16 December 2010

SAKATA LA VIWANJA DAR

Tibaijuka akwaa kisiki

*Maagizo aliyotoa juzi kurudisha maeneo yapingwa
*Wahusika watumia barua Ofisi ya Rais kujitetea
*Wasema Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye alibariki
*Watishia kumburuta mahakamani endapo atavunja uzio
*Yeye asema hakukurupuka, atasimamia maamuzi yake


Na Grace Michael
SIKU moja baada ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka kuamuru kuvunjwa ukuta wa kiwanja
namba 1006 kilichopo Palm Beach jijini Dar es Salaam kuna kila dalili za kuibuka sakata la mgogoro katika kiwanja hicho ukihusisha Ofisi ya Rais Ikulu na watendaji katika wizara yake akiwemo Mkurugenzi wa Mipango Miji.

Ofisi ya Rais imetajwa kuhusika katika sakata hilo kwa kutoa maelekezo kwa Wizara kutekeleza amri ya mahakama ambayo inampa uhalali Bw. Taher Muccadam kuwa ni mmiliki halali wa kiwanja hicho na pia apewe hati miliki mpya  kumiliki eneo hilo na aruhusiwe kuzungusha uzio na kupewa kibali cha ujenzi.

Maelezo ya malalamiko ya Bw. Muccadam kwa Ofisi ya Rais yanathibitishwa kupitia barua yenye kumbukumbu namba CEA 157/638/IV/01 ya Juni 2, mwaka jana iliyosainiwa kwa niaba ya Katibu wa Rais na G.M. Masaju ikiwa na kichwa cha habari kisemacho 'Ucheleweshaji wa kutekeleza uhuru wa sheria katika kiwanja namba 1006 Upanga'.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Bw. Muccadam alisema kuwa atamfikisha mahakamani Prof. Tibaijuka endapo atavunja uzio wa kiwanja chake bila kutengua amri halali ya Mahakama Kuu iliyopo na atafanya hivyo kwa kuwa ana uthibitisho wa vibali vyote vya ujenzi na amevipata kihalali.

"Tibaijuka asipokuwa makini ataingia kwenye scandal (kashfa) mapema, asikurupuke katika maamuzi kwa kuwa ataifanya Serikali kuingia kwenye gharama kubwa za ulipaji fidia," alisema Bw. Muccadam.

Alisema kuwa mbali na Ofisi ya Rais kutaka amri ya Mahakama itekelezwe, Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye alishauri kutekelezwa kwa amri ya mahakama baada ya Wizara kuomba ushauri kwake.

"Kwanza eneo hilo si la wazi kama wanavyosema bali ilipendekezwa tu lakini baadaye Manispaa ilitoa hati kwa wamiliki wa kwanza kwani eneo hilo lilipaswa kuchukuliwa na AMREF...je kama hao wangejenga wangewabomolea?" Alihoji.Alisema Kamishna wa Ardhi ndiye mwenye mamlaka makubwa ya ardhi kwa kuwa ana uwezo wa kumshauri Rais kubatilisha lakini baada ya kuona uhalali wa kiwanja hicho, alisaini hati ya kiwanja 1006 kilichopo Upanga.

Akizungumzia suala la hati hiyo kubatilishwa na Rais Mkapa kama Prof. Tibaijuka alivyoelezwa na wataalam wake, alisema kuwa si kweli kwamba Rais yupo juu ya sheria kwa kuwa nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya sheria na Katiba ya nchi, ndio maana hata wakati akila kiapo aliapa kuilinda katiba na sheria za nchi.

"Kwa misingi hii ndio maana Mahakama ilitoa uamuzi huo kwa kuwa ubatilishwaji haukufuata taratibu husika," alisema.Mbali na hayo, pia Bw. Muccadam alimtaka Prof. Tibaijuka kufuatilia uhalali wa upatikanaji wa kiwanja namba 305 ambacho ni kiwanja jirani na kiwanja hicho ambacho kimeamuriwa kuwa eneo la wazi kwa kuwa taratibu za tenda hazikufuatwa.

