Na Zahoro Mlanzi
CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimetoa pongezi kwa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania Bara kwa kutwaa ubingwa wa Chalenji kwa mwaka huu.Si kwa timu hiyo, chama hicho pia kimetoa pongezi kwa
viongozi wateule wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu na Bonicafe Wambura ambaye ni Ofisa Habari.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu wa chama hicho, Amir Mhando, ilieleza kwamba, wanaungana na Watanzania wengine katika kufurahia ubingwa huo ambao kwa miaka 16, Kilimanjaro Stars haijaupata na miaka 15 kwa Zanzibar 'Zanzibar Heroes'.
Alisema wanawaomba wachezaji watumie ubingwa huo kama changamoto ya kufanya vizuri katika kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa Ndani (CHAN) za mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment