Na Mwandishi Wetu
MNYANGE wa Tanzania 2010, Genevieve Mpangala, atawaongoza warembo walioshiriki mashindano ya Miss Tanzania 2010 katika ziara ya shughuli za jamii katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.Akizungumza jijini jana, Mkurugenzi wa
Lino International Agency Limited, Hashim, alisema wanyange hao wataanza ziara hiyo ya kijamii leo mpaka Desemba 20, mwaka huu.
Alisema katika ziara hiyo, watatembelea baadhi ya vituo vya kulelea watoto yatima na wanafunzi wa shule za msingi wanaosoma na kuishi katika mazingira magumu. Warembo watakaokuwa kwenye ziara hiyo ni Glory Mwanga, Anna Daudi, Buduri Ibrahim, Christina Justine, Prinsca Mkonyi, Furaha David na Salma Mwakalukwa.
Lundenga alisema ziara hiyo, imedhaminiwa na Ndege Insurance na Vodacom Tanzania Limited.
No comments:
Post a Comment