Barua nyingine ambayo nakala yake Majira linayo, imeelekezwa kwa Mrungenzi wa Manispaa ya Ilala ambayo ilisainiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo yenye kumbukumbu namba CA87/01/52 ya Septemba 28 mwaka jana ambayo inatoa maelekezo ya kugawanywa kwa kiwanja hicho ili kupatikana sehemu ya kuegesha magari na ikaruhusiwa ujenzi wa jengo la ghorofa kumi kwa matumizi ya makazi.

"Mchoro namba 1/504/369 inaonesha mgawanyo wa kiwanja tajwa umeidhinishwa na Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Septemba 25, 2009, kiwanja hicho kilichogawanywa kwa kufuata amri ya mahakama, imepatikana sehemu ya kuegesha magari na ujenzi wa jengo la ghorofa kumi," ilisema sehemu ya barua hiyo.

Majira lilipowasilina kwa njia ya simu na Prof. Tibaijuka kutaka ufafanuzi kuhusu kauli ya Bw. Muccadam, alisema kamwe hawezi  kubadili msimamo wake katika kushughulikia sakata hilo, ndio maana wakati anatoa amri hiyo alikuwa na wataalam wote wa Wizara akiwemo Mkurugenzi wa Mipango Miji.Alisema kuwa endapo mlalamikaji anaona ana haki, watakutana mahakamani kwa kuwa mahakama zipo kwa ajili ya kutoa haki kwa pande zote mbili na haijalishi kama ni Serikali.

"Niseme tu kwamba sikukurupuka na siwezi kukurupuka katika uamuzi wowote na katika hilo naona hana haki hata kidogo kwa kuwa hana hati halali ya eneo hilo na kama ameruhusiwa ni kinyume cha sheria hivyo sitabadili uamuzi wangu," alisema Prof. Tibaijuka na kuongeza;

"Ndio maana wakati nafanya maamuzi hayo sikuwa peke yangu, nilikuwa na Katibu Mkuu, Wataalam wengine wa wizara, Naibu Waziri wangu na wadau wengine hivyo nitahakikisha nasimamia uamuzi wangu kwa ajili ya Watanzania," alisema Prof. Tibaijuka.

27 comments:

  1. That is it Prof, fanya kazi yako , mngekuwa kumi kama wewe roho yangu ingesuuzika. Tunahitaji mawazili watekelezaji kama wewe na si waongeaji tu. Asikutishe huyo mwarabu ukoko

    ReplyDelete
  2. That is excellent mama. You are now representing the many women that could be leaders if given opportunity. Please follow up the isssue to the end. hawa makwablela tumeachoka

    ReplyDelete
  3. NI JAMBO LA KWELI NA LA KISHANGAZA PIA KWAMBA WAARABU NA WAHINDI NDIO WANAOTUCHAFULIA AMANI, UTULIVU,MSHIKAMANO NA HAKI YA NCHI YA TANZANIA NA WATANZANIA. HAWAFIKI HATA 1% YA POPULATION LAKINI KWA KUWANUNUA VIONGOZI WETU WASIOJALI NA KUTUMIA IKULU NA MAHAKAMA WATATUPA SHIDA SANA TUPIPOANGALIA!KUSEMA TUNAWABAGUA NI UPUUZI MTUPU MAANA WAO NDIO WANATUBAGUA NA KUTUIBIA. MAMA PROF SONGA MBELE. HAWA HAWAKUJUI. WAO WANA PESA WEWE UNA HAKI YA MUNGU.

    ReplyDelete
  4. NAKUPONGEZA SANA MAMA TIBAIJUKA SONGA MBELE NA DIRA NI ILE ILE ALIYOIANZISHA MH,LUKUVI NA KUONA UBADIRIFU NA UTAPELI ULIOFANYWA NA WIZARA YA ARDHI WAKISHIRIKIANA NA HALMASHAURI ZA JIJI. KUHUSU MTOA MAONI NO 3 WA 11.29 KUSEMA WAARABU NA WAHINDI HUO NI WIVU WA AKILI KABISA NA UBAGUZI MAANA HAPA HAKUNA UHINDI WALA UARABU HAO NI RAIA KAMA WEWE,NA HUYO SUMAYE ALIENUNUWA EKA 500 KILOSA NAE MHINDI? NA HUYO MUNGAI ALIENUNUWA ENEO LA WAZI HUKO MSASANI NAE MWARABU? KAMA HUNA LA KUSEMA KAA KIMYA

    ReplyDelete
  5. Mama kaza buti mwanamke mwenzetu huyo mhindi asikutishe mafisadi wakubwa hiki sio kipindi cha ufisadi kama wanavyodhani ameng'ang'ania kiwanja toka mwaka 1975 kama sio ufisadi ni nini kiwanja kina umri wa mwanadamu kwa nini kama ni cha halali asikiendeleze kweli wewe mhindi koko rudi kwenu ukale pilipili acha kumtishia mama yetu PROFFESOR ajuae mazingira

    ReplyDelete
  6. Watanzania kuweni macho na magabacholi! Gabacholi gabacholi wasitishe nchi. Wakitaka wafuate sheria na wawaheshimu wazawa halisi. Ama sivyo, matatizo tu.

    ReplyDelete
  7. Mama Tiba angalia vilevile na hao maofisa waliotoa viwanja hivyo,wawajibike kama waligawa kinyume badala ya kushughulikia upande mmoja.

    ReplyDelete
  8. Sawa namsifu Mhesh.Mama Tiba kama ataendaendelea na msimamo wake huo. Ila wasiwasi unaoanza kuupata ni kwamba kumbe wapo viongozi na wataalamu ambao wapo nyuma ya ufisadi huo ndio maana wahusika wana nguvu za kukimbilia mahakamani. Sasa je Waziri anaonaje kama angeanza kushughulikia kwanza hao wataalamu na viongozi waliohusika kupitisha kazi hizo kabla ya kwenda mbali??

    ReplyDelete
  9. Sio Magabacholi tu hata Wachaga ni wengi sana wanaohujumu uchumi wetu. Mama Tibaigana sidhani kama umeangukia kukomoa jamii fulani zaidi ya sheria,tuna tabia ya kunyooshea wengine vidole lakini unapomnyooshea mwenzio kidole angalia kuna vingine unajinyooshea mwenyewe,wapo wapumbavu wengine tayari wameshaanza ujinga kwa kunyooshea vidole rangi fulani kutokana na yaleyale ya udini,sasa Mungai,Sumaye na wachaga wengi pale Arusha,Dar na kwingineko wamefanya mambo ya ajabu sana kwa jeuri ya pesa yao.bila kusahau wazungu na migodi,mbona hawa hamuwataji? Msiharibu mazuri aliyokusudia mama huyu. Nakumbuka wakati Mwalimu Nyerere alipotangaza azimio la Arusha alianza na jamii hiyo na baadaye akawageukia waafrika hapo jamaa wakaanza kumchukia Nyerere,uzuri Nyerere alikuwa muwazi sana hakuwaficha aliwaambia wazi bepari hana rangi hivyo atamshughulikia yeyote awe matumbi,muarabu au mhindi.poleni sana Watanzania sumu ya ubaguzi aliyoisema Nyerere kabla hajafa ndio hii inaanza kuwatafuna,mtaanza kubagua mhindi na mwarabu mkimaliza mtaanzana wenyewe kwa wenyewe. huyo mjinga aliyeanza kusema waarabu na wahindi ndio hao waliongia mjini na matongotongo.ustaarabu bado uko mbali na yeye. leo hii mmatumbi ndie rais wa marekani kama wao walioendelea wameweza kumchagua huyo mmatumbi sembuse wajinga nyie? huyu mama anajaribu kuweka utawala wa sheria ambao umepotea katika nchi yetu kwa sababu kila mtu anajifanyia kivyake maadhali mbele kuna pesa,haki haiendani na rangi ya mtu bali inaendana na haki,ndio maana mtuhumiwa alisema atakwenda mahakamani na waziri kamjibu tutakutana huko,acheni sheria ifanye kazi na huyu mama afanye alilokusudia,mkianza hayo mliyoyaanza kila mtu ataanza kutetea kivyake. HONGERA MAMA KAZANA SANA.

    ReplyDelete
  10. Mkono wa Mungu na ukuongoze

    ReplyDelete
  11. Huyu alieandika hapa juu ni kichaa, kasuku au ni mwendawazimu. Yaani maelezo yake yanaonyesha jinsi alivyo hovyio, sijui sura yake, tabia yake na roho yake mbaya anamuonyesha nani. Hawa wachaga wameingiaje hapo. Inaonyesha alikuwa anamtaka mchaga lakini mchaga kamtema.

    ReplyDelete
  12. Kwa kweli wachaga wanasumbua sana kwenye viwanja kila mahali wanazua migogoro ya kutanua mipaka, kutapeli viwanja,dhuluma na kila choko choko. Yaani mchaga akiwa jirani yako una kazikubwa!!!!!

    Wachaga jirekebisheni, Msikimbilie kudai ukabila, jichunguzeni na mjirekebishe

    ReplyDelete
  13. Hongera Mama Tibaijuka. Mungu akuzidishie uone hata Temeke kulivyoingiliwa na ujenzi wa Vituo vya mafuta kwenye maeneo ya wazi na makazi ya watu. Tuombe Mungu janga la moto lisije kutokea!!!!.
    WAtanzania tuache ubinafsi wa kujaqli fedha bila kujali utu wa Watanzania wenzenu. Pesa hazitawazika!!!!.
    HONGERA MAMA TUNAKUHITAJI SANA.

    ReplyDelete
  14. songa mbele Prof wa ukweli sio akina Prof Mungai waliokuwa mawaziri na wakatuingiza choo cha kike, fanya kazi yako kama waziri uliyechaguliwa na rais na sis wananchi tupo nyuma yako. kama huyo ponjoli anaweza kusimama na wewe kuhusu hilo basi ameiingia chaka kwanza hawa akina patel ni mafisadi wakubwa hapa nchini na kuna wengine bado wana kesi ya kujibu. inawezekana amepata hivyo vibali kutoka huko juu kwenye ofis ya rais ndio maana anajeuri but Mungu atakusaidia Mama na sheria ipo,endeleza mapambano ili hao mafisadi wakujue wewe ni nani na huhitaji vijicent vyao kwa kuwa ulishafanya sehemu mbalimbali mpaka UN.hakuna wa kukubabaisha.

    Na nyie watoa comment acheni ukabila, sisi tupo kwa ajil ya kujenga nchi na si kubomoa, so toeni comment za kujenga.

    ReplyDelete
  15. Hakuna ubishi kwamba Waarabu na wahindi ndio wanaofaidi uhondo na kila kitu cha Tanzania. Ubaya zaidi wameishika system nzima ya nchi yetu. Hii yote ni kwa ajili ya jeuri ya fedha walioyonayo. Ukienda ardhi wameshika system nzima wachora ramani, watu wa mipango miji wote wako chini yao. Ukienda mahakamani wameshika hata system ya mahakama zetu zinatoa uamuzi wa kuwafavor, yote hiyo ni fedha waliyonayo. Kwenye siasa wameshika viongozi wote wenye influence ya kutoa maamuzi yote hiyo ni fedha waliyonayo. Watanzania ifike mahali tuseme inatosha sasa! Na amani ya nchi yetu ipo hatarini kwa ajili ya hawa wahindi na waarabu. Tulipiginia uhuru ili tuwe huru badala yake wanaomilki nchi hii ni hawa wahindi na waarabu. Itafika mahali tuwaambie warudi kwao Uarabuni na India ili watuachie nchi yetu. Ninajua wapo baadhi ya waarabu na wahindi wazuri tu wanafuata sheria na wanaona haifai kuichezea nchi kwa sababu ya fedha uliyonayo lakini wengi wao ni watu wabaya kabisa na wala hatuwahiji.

    Ni naomba kila mwenye mapenzi mema na nchi yetu Tanzania amuunge mkono huyu mama professor Tibaijuka ambaye ameonyesha uzalendo wa hali ya juu. Siyo tu kumuunga mkono lakini pia apewe ulinzi. Hawa waarabu na wahindi ni watu wabaya sana, wanaweza kabisa kumzuru huyu mama. Kwani wana fedha na ni watu jeuri kabisa. Wanaweza kununua mtu hata akaenda kumgonga na gari na kesi ya huyo mtu ikaisha hivi hivi. Jamani tumwombee ulinzi wa Mungu huyu mama na kuomba kwamba watu waone wanawake wakipewa nafasi wanaweza kufanya vitu vinavyoeleweka.

    Rushwa kubwa jamani ipo ardhi na inafanywa zaidi na Waarabu na Wahindi. Wahindi na waarabu wameiweka system nzima mifukoni mwao hata serikali iko mifukoni mwao. Mama Tibaiijuka anasema sasa inatosha tumunge wote watu wenye mapenzi mema na nchi. Mungu akupe maisha marefu Professor Tibaijuka

    ReplyDelete
  16. ndg zanguni watanzania kisa nini kutupiana maneno makali na yenye hasira.? nafiki sote tumpe moyo waziri kwa hili alilolosema, hatua haijachukuliwa wenyewe kwa wenyewe tumeanza kutoana macho haifai tupendane nchi ni yetu yule aliyeenda tofauti bila kujali kabila wala dini yake , kama serikali imeamka basi atuko naye keki ya nchi hii ni yetu sote.

    ReplyDelete
  17. WACHAGA HAWANA TOFAUTI NA MAGABACHOLI. WALE WAZUNGU KULE MIKOA YA ZIWA MMEWASAHAU? AU BADO MKO WATUMWA KWA WAZUNGU?

    ReplyDelete
  18. Aisee kumbe ujinga uko bado nchini mwetu,rushwa anatoa mhindi na mwarabu tu? poleni sana. rushwa haina rangi wala kabila wala dini,hivi waarabu/wahindi wanamiliki asilimia ngapi ya ardhi nchii hii? Sumaye pekee yake ametajwa kumiliki ngapi? tena kapora wanakijiji,Mungai,nenda Morogoro kule uone jamii iliyotajwa hapo juu ilivyohodhi ardhi,tuache ujinga,Tibaigana shughulikia wote bila kujali rangi wala kabila,mambo akifanya mchaga sawa akifafanya mtanzania mwenye asili ya kiarabu nongwa.ni sumu hiyo. ubadhirifu wa ardhi nchi hii unaongozwa na watu wenye pesa wa mikoa ya kaskazini.

    ReplyDelete
  19. kila mtu ana hak ya kutoa mawazo na maon yake kama unampinga mpinge kwa hoja na sio matus

    ReplyDelete
  20. NYIE WATANZANIA MSIRUKIE GARI KWA MBELE,FUATILIENI KISA KIZIMA MJUE KOSA LIPO WAPI,SIO KUSHANGILIA UPUUZI BILA KUJUA CHANZO.

    HAPA TUNATAKIWA KUJIULIZA SANA,KABLA YA MAMA TIBA HIVI HAWAKUWWEPO WENGINE WALIOKUWA WANAONGOZA WIZARA HII? WAO HAWAKULIONA? NA WALIOSAINI HIZO NYARAKA WAO NI WENDA WAZIMU?
    NADHANI TUNGEMSHAURI MAMA TIBA AWASHUGHULIKIE KWANZA HAWA WALIOSAINI HIZO DOCUMENTS HALAFU NDO TUMFUATE HUYU JAMAA ATUAMBIE UKWELI,MANAKE HADI MAHAKAMA IMETOA AMRI HALALI,SASA MAKELELE YA NINI? MSIMPE MAMA TIBA MZUKA WA BURE HALAFU KESHO MUANZE KUSEMA HAFAI,MANAKE TUNAWAJUA SANA KUSHABIKIA MAMBO HALAFU KESHO MNAGEUKA.PIA KAMA HAKUNA ATHARI ZOZOTE KITAIFA TUACHE ACHAPE KAZI SI ANALIPA KODI AU MNATAKA MUENDELEE KUJAZA MIKOJO YENU NA VINYESI BILA KULIPA KODI? TUWE WAPOLE JAMANI

    ReplyDelete
  21. Wakati Mwalimu alivyoenda U.N mara ya kwanza kuomba uhuru aliuahidi Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tanzania itakuwa nchi ya kiafrika kwasababu weusi ndiyo sehemu kubwa ya watu wa Tanganyika.lakini pia itaheshimu na kuzilinda haki za wachache wasiokuwa waafrika kama vile nchi hiyo itavyolinda haki za waafrika.

    Wakati anawahutubia wanahabari kwenye ukumbi wa Habari Maelezo mwaka 1995 akasema tena "hatukuwa tunawachukia makuburu kwasababu ya rangi zao bali kwasababu ya ubaguzi wao.Hivyo watanzania wawachukie pia makuburu weusi."

    Inasikitisha kuona leo miaka 49 baada ya uhuru tunaona watu wa nashindwa kujadili hoja wanaanza kurukia ubaguzi.Wanachomaanisha ni kuwa weusi wenzetu ambao wamevamia viwanja vya mipira na kujenga vituo vya mafuta waachwe tu kwasababu ni weusi.

    Sisi ni watu wazima.Tuone haya kabla ya kusema mambo mengine.

    Mungu Ibariki Afrika,

    Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  22. Muccadam ni mmojawapo wa kizazi cha mafisadi ambao wanaitafuna nchi hii toka wakati wa ukoloni huku mifukoni mwao wakitembea na passport ya Canada. Asikutishe Prof. Tibaijuka, tuko nyuma yako.

    ReplyDelete
  23. DOKEZO!

    Nawaombeni tuwe makini tunapojadili hoja, hii hoja ni ya msingi inahusu usawa na haki ya kila raia katika matumizi ya rasilimali ardhi ya Tanzania!

    Sasa naona hoja hii inaanzan kutumbukia nyongo mbaya na hatari ya ubaguzi! Uhindi, Uarabu na Uchaga! Tukimaliza hizi tutaanza na ubaguzzi wa Dini! Hoja hizi hazijengi na si lengo la Mama Tibaijika na kila Mtanzania Mzalendo!

    Tujadili kwa hekima bila kumuumiza mtu yeyote kwa sababu alivyo! Kuna Wahindi pale Shinyanga hata chakula cha mchana wanapata taabu kula! (Hawana Hela) Hawa nao tunawaweka kundi gani?

    Hebu tuachane na ubaguzi huu!! Ni matumaini yangu baada ya comment hii sintaona tena na Watanzania hawatarajii tena kuona comments za ubaguzi badala yake tutajadili hoja iliyopo mezani!

    Mungu Ibariki Africa, Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  24. INASIKITISHA KUONA NCHI HII TUNAO VICHAA WENGI BADO MNAJADILI VITU KWA UBAGUZI BILA KUANGALIA UKWELI MMEPOTEA NYOTE NYIE

    ReplyDelete
  25. kila kitu na wakati wake na sheria ina wakati wake.kuna wakati tunahitaji nguvu. kuna wakati tunahitaji sheria.sasa hivi ni wakati wa amani ni wakati wa sheria sasa nasema kelele za nini wacha sheria ichukue nafasi yake.sio mwananchi au waziri mwenye nguvu wote nisawa mbele ya mahakama wacha sheria ichukue nafasi yake.

    ReplyDelete
  26. La msingi ni sheria kufuata mkondo wake, haijalishi ni kwa nani.katika kila jamii kuna wema na wabaya , mbaya ahukumiwe kwa ubaya wake si kwa rangi yake au uasili wake.Tuachane na chuki binafsi

    ReplyDelete
  27. Mama Tibaijuka endelea mbele kwa mbele usimuache wa kabila lo lote madhali amevunja sheria!

    ReplyDelete