22 December 2010

Nahodha, Kwambwa watinga UDOM

Na Pendo Mtibuche, Dodoma

SIKU moja baada ya kutokea kwa mgomo na kufanyika kwa  maandamano ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma na kusababisha vurugu zilizopelekea polisi kuwatawanya kwa virungu na mabomu ya machozi, Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Bw. Shamsi Vuai Nahodha na yule wa Elimu na Mafunzo ya Ufusdi, Dkt. Shukuru Kawambwa wamefika chuo hapo ili kufanya mazungumzo na uongozi wa chuo na Serikali ya Wanafunzi ili kupata ufumbuzi wa tatizo lililopo.

Wanafunzi wa chuo hicho walifanya mgomo na kutaka kuandamana kuelekea katika Ofisi ya Waziri Mkuu, wakidai fedha kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na kulalamikia uchafu wa mazingira.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. James Msekela alifika  chuoni hapo na kuwasihi wanafunzi hao kuingia madarasani na kuendelea na masomo wakati matatizo yao yakishughulikiwa, lakini hawakukubali.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu baina ya uongozi wa wanafunzi na serikali ya Mkoa kushindwa kufikia muafaka, Polisi waliingilia kati na kuwatawanya wanafunzi kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha na kuwajeruhi wengine na kuwatia nguvuni ambapo wanaoshikiliwa ni pamoja na Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Bw. Leonard Singo.

Baada ya mazungumzo hayo ilielezwa kuwa litatolewa tamko ili kurudisha hali ya amani na utulivu chuoni hapo.Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idrissa Kikula alisema kuwa suala hilo walishazungumza na lipo katika mchakato.

Alisema kuwa yeye kama mzazi alisikitishwa na tukio hilo na chuo hakitafungwa, hivyo wanafunzi wataendelea na masomo huku masuala yakiendelea kushughulikiwa.

Profesa Kikula alisema kuwa katika mazungmzoa na Waziri Nahodha na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, imeundwa tume ya watu watano ambayo itatoa ripoti baada ya siku tano.

7 comments:

  1. HIVI KUNA NINI HUKO TANZANIA KWETU MBONA MAMBO HAYAELEWEKI? HIVI SERIKALI INAWANYANYASA WANAFUNZI KWANINI? KUTOA PESA ZA MAFUNZO KWA VITENDO HADI ZIOMBWE KWA MAANDAMANO? KWANINI KUSIWEKWE UTARATIBU KABLA YA WAKATI..SERIKALI INATIA AIBU.
    FROM BUFFALO NY

    ReplyDelete
  2. MI NAWASHANGAA SANA HAO WANAFUNZI WA DOM...
    WAO SI NDIO WALIMCHANGIA PESA ZA KUCHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAISI...SASA MNALALAMIKA NINI?... ATA BADO SI PESA ZA VITENDO TU ATA ZA NADHARIA HAMTAPEWA...MUTASHIKA ADABU ZENU...SHAME ON U...!

    ReplyDelete
  3. HIki chuo cha kata kinaleta aibu kabisa. Kinatakiwa kiisikilize serikali yake. Kama hawakukanusha kuwa wao sio chuo cha ccm na sera yake ya elimu katika kila kata . UDM ikiwa moja ya kata hizo, itakwua upumbavu kushirikaina nao hawa premature katika vita ya ukombozi.

    Watoe tamko kuwa wanalaani wenzao kuwa wao sio sehemu ya chama, vinginevyo wataonja joto ya jiwe. Wao hawajui kwenye chama ni wachache wajanjawajanja wanakula kwa niaba ya wajinga wengi. Wengine huku ni watoto wa wakulima.

    Sasa elimu hiyo itaacha kuwa ya kata kweli kama haina vitendo, wakati sahihi wa kupeleka madai yenu ilikuwa wakati kabla ya uchaguzi - sasa serikali yeni imemalizia pesa kwenye uchaguzi - hata mawaziri wanalipwa kwa kusubiriana, sembuse ninyi....

    Mtafanya vitendo mkiwa kazini. lazima mtubu kwa umma wa watanzania, ili waweze kuwasupport, vinginevyo, ninyi ni tawi la chama, na mkitaka kujua maana ya tawi la ccm ndio hiyo, mmoja anakula badala yenu.

    Toeni tamko la kukataa kuwa ile aibu haikuwa tamkolenu!!

    Poleni, mkale sangara mtapata akili.....

    ReplyDelete
  4. Mh.kawambwa ninaomba utumie hekima zako bila kupendelea upande wowote ule.

    ReplyDelete
  5. udom acheni kukichafua chama chenu ccm,hatuwahitaji kwenye ajira manake mtaleta uccm mawazo mgando.inafaa mlaani kitendo cha wenzenu kuandamana,Watanzania tunataka mupigwe sana,muonewe ili akili ziwakae sawa

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli hayo ndiyo matunda ya vyuo vya kata na kwa mtindo huu hata kazini wata-behave kikata kata tu kwa uduni na ufinyu wa ukombozi wa kifkra.Haya nirudi kwako ndugu wa mambo ya chumbani utayaweza hayo!!!!ulikuwa umezoea rusha roho hapa petu, huko bara ni rusha bongo.Kazi kwako kaka.

    ReplyDelete
  7. HATA HIVYO HAKUNA ASSESSMENT MLIZOFANYIWA KWENYE MAZOEZI YA VITENDO BADALA YAKE YALIKAGULIWA MAFAILI. HII ELIMU GANI? NDIO MAANA HAMJUI HATA KUDAI HAKI ZENU ZA MSINGI. BADILIKENI MUWE WASOMI WANAOENDANA NA CHANGAMOTO ZA MABADILIKO YA KISASA!

    ReplyDelete