28 December 2010

CUF kuandamana licha ya polisi kuzuia

Rabia Bakari na Lead Kassopa

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeazimia kufanya maandamano leo ya kutoa rasimu ya mapendekezo ya katiba serikalini, licha ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuyazuia.Akizungumza na gazeti hili, Naibu Katibu Mkuu Bara, Bw. Julius Mtatiro alisema
kuwa zuio la polisi juu ya maandamano hayo halina msingi kisheria na limechelewa kuwafikia, wakati wameshapata hasara ya kutoa matangazo kwa wananchi na wadau mbalimbali.

Maandamano hayo, yanahusisha kupeleka rasimu ya mabadiliko ya katiba kwa Waziri wa Sheria na Katiba na kufuatiwa na mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

"Mnamo Desemba 21, mwaka huu, tulimwandikia barua Waziri wa Sheria na Katiba kumtaarifu kuwa mnamo Desemba 28, mwaka huu, tutaiwasilisha rasimu ya mapendekezo ya katiba kwake. Pia tuliwaandikia na polisi kuwajulisha kuhusu maandamano wakati wa kupeleka rasimu hiyo.

"Na baada ya hapo tukamwandikia barua Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuhusu kutumia uwanja wa Mnazi Mmoja kwa ajili ya mkutano wa hadhara baada ya kuwasilisha rasimu yetu ya mapendekezo. Lakini cha ajabu polisi hawakutujibu siku zote hizo, hadi leo (jana), ambapo Kamanda Kova alituita na kutupa majibu ya mdomo eti maandamano yetu yamezuiwa," alisema Bw. Mtatizo.

Kwa mujibu wa Bw. Mtatiro, Kamanda Kova amezuia maandamano hayo, kwa madai kuwa barua ya chama hicho kwenda kwa waziri, haikuonesha kama kutakuwa na maandamano.

"Waziri sio kazi yake kujua maandamano, isipokuwa kwenye barua tumemjulisha kuwa, tutakapofika ofisini, tutateua watu wachache kwa ajili ya kwenda kumkabidhi rasimu ya mapendekezo ya katiba, na kisha tutarudi na maandamano yetu hadi Mnazi Mmoja tutakapofanya mkutano wa hadhara.

Cha ajabu polisi, hawakutujibu mapema, na wameacha tumewatangazia wananchi na imetugharimu zaidi ya sh. milioni 10 kutangaza, halafu ndio wanazuia maandamano kwa sababu zisizo na msingi," aliongeza.

Alidai kuwa pamoja na maneno hayo ya Kamanda Kova, maandamano yao yapo palepale, na wanataka wananchi saa mbili kamili kukutana Buruguni Shell kwa ajili ya kuanza maandamano kuelekea kwa Waziri wa Sheria na Katiba, Bi. Celina Kombani.

Bw. Mtatiro aliongeza kuwa ni kawaida kwa Jeshi la Polisi nchini kuwaonea raia na kuwandamiza katika haki zao za msingi, na ndio maana Bw. Kova amekuwa na majibu rahisi ya kuzuia maandamano hayo katika mambo ya msingi kama kudai mabadiliko ya katiba.

Hivi karibuni, katika mkutano uliofanyika viwanja vya Temeke jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa chama hicho, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad alisema kuwa chama hicho ndo cha kwanza kuanzisha vuguvugu la katiba mpya, na kuwa ilisababisha viongozi wake kadhaa kufungwa jela kutokana na harakati za kudai katiba mpya.

Aidha alisema kwa kusisitiza ukweli huo, chama hicho kilikuwa kimeandaa rasimu ya mapendekezo ya katiba tangu muda mrefu na kumtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Siasa, Bw. Mbaralah Maharagande kumpatia rasimu hiyo Bw. Mtatiro ili aweze kuipeleka kwa Bi. Kombani.

