22 December 2010

Mtandao Tigo wageuka kero kwa wateja

Na Job Ndomba

WATUMIAJI wa simu za mkononi kwa mtandao wa Tigo juzi na jana walijikuta katika wakati mgumu baada ya kukosa mawasiliano kwa saa kadhaa.
Tukio hilo lilianza juzi mchana na kuzua usumbufu mkubwa miongoni mwa watumiaji wa
mtandao huo.

Wakizungumza na Majira baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walisema kuwa tatizo hilo limezua usumbufu mkubwa, kwani wafanyabiashara, wafanyakazi wa maofisini na wengine wengi walishindwa kutekeleza mipango yao iliyotaka mawasiliano ya simu.

Mmoja wa wakazi hao aliyejitambulisha kwa jina la Emilian Philipo alisema tatizo hilo lilimpa usumbufu mkubwa kwani huduma zote za tigo zilikuwa hazifanyi kazi kuanzia kuuliza salio, kupiga, kutuma ujumbe na hata kupata huduma ya wateja.

"Tatizo hili si la kufumbia macho wala kulichekea kwani kwa watu kama wafanyabiashara ni hasara kubwa na huenda wakawa wamepoteza mamilioni ya fedha kwa kukosa mawasiliano, nadhani watuombe radhi," alisema Philipo

Kutokana na malalamiko hayo, Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya TiGO, Jackson Mmbando aliwaomba radhi wateja wao kwa usumbufu waliopata kwani ni tatizo la kiufundi.

Alisema tatizo hilo limetokea kutokana na hitilafu ndogo kwenye moja ya mitambo yao na kuwa jana walikuwa katika hatua za kuiongezea nguvu ili iweze kutoa huduma bora zaidi.

Tatizo hilo halikuwawakumba wakazi wa Jiji la Dar es Salaam pekee bali pia wa mikoa mingine kama vile Jiji la Mwanza na Arusha.

Mkazi wa Jiji la Mwanza, Bi. Zamda Ally alisema jana kwa saa tatu hakuweza kupata huduma yoyote ya TiGo kwani hata alipokuwa akituma ujumbe wa maneno (SMS) zilikuwa haziendi.

Mkazi mwingine wa Jiji la Arusha, Bw. John Ngunge alisema naye pia alikumbwa na tatizo hilo na kuwaomba wahusika kuwaomba radhi Watanzania kwa kushindwa kuwapa huduma waliyokuwa wakistahili.

"Nadhani kwa hili wanatakiwa watuombe radhi kwani tumepata usumbufu mkubwa na pengine wengi wameshindwa kupata vitu walivyokuwa wakivitarajia hasa katika sekta ya biashara," alisema Ngunge.

8 comments:

  1. Tigo acheni uzembe tutawakimbia mda sio mrefu. Huduma zenu ni duni sana ikilinganishwa na watoa huduma nyingine ninachopendezewa nanyi ni bei nzuri tu ila kama mtaendeleza huduma zenu mbovu bila shaka nitawakimbia

    ReplyDelete
  2. Ndo maana sie wengine tunatumia THURAYA !!kwa kuogopa hayo.....
    Sanawari

    ReplyDelete
  3. kwel bhan sio ishu alafu watu wenyewe masharti kibao kama waganga wa kienjeji

    ReplyDelete
  4. kama vp serikali iwapumzishe nini coz cku hiz tigo mashauz kibao wanawaringia wateja [clemence wa mbeya kata ya nonde]

    ReplyDelete
  5. Tigo mtambue kwamba 2po kwenye dunia ya soko huria!2tawakimbia sisi!

    ReplyDelete
  6. tutahama wote tuone kama watakula hiyo minara yao. kazi zinalala bila mawasiliano na wao wamekekaa kimya hata hawatoi tamko.

    ReplyDelete
  7. Ndiyo matatizo ya vitu rahisi rahisi, hata walio nje ya nchi wakiwapigia ndugu zao wenye kutumia TIGO hawapati mawasiliano mazuri huwa yana katika katika ghafla bila sababu yeyote.

    ReplyDelete
  8. raisi uwa khali na mkaidi afaidi ila kurejea mara mbili mimi na amini shibe na umaarufu una wadekeza ila jueni ya kwamba mti hauwezi kuna wiri bila ya shina hii ni takwimu fikirieni kwa kina tigo bay bay endapo hamtojirekebisha.

    ReplyDelete