Na Amina Athumani
SHIRIKISHO la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA), limewapongeza wachezaji wa timu ya Kilimanjaro Stars kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji katika michuano ya CECAFA iliyomalizika
Dar es Salaam wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa SHIMMUTA, Awadh Safari, alisema pongezi hizo wanazitoa kwa wachezaji na viongozi wao kwa ushirikiano waliouonesha na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuukosa kwa miaka 16 mfululizo.
"Ushindi wa Kilimanjaro Stars haukuja kirahisi, umetokana na nidhamu, ushirikiano na upendo," Safari.Alisema kuifunga timu kama Ivory Coast ambayo ni moja ya timu vigogo barani Afrika, si jambo rahisi na kwamba, ni ushirikiano mzuri wa wachezaji, viongozi na mashabiki waliokuwa wakifurika uwanjani kuishangilia.
Alisema wao kama SHIMMUTA, wanaomba wadau wa michezo kuipa ushirikiano timu Kilimanjaro Stars na Taifa Stars, ili ziweze kufanya vizuri zaidi katika maandalizi mbalimbali watakayoshiriki.
No comments:
Post a Comment