16 December 2010

Morogoro waomba Manispaa izuie biashara ya vyakula

Ramadhan Libenanga, Morogoro

WANANCHI wa Manispaa ya Morogoro wameiomba uongozi wa halmashauri hiyo kupiga marufuku uuzaji wa vyakula barabarabani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika baadhi ya maeneo mjini  hapa.Wakizungumza na mwandishi wa
habari  hizi jana, wananchi hao walidai pamoja na kusikia mlipuko wa ugonjwa huo katika baadhi ya mitaa ya Manispaa hiyo wanashangaa kuona bidha za chakula kama mama ntilie zikiendelea kufanyika katika mazingira yanayotishia afya za walaji.

Bw. Piter  Kimati, mkazi wa vibandani alisema kwa sasa mkoa wa Morogoro umekuwa na mabanda mengi ya watu wanaokaanga kuku na kuuza  zikiwa nje nje bila kufunikwa hali ambayo ni hatarishi kwa kuweza kusambaza ugonjwa wa kipindupindu.

Alisema katika mtaa wa Kiwanja cha ndege, sabasaba, chamwino na mawezi kumekuwa na vibanda vingi vya aina hiyo huku Manispaa wakiendelea kulalamikia hali ya ugonjwa huo.

Tayari watu zaidi ya watu 10 wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kutokana na ugonjwa huo wa kipindupindu hali ambayo  mabwana afya wa manispaa wanatakiwa kuwa makini katika kutoa elimu kwa wananchi ya jinsi ya kujikinga na ugonwja huo.

No comments:

Post a Comment