Siku chache baada ya agizo hilo, Bw. Mtatiro alitangaza maandamano ya kupeleka rasimu hiyo ya katiba kwa Waziri Kombani, na kwa mujibu wa chama hicho, wananchi mbalimbali, pamoja na wapenzi wa chama hicho watajitokeza katika maandamano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Bw. Kova alisema chama hicho kiliandika barua hizo mbili tofauti kuomba maandamano hayo, hivyo wakaona hayatakuwa na tija.

7 comments:

  1. Kaeni chini mtulie sio parapapa, angalieni CHADEMA wanavyonyatia kama paka na panya. Hivi nyinyi CUF kila maandamano yenu hayafanikiwi ni kwa sababu gani? Kaeni mjipange sio kukurupuka tu. Muwe na sababu sio kulundika hutuba yote ya siku nzima ya LIPUMBA na kupeleka kuomba kibali cha maandamano.

    ReplyDelete
  2. Tatizo la CUF ni hili, wanataka waonekane wao ndio wa kwanza kudai katiba mpya! Hopeless kabisa!
    Subirini chama kikuu cha upinzani kipeleke hoja bungeni. Kama nyie ni wapenda demokrasia tutawaona mkiunga mkono hoja ya CHADEMA. Msitudanganye kwa maandamano yenu ambayo huishia kutoa roho za watanzania wenzetu.

    ReplyDelete
  3. Mimi ni yule yule mpenda mageuzi Hafidh -kutoka visiwa vya Zanzibar.Napenda kuwajibu ndugu zangu walionitangulia kua wote wanaona kua wanarukia na waonekane kua ndio wao waliolete hoja kudai katiba mpya!! lakini la pili mchangiaji wa kwanza anasema CUF kwa nini maandamano yao hayafanikiwi?!

    Mimi napenda nikutoe hofu ndugu zangu kwa CUF.Kwanza napenda mujue kua CUF ni chama cha mwanzo kudai katiba mpya na ushahidi huo ni wakati wachaguzi zote zilizofanyika kabla ya huu ulopita 2010,CUF ilikua inalilia kuundwa kwa katiba mpya mara nyingi tu na hata kabla ya chadema kupata nguvu kwa upande wa Bara, ushahidi wa hilo kama mnafatilia wakati alipoteuliwa Jussa kuingia bungeni hatuba yake ya mwanzo ya kuchangia alilisema hili la kuwa na katiba mpya kwa Tanzania, wakati huo hata chadema hawajawa na wabunge wengi kabla hata ya uchaguzi.sasa jee ni nani aliyeleta hoja ya mabadiliko ya katiba?!

    kuhusu suala la maandamano ya CUF kufanikiwa kwanza napenda mujue kua siku zote watawala hawapendi kushinikizwa kwa maandamano maana dunia itakua inajua hilo na ndio mana CUF walipoandamana nchi nzima 21 Jan 2001 watu walikufa na wengine vilema, suala linaulizwa jee walifanikiwa?

    Jibu ndio walifanikiwa maana mabadiliko yote munayoyaona kwa CCM kukubali kukaa meza moja na Cuf ni matunda ya maandamano hayo,kiukweli CCM wanaijua Cuf vizuri maana ikiamua kua tutafanya manake tutafanya - NO ONE CAN STOP sio Chadema munatishiwa nyau mnakaa kimya ni mikutano mingapi mikoani munakatazwa bila ya sababu za msingi na ni haki yenu lakini kwa woga wenu mnakaa mnapiga kelele tu.!!

    Jengeni hoja ndugu zangu na sio kuropokwa tuu .

    moja ya slogan ya CUF ni hii WOGA NI ADUI WA HAKI.

