28 December 2010

Mbivu, mbichi za Dowans wiki ijayo

*Mwanasheria mkuu amaliza kupitia hukumu
*Waziri Ngeleja ajiandaa kutoa taarifa rasmi


John Daniel na Grace Michael
SIKU moja baada ya wananchi kuja juu na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kumtaja kwanza mmiliki wa Kampuni ya Dowans kabla ya kulipwa mabilioni ya walipa kodi, serikali imeahidi kutoa taarifa rasmi juu ya
sakata hilo wiki ijayo.

Kutolewa kwa taarifa hiyo wiki ijayo inatokana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Fredereck Werema, kukamilisha kupitia jalada la maamuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya kibiashara (ICC) na kuwasilisha mapendekezo yake Wizara ya Nishati na Madini.

Nimefanya kazi hiyo na nimeimaliza. Nimetoa maamuzi kuhusiana na kilichokuwemo humo ndani na nimewasilisha kwa Waziri wa Nishati na Madini, hivyo nendeni huko atawaeleza,รข€ Jaji Werema aliwaeleza waandishi wa habari, Ikulu baada ya kuapishwa kwa Jaji Mkuu Mohamed Othamn Chande.

Alipohojiwa zaidi kuhusu alichoshauri na 'kiu' ya wananchi kuhusu wamiliki wa Dowans, Jaji Werema alisema: Jamani msiwe mnaongea kama bata ebu itafuteni hiyo hukumu inaonesha kila kitu na wamiliki wa kampuni hiyo mtawajua humo hivyo katafuteni hukumu.

Akizungumza na Majira kwa njia ya simu, Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja alikiri ofisi yake kupokea jalada la ushauri kutoka kwa Jaji Werema kuhusu Dowans.

"Ninachoweza kukuhakikishia ni kuwa nimetaarifiwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameleta taarifa hiyo baada ya kupitia jalada husika.
"Ninawaahidi Watanzania kuwa serikali itatoa taarifa kamili juu ya suala hilo wiki ijayo, siwezi kusema zaidi kwa sasa kwa kuwa hata mimi sijapitia hiyo taarifa," alisema Bw. Ngeleja.

Alipoulizwa kuhusu uhalali wa madai ya sh. bilioni 185 za Dowans, Bw. Ngeleja alisema hawezi kuzungumza suala hilo kwa sasa kwa kuwa hajapitia jalada husika ili kujiridhisha.

"Nakuomba vuta tu subira, serikali itatoa taarifa kamili juu ya suala hilo wiki ijayo kama nilivyokwambia. Kila kitu kitajulikana wazi hakuna kitu cha kuficha, nipe tu muda," alisisitiza Bw. Ngeleja.Awali vyanzo vya vya Majira ndani ya Serikali na nje vilieleza kuwa malipo halisi ya Dowans si sh. bilioni 185 kama ilivyotangazwa awali na kwamba kiwango hicho kilipandishwa na wapambe wa kampuni hiyo kinyume na hali halisi.

Habari hizo zilieleza kuwa Jaji Werema ametoa ushauri mzito kwa serikali, ikiwemo kuwa makini zaidi katika mikataba na uvunjaji wake ili kuepusha nchi kuingia gharama kubwa kulipa fidia ya mabilioni ya fedha bila sababu.

Hata hivyo, Jaji Werema hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani kwa maelezo kuwa yeye si msemaji bali mwanasheria na maadili yake hayamruhusu kusema lolote kwa kuwa hakutumwa kufanya hivyo.

Habari kutoka vyanzo vyetu ndani ya Serikali vilieleza kuwa malipo halisi ya Dowans kwa mujibu wa hukumu ya mahakama hiyo ni dola milioni 64 karibu sawa na sh. bilioni 90 za Tanzania.

"Katika hali inayotia mashaka taarifa ya ICC inasema madai ya malipo ya bilioni 185 kwa Dowans ni feki na yamepikwa na wapiga debe wa kampuni hiyo nje na ndani ya nchi kwa malengo wanayojua wao.

Malipo halisi yanatajwa kwa ni tuzo ya dola milioni 64.2, lakini wanasheria wa masuala ya usuluhishi wanasema hata hiyo tuzo ya milioni 64.2 si mwisho, bado TANESCO wanaweza kuirekebisha kupitia Judiciary Review katika Mahakama Kuu ya Tanzania," alisema Chanzo chetu.
Chanzo hicho kilisema wakati shauri hilo likiendelea katika mahakama hiyo jina la mbunge mmoja lilitajwa kama mwakilishi wa kampuni hiyo hapa nchini.

"Majina ya wamiliki wa Dowans haikutajwa, lakini aliyekuwa anaiwakilisha kampuni kortini alimtaja mbunge huyo kuwa ndiye mwakilishi wa Dowand nchini, ni jambo la kawaida katika biashara," kilisema chanzo chetu.Chanzo hicho kilidai kuwa tatizo kubwa iliyosababisha Tanzania kushindwa katika ushauri huo ni maandalizi hafifu ya mwanasheria aliyewakilisha TANESCO.

Ilielezwa kuwa mwanasheria huyo alienda katika shauri hilo akiwa na hoja moja tu ya 'mkataba wa kampuni ya Richmond iliyouzwa kwa Dowans usivyo halali' na baada ya kushindwa na upande wa utetezi hakuwa na njia nyingine.

"Katika mazingira haya ya sasa ni ngumu sana Tanzania kukwepa kulipa japo kiasi halisi kitakacholipwa si bilioni 185 kama ilivyotangzwa," kilisema chanzo chetu.

12 comments:

  1. Hebu tumuulize Asange atutengulie kitendawili hiki! cha nani haswa ni dowans, richmond, kagoda etc!

    ReplyDelete
  2. Mh.Rais JK,ninaomba sana utumie busara ulionayo katika kutatua tatizo la Dowans.Viginevyo utazidisha machungu makubwa sana kwa watanzania ambao wengi wao ni maskini wa kupindukia.

    ReplyDelete
  3. Ogopa sana mtu anayetoa ahadi ya kutoa taarifa wiki ijayo wakati hata hajalipitia jalada la kesi na mapendekezo yake! Maana yake nini: Hatajishughulisha kusoma maamuzi hayo mwenyewe. Anatarajia watimushi wake wampe briefings! Ndio kisa cha kusaini mikataba hewa!

    ReplyDelete
  4. HILI NI DILI LA MTUKUFU RAIS DK. KIKWETE,DR IDRISSA, MH LOWASSA, MHE ROSTAM NA WAKILI WAO MHE. MKONO, MBUNGE KULE MKOANI MARA. NI JAMBO LA KUSTAAJABISHA LAKINI LA KWELI.BALOZI KAZAURA ANAJUA HUO UKWELI NA VIONGOZI WOTE WANAJUA.

    ReplyDelete
  5. ufumbuzi wa matatizo kama haya ni kua na sheria kama za china,kwamba yeyote kwa njia moja au nyingine atakayehusika na kuibia serikali au kuingia mikataba hewa ya richmond,dowans nk anyongwe hata akiwa madarakani tutakomesha kila kitu

    ReplyDelete
  6. Jina tu haitoshi kwani wanaweza kuweka jina, mtu mwingine na jalida kwenda kwa Ngereja ni sawa na simba mtoto wa nyati amupleke kwa mamaye. Huyo ni waziri asiye na sifa kuwa waziri sijui walikutana wapi na kikwete mpaka kumchagua. Anajulikana tangu chuo muoga wa kujificha chini ya uvungu.

    ReplyDelete
  7. Ingawa mimi si rais, nawatajieni wenye kampuni la Dowans.
    1 Jakaya Kikwete
    2 Edward Lowassa
    3 Rostam Aziz
    4 Nimrod Mkono
    5 Andrew Chenge
    6 Nazir Karamagi
    Waliobaki malizieni wenyewe. Je mna swali jingine au wasi wasi juu ya kuwatajia wezi wenu wakuu wanaoitwa waheshimiwa?
    Kazi kwenu mchawi eshafichuliwa.

    ReplyDelete
  8. Huyo mbunge aliyeiwakilisha Tanesco kama mwanasheria ni NIMROD MKONO!!!!!!

    ReplyDelete
  9. Joseph Kaaya
    Washington DC 4545
    USA
    Huyo jaji mkuu, mwanasheria wa serikali na tanesco ni ni sahani za kikwete na vibaraka wake so nao hukumu yao yaja. Namshangaa ngeleja kusema eti ameipitia taarifa ya werema na atatoa uamuzi soon. Hao wote ni wapumbavu tena sana wasije wakaona kama wanaongoza kijiji kwani ni aibu sana kwa nchi kuwa na wasemaji wasio na ufahamu.
    Hii ni mpya eti deni lilikuwa $ 64.2, Imekuwaje ikafika $ 185? Na ni nani alie ibariki hii statement ya $ 185? Na je huyo kikwete na tanesco walikuwa wapi wakati wa siku ya hukumu hadi watanzania wapate taarifa tofauti juu ya hukumu? Na je huyo mwanasheria wa tanesco ilikuwaje aende mahakamani na ushahidi juu ya richmond hali kesi ni ya dowans?
    Ilielezwa kuwa mwanasheria huyo alienda katika shauri hilo akiwa na hoja moja tu ya 'mkataba wa kampuni ya Richmond iliyouzwa kwa Dowans usivyo halali' na baada ya kushindwa na upande wa utetezi hakuwa na njia nyingine.
    Hii sio sawa hata kidogo inatakiwa watu wawajibishwe na sio kuchekeana. Wananchi wamechoka na inakuja wakati nchi itatoa harufu yake. Si wanajifanya nchi ya amani wakati wananchi wanakufa kwa njaa,

    ReplyDelete
  10. Anonymous said...
    Karibu asilimia 70 ya maoni mbalix2 yatolewamo hapa Majira huwa yanamalizikia kumlaumu JK in person na kama kwamba yeye tulimpa pesa atunulie nchi iliyo nzuri na badala yake katununulia nchi iitwayo Tanzania.

    Munajisumbua tu. Nani anaeiendesha TZ, Tanesco, Judiciary, n.k? Tanzania imesomesha wasomi wangapi hadi sasa. Pia angalia sehemu zote NYETI zinaongozwa na cc waTz (ambao wengi wetu tumeenda shule) lakini bado tunalalamika kipuuzi.

    Ukweli ni mfumo(system) mulioukubali na kuupigia debe miaka karibu 50 sasa ndio wa kulaumiwa. Na ukifanya hivi, wewe na mimi ndio wa kulaumiwa kwani kwa sababu ya roho zetu ni mbovu na ubinafsi, bado hatutaki kwenda na wakati. Na ikiwa hamtobadilika vichwa vyenu,basi tutaendelea na sakata hili kwa nusu karne ijayo.

    Hata wewe mchangiaji ikiwa utapewa uongozi katika mfumo huu nini kipya utakileta. Usijidanganye, muda utapita na lawama zitakuwepo pale x2.

    Kutafuta mchawi, yaani JK, udini, ukabila ni kupoteza wakati. Mgonjwa hamfichi dakitari vyenginevo, hatopata matibabu sahihi.

    Tunatakiwa tuwe na SYSTEM OVERHAUL baada ya kujua nini tunataka.

    Mwisho, nimesema kabla na nitazidi kuwakumbusha, ICC na waTZ c wapumbavu kukubali kuheshimu uamuzi wa mahkama. Ikiwa kampuni imesajiliwa kihalali na wamiliki hawakujulikana tokea awali, ni Mrajisi wa Makampuni na Wizara husika ndio responsible sio JK, uisilamu, ukabila na lawama za kijinga!.

    ReplyDelete
  11. Haya yote yana mwisho mbaya maana vita ya wenyewe kwa wenyewe huwezi kuiepuka kwa staili ya viongozi kuendekeza ufisadi.
    Rais anayajua yote haya ila kwani asichukue hatua?

    ReplyDelete
  12. Ngugu yangu unaishi wapi wewe hapa Tz. Rais pekee hana mamlaka ya kutengua sheria bila ya kushirikiana na mihimili mingine miwili ya Bunge na Mahakama.

    Kazi kubwa ya Rais wa nchi yeyeote ni Kuamua (DECISION MAKING kwa yale aliyoandaliwa. Iwapo Bunge, Mahakama na viongozi waandamizi (aliowateua na aliowarithi)walioko madarakani hawatofanya ipasavyo, vipi Rais ataweza kufanya kazi vizuri.

    Pia hata wewe, kwanini shutuma hizi hizi hamuwapelekei wabunge wenu amabao mmewapa kura zenu? Isitoshe, iwapo hujaridhika, tafuta msaaada na fungua kesi mahakamani na Majaji wataamua. Kulalamika na kutafuta mchawi ni kutafuta scapegoat na ikibaki hivo hakuna kitakachokuwa!

    ReplyDelete