17 December 2010

Netiboli Morogoro wakumbwa na ukata

Na Lilian Justice, Morogoro

CHAMA cha Netiboli  Mkoani Morogoro 'CHANEMO', kinakabiliwa matatizo mbalimbali likiwemo la kutokuwa na fedha na vifaa vya mchezo huo.
Matatizo hayo yanawafanya washindwe kushiriki kwa wakati mashandano ya kombe la Taifa la
  yanayotarajiwa kufanyika mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro, Mwenyekiti wa chama hicho, Kaundime Kizaba, alisema timu ya Mkoa ya netiboli, imeandaliwa kwa mashindano ya Taifa, lakini wamekumbwa na tatizo la ukosefu wa fedha.

Alisema fedha hizo zingewasaidia kuwasafirisha wachezaji mpaka mpaka mkoani Pwani, kwenye shule ya Firbet Bay, ambako yatachezwa mashindano hayo.

Kaundime alisema wanahitaji kiasi cha sh. milioni 2, ambazo zitatumika  kununulia madawa, usafari na maji  wakati wa mashindano na matumizi mengine madogo madogo.

'' Timu haina vifaa, kama mipira, jezi, kwani watakazitumia wameazima kutoka katika timu za  Polisi, Magereza na timu ya kampuni ya Tumbaku ya TTPL. Alisema, awali bajeti ya timu hiyo ilikuwa ni sh. milioni 18, lakini walipunguza ili timu iweze kufika mkoani Pwani.

Kaundime amewataka wadau wa michezo, kuwasaidia ili waweze kufanikisha malengo yao.Alisema katika jitihada zao za kutafuta msaada, wamekosa ushirikiano na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kwani walikuwa wakienda kwenye ofisi za Katibu Tawala (RAS), lakini hawasaidiwi.

No comments:

Post a Comment