08 December 2010

Mbwete kutoa mhadhara wa kiprofesa keshokutwa

Na Edmund Mihale

MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu Huria nchini, Profesa Tolly Mbwete keshokutwa anatarajia kutoa mhadhara wa kiprofesa ikiwa ni miaka ya mitatu baada ya kutunukiwa hadhi hiyo kitaaluma.Mhadhara huo ambao utakuwa ni wa kwanza kutolewa katika
chuo hicho tangu kianzishwe mwaka 1992, ni moja ya mikakati ya wanataaluma wa chuo hicho kunoa bongo zao.

Prof. Mbwete analeta mada inayohusu ubora wa maji ya chupa na tahadhari ya ongezeko la wajasiriamali wanaotoa huduma ya maji kwa njia ya chupa.

Katika mhadhara huo, msisitizo utakuwa katika vyombo vinavyohusika na utoji wa maji ya bomba kuboresha huduma zao na ubora wa maji ya chupa, ili kuwalinda Watanzania na madhara wanayopata kutokana na kutumia maji ya chupa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Elifas Bisanda alisema kuwa mhadhara huo utatolewa saa 8:30 mchana.Prof. Mbwete atazungumzia utafiti alioufanya kuhusu teknolojia ya kuchuja maji kwa kutumia mchanga ili kupata maji safi hasa katika maeneo ya vijijini na pembezoni mwa nchi.

"Ili kuhakikisha kuwa huyu mwanataaluma ambaye ni profesa kamili anaendelea kujionoa ubongo, anatakiwa kutoa mada au hotuba hizo kila baada ya miaka mitatu. Profesa anapewa nafasi kwenda likizo ya kunoa ubongo (sabbtical leave) au likizo fupi ili afanya maandalizi na kuchapisha hotuba yake," alisema.

Alisema utamaduni huo umejengwa katika vyuo vikuu kwa wanataaluma waliofikia cheo cha profesa ambao hutakiwa kutoa mihadhara ya kiprofesa 'professorial Inaugural Lecture' inayotakiwa kutolewa katika kipindi cha miaka mitatu tangu mhuska alipotangazwa kuwa profesa kamili.

Alisema OUT inatambua umuhimu wa wanataaluma kuendelea kufanya tafiti mbalimbali na kutoa matokea hadharani.Alisema pendekezo la mtoa mada ni kwa serikali ya Tanzania na sekta ya maji kuongeza uwekezaji katika sekta ya maji wakati huo huo kukiwa na fursa nzuri ya kibiashara

1 comment: