14 December 2010

Ajifungua wapacha watano Shinyanaga

*Ni mimba yake ya kumi
*Sasa afikisha watoto 13


Na Patrick Mabula, Kahama

MWANAMKE mmoja mkazi wa Kijiji cha Bulungwa Kata ya Bulungwa, Wilayani Kahama Bi. Shija Maige (33) amejifungua watoto watano, kati yao
wa kike watatu na wawili wa kiume.

Bi. Maige alijifungua juzi katika Kituo cha Afya cha Bulungwa na baadae kuhamishiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kahama kwa ajili ya kupata huduma na watoto wake watano ambao wote wako hai.

Kwa mujibu wa mama huyo, mimba hiyo ya watoto 5 ni ya 10 maishani mwake, akiwa amefikisha jumla ya watoto 13 sasa. Wauguzi wa Hospitali ya Wilaya walisema mwanamke huyo alifikishwa hapo saa 12 alfajiri juzi na gari la kubeba wagojwa lililokwenda kumchukua baada ya kutolewa kwa taarifa juu ya tukio hilo na ombi la kupatiwa huduma zaidi.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama Bw.Leonard Subi alisema kuwa Bi. Maige alianza kupatwa na uchungu wa kuzaa na kuanza kujifungua akiwa nyumbani kwake ndipo familia yake ilipomkimbiza kwenye Kituo cha Afya cha Bulungwa.

Dkt. Subi alisema baada ya kufikishwa hapo wauguzi wa kituo hicho cha afya, waliweza kumhudumia hadi gari la wagonjwa lilipokwenda kumchukua kumpeleka Hospitali ya Wilaya, ambapo alipofikishwa alilazimika kuongezewa damu kutokana na upungufu uliokuwa umesababishwa wakati wa kujifungua.

Akieleza juu ya uzito wa watoto waliozaliwa alisema wako katika kati ya kuanzia Kg . 1. 250 gm hadi kg. 1.700 gm na kuwa uzito huo uko chini sana kwa vile wastani mzuri wa watoto kuzaliwa nchini Tanzania ni wastani wa kuanzia Kg. 2 . 5 gm kwa hiyo walikuwa katika mkakati wa kuondoa upungufu huo ili uzito uweze kupanda kitalaamu.

Akizungumza na Majira, Bi. Maige akiwa katika wodi ya wazazi alisema mimba hiyo aliyozaa watoto hao ni ya 10 maishani mwake.Alieleza pia kuwa alishajifungua mapacha katika siku zake za nyuma katika  mimba yake ya sita na sasa amefikisha watoto 13 pamoja na hao watano.

Bi. Maige akiwa na afya jema alisema ameolewa na anaishi na mume wake aliyemtaja kwa jina la Bw.Charles Marco ambapo ameomba msaada toka kwa wasamaria wema pamoja na mashirika mbali mbali ya kulea watoto wake hao.

12 comments:

  1. Aelimishwe juu ya uzazi wa mpango na ikibidi afungwe uzazi! watoto 13 wanamtosha kabisa na still anaomba msaada! Mungu mkubwa hata kuona kajifungua salama tena nyumbani!

    ReplyDelete
  2. NAOMBA AELIMISHWE KUHUSU UZAZI WA MPANGO KWANI KUZAA BILA MPANGO SI ISSUE, ISSUE NI KUZAA WATOTO UNAOWEZA KUWATUNZA.

    ReplyDelete
  3. Suala sio uzazi wa Mpango hapa,suala ni kuzaa watoto watano kwa mkupuo,hiyo ni issue na matuzno yake inabidi asaidiwe,hakuna awezaye kutunza watoto wachanga watano kwa pamoja,labda Rostam Aziz.

    ReplyDelete
  4. Naomba huyo mama afungwe kizazi kabisa kwa hao watoto13 its enough for now.maana siku hizi kuna magonjwa vifo wazizi wanaweza kufariki watoto wabaki yatima bila malezi. kwa ushauri wangu ni vizuri zaidi afunge kizazi tena ikiwezekana saiz.

    ReplyDelete
  5. TUPENI BANK ACCOUNT NAMBA YA HUYO MAMA/BABA TUMCHANGIE PESA KIDOGO NA FAMILIA YAKE. NINAHIDI NITAMCHANGIA LAKI MBILI NA NAAMINI MUNGU ATAICHUKULIA KAMA SADAKA KWANGU PIA. SUALA LA ELIMU YA UZAZI PIA LINAKUJA KAMA CHANGA MOTO KWETU SOTE.

    ReplyDelete
  6. mwanamke jasiri

    Huyu mama anastahili kusaidiwa na serikali hasa hao mapacha watano ili waweze kukua vema na tupate mfano duniani wa watoto watano kwa uzazi wa kawaida tena maisha ya kijijini.

    She is very brave. Mungu ambariki sana

    ReplyDelete
  7. jamani huyo Baba watoto wake inaonekana hana uruma na huyo mke, mimba 9 na bado walikuwa wanataka watoto wengine, au tajiri sana? pole sana mama , mungu atakusaidia utapata wafadhili, ningekuwa na pesa ningekusaidia lakini nasitikika mimi bado mwanafunzi, Serikali yetu hebu angali swala hili , mlifanyie kazi kuwaelimisha wakinamama na wakina baba pia, juu ya uzazi wa mpango.

    ReplyDelete
  8. Hii sii kawaida ila Apewe mungu sifa maana ni viumbe vyake. ikiwezekana gazeti la Majira tuwekeeni account number yake kweny mtandao wenu tumsaidie huyu mama angalau kifedha. Hongera sana mama Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  9. Mungu mwema, mume wa mama huyo si wa kulaum hayo ni mapenzi ya mungu, kwani wapo watu wengi wanatamani kuzaa japo mtoto mmoja lakini hawajafanikiwa .Yote ni mipango ya Mungu.Majira wekeni account tuanze kuchanga faster hao wapwa zetu watano waanze kula maisha kwa kupata RISHE BORA.

    ReplyDelete
  10. Kweli mama huyu anahitaji msaada, atawezaje kuwatunza watoto hawa jamani? Kweli watanzania mliojaliwa nafasi kidogo muangalieni mama huyu! Mungu atawarehemu.

    ReplyDelete
  11. Mwandishi wa makala hii tunakushukuru sana kwa kutupa taarifa za ndugu zetu wa Kahama; lakini tunakuomba uwe mwangalifu na utumiaji wa maneno ya Kiswahili; sina hakika kama "wapacha" ni Kiswahili sanifu au kitarafa! Wingi wa pacha ni pacha na sio mapacha au wapacha.

    ReplyDelete
  12. jamani kwanza nampa hongera kwani amepitia mengi mno watoto kumi na tatu sio mchezo ee kweli huyo ndiye ametimiza agizo la Mungu la kuijaza nchi.nampa hongera ndugu zangu ni vema tukamsaidia mwenzetu.tusisaidie wakati amekufa mtu tu bali akiwa mzima tusaidiane.na serikali tunaomba mchango wake hiyo account iwekwe mapema jamani.Mungu amsaidie sana.

    ReplyDelete