uwezo katika nchi zote za barani Afrika" alisema Dkt. Bujari.

Pia alisema kuwa matokeo muhimu yanayotegemewa na CEPA ni watoto wanaozaliwa na akina mama wenye VVU wanapima na kupatiwa majibu ndani ya wiki 10 sambamba na upatikanji wa dawa za kuzuia au kutibu VVU zinapatikana pamoja na lishe.

kutenga fedha yabkutosha kwa ajili ya matumizi ya PMTCT kufikia asilimia 80 ya wanaohitaji huduma hizi kama ilivyo ainishwa katika mkakati wa Wiazara ya Afya ya mwaka 2008-2013.

Hata hivyo alisema kuwa bado CEPA inakabiliwa na changamoto mablimbali katika kutoa huduma zake kwa akina mama na watoto ikiwemo upungufu wa wafanyakazi wa afya kwa ajili ya kutoa huduma za PMTCT na zile za matibabu kwa watoto waliozaliwa kwa maam mwenye VVU.

Pia kutoelewa ukubwa wa tatizo la watoto wanaohitajib dawa kuzuia wasiambukizwe na wanaohitaji dawa kwa ajili ya matibabu.

hata hivyo aliitaja chanagomto nyingine kua ni kukosekana kwa huduma mseto ambapo huduma zipo sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushiriki wa wanaume kwenye afya ya uzazi .

No comments:

Post a Comment