17 December 2010

Dodoma, Morogoro, Mwanza zaanza vizuri netiboli Taifa

Na Amina Athumani, Kibaha

TIMU ya netiboli ya Mkoa wa Dodoma, jana imeanza vema mashindano ya Taifa kwa kuifunga Mtwara mabao 43-19, mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Filbert Bay, Kibaha, Pwani.Hadi mapumziko, Dodoma ilikuwa
mbele kwa mabao 22-9, katika mchezo uliokuwa na upinzani mkubwa, licha ya timu pinzani kushindwa kufunga mabao.Michuano hiyo ilianza jana.

Katika mchezo wa pili, Morogoro ilianza vema dhidi ya Lindi kwa kuifunga mabao 35-7, hadi mapumziko, ilikuwa mbele kwa mabao 16-6.Katika mchezo wa tatu, Mwanza iliibuka kidedea baada ya kuifunga Arusha mabao 25-17, mpaka  mapumziko,  Mwanza ilikuwa mbele mabao 13-7. Michezo yote ilichezwa asubuhi.

Wakati huo huo, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Iddi Azan na John Mnyika wa Ubungo, wameipiga tafu timu ya Kinondoni kwa kuwapa ufadhili na chakula katika kipindi chote cha mashindano.

Mashindano hayo yanashirikisha mikoa 15 ya Tanzania Bara, yanatarajiwa kumalizika Desemba 23.  Mkoa wa Pwani ni bingwa mtetezi.

No comments:

Post a Comment