20 December 2010

UN yajibu vitisho vya Rais Gbagbo

NEW YORK,Marekani

UMOJA wa Mataifa (UN) umejibu vikali hatua ya kuwafukuza wanajeshi wa umoja huo nchini Ivory Coast huku mzozo kuhusu uchaguzi wa urais wa mwezi uliopita ukizidi kutokota.Rais Laurent Gbagbo ambaye amekataa kuondoka madarakani baada ya
kushindwa katika uchaguzi huo anasema majeshi ya ufaransa na yale ya UN ni sharti yaondoke nchini humo kwa kuwa yanashirikiana na wapinzani wake.

Lakini hata hivyo Katibu Mkuu wa UN,Bw. Ban Ki Moon, alisisitiza jana kuwa majeshi ya umoja huo hayataondoka nchini humo hadi pale yatakapokamilisha muhula wake wa wa mwisho  mwishoni mwa mwezi huu.

Akijibu aguzo hilo la Rais Gbagbo,Bw. Ban ki Moon alionya kuwa itachukuliwa hatua kali iwapo wanajeshi wa kulinda amani wa umoja  huo  watashambuliwa na wanajeshi wanaomtii kiongozi huyo.

Kabla ya kauli hiyo ya Bw.Ki-Moon, awali UN ilitangaza kuwa wanajeshi wake wana idhini ya kujibu mashambulizi iwapo itawabidi.

Jumuiya za kimataifa zinamtambua mpinzani wa Rais Gbagbo, Bw.Alassane Outtara kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment