17 December 2010

Mzungu kurekodi sauti ya Nyerere kwa kuigiza

Na Tumaini Maduhu

MSANII chipukizi na mchekeshaji Simon Mzungu, anatarajia kuandaa sauti ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ikiwa ni njia mojawapo ya kumenzi.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, alisema sauti hiyo itabeba ujumbe
wa kupenda kazi za sanaa.

Alisema wadau, mashabiki na taasisi mbalimbali, zitarajie kupata mambo mazuri kutoka kwake, kwani sauti hiyo itakuwa na ujumbe mzuri kwa kila mtu.Ninaamini kupitia sauti ya mwasisi wa taifa letu, tutajifunza mambo mengi, pia tutakuwa tukienzi utamaduni wetu kupitia ngoma, ngonjera,¡± alisema.

Msaniii huyo alisema, licha kuweza kutoa sauti ya Mwlaimu Nyerere, alisema anakabiriwa na changamoto nyingi ikiwemo kuungwa mkono na waandishi wa habari.Ninawaomba waandishi wa habari mjitahidi kututangaza wasanii chipukizi ili tujulikane kwenye soko la sanaa,¡± amesema.

No comments:

Post a Comment