20 December 2010

Stewart: Nimepata somo Yanga

Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa Azam FC, John Stewart, amesema mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga, umempa mwanga wa kujua aanze vipi kupanga mikakati yake kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.Timu hizo zilikutana juzi kwenye Uwanja wa
Uhuru, Dar es Salaam,  ambapo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, katika mchezo wa kujipima nguvu kujiandaa na ligi hiyo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Stewart alisema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake, kwani mchezo huo atautumia kupata kikosi cha kwanza.

"Mchezo ulikuwa mzuri licha ya wapinzani wetu kuchezesha timu dhaifu kipindi cha kwanza, lakini nilipata wakati mgumu baada ya kuona akibadilisha timu nzima na ndipo sasa, mechi rasmi ilipoanza," alisema.

Alisema wachezaji walioingia kipindi cha pili ndio walikuwa kipimo tosha kwake, kwani ushindani ulikuwa mzuri na hata wachezaji wake walicheza kwa nguvu tofauti na kipindi cha kwanza.

Alisema baada ya mchezo huo,  wataendelea na programu yao kesho ikiwa ni maandalizi ya mwisho, kabla ya ligi hiyo kuendelea Januari 15, mwakani.

Akizungumzia michezo mingine ya kirafiki, Stewart alisema ni vizuri kucheza zaidi na hilo atawasiliana na viongozi wake kujua kama kuna uwezekano wa kupata mechi hizo.

No comments:

Post a Comment