    ReplyDelete
  4. Mh.Mwanasheria mkuu,jaribu kutumia busara kama mwanasheria aliesomea sheria.ubishi unaouleta umeupata wapi?wanasheria waliosoma zaidi wanataka katiba ibadilishwe wewe unapinga kwa utashi wako mwenyewe je?umma ukueleweje?
    Ninaomba uwache ubishi wa bush lowyer.suala hilo liache liende bungeni,maamuzi yatatolewa na wabunge na wewe ukiwemo ndani ya bunge hilo la jamhuri ya muungano wa Tanzania.Asante kwa kunielewa

    ReplyDelete
  5. CUF iungeni mkono CHADEMA kudai katiba kwani CDM ndio wamechukua uongozi wa upinzani bungeni. Acheni maandamano hayo yanayoumiza watu. Acheni kujifanya nyie ndio chama cha upinzani. Wapeni CDM mawazo yenu watayapeleka mahali stahiki.
    Mlitisikitisha sana mlipoacha kumpa mgombea uspika anayetoka CDM, mkaiunga mkono CCM. sasa nyie ni wapinzani gani? Tuonyesheni uzalendo wenu, ukomavu na uzoefu wenu wa upinzani
    Kila mnapoiunga CCM mkono kwenye hoja bungeni, mnaonyesha unafiki. Jirudini na ikibidi muachie huo umakamu na uwaziri mliopewa.

    ReplyDelete
  6. Hawa CUF waache unafki, ushamba na ubinafsi. Pupa zao ndio maana wanapigwa na kuanza kulalamika. Kama ni wastaarabu kweli kwa nini wasiungane na CHADEMA kutumia njia ya kisomi. Ikishindikana ndio maandamano. Tunawashangaa hili suala la katiba sijui CUF ndio wameanza sasa wakaishia wapi? Wasituletee hizo hotuba za LIPUMBA.

    ReplyDelete
  7. Mimi ni yule yule Hafidh mpenda Mageuzi wa kweli kutoka Visiwa vya amani Zanzibar .

    Ndugu zangu Wanachadema napenda niwape somo la ukweli sasa maana naona siasa hamuijui.

    Hoja zilizojengwa hapo juu kua CUF si chama cha upinzani na Chadema ndio chama kikuu cha upinzani !! halafu eti kupeleka hoja bungeni ndio njia sahihi na maandamano sio sahihi !!halafu eti tuachie uongozi katika serekeli ya pamoja Zanzibar na kufanya hivyo ndio sio unafiki!! hoja zote hizi ndugu zangu ni kutokua na uelewa mpana au kuwa na kikiomo cha uelewa wako (umaskini wa akili na kufiri mbele).

    Najibu hoja zenu sasa na kujenga hoja zangu kama kuna mtu anaweza ku challenge aingie uanjani hoja za msingi ili tufaidike sote.
    1) Kusema Chadema ndio chama kikuu cha upinzani Tanzania !! hili sio kweli kwa sababu hizi :- a)Tanzania ni muungano wa nchi 2 (Tanganyika na Zanzibar) ikiwa ni sawa manayake ni kua Chadema ina nguvu Tanzania Bara na Cuf ina nguvu Tanzania visiwani.b)Historia ya siasa za vyama vingi tangu 1995 Cuf ndio chama pekee kilichoweza kupeleka wabunge wengi (katika kila uchaguzi ukiachia huu ulopita) Bungeni na sio chadema.c)Moja ya mikakati ya chama chochote cha siasa Duniani ni kuingia madarakani ndio mana ukawaona leo kina Raila Odinga na Shangirai wapo madarakani kutoka vyama tofauti.na mwisho CUF ni chama pekee kilichoipa challenge kubwa CCM tangu mfumo wa vyama vingi kuanza na sio chadema ! kwa hoja hizi bado CUF ni chama cha kikubwa cha upinzani (ukibisha jenga hoja)

    Maandamano ni njia sahihi kuliko hoja bianafsi Bungeni? Ndio - mana mfumo wa Bunge letu bado haupo uwazi zaidi katika kujadili mustakbal wa Taifa letu , tulikua na kiongozi amabaye tulimuona jasiri kwa Bunge lilopita - (Mzee Sita)lakni tuangalie jee hoja zilizopelekwa bungeni zilikidhi haja za wananchi?? hapana maana hoja Richmond mwisho wake kwa Serekali kuwajibika ilizimwa na kufungwa mjadala !! sasa jee hamuoni kwa bunge la sasa linaloendeshwa na mama litaweza kuwa wazi zaidi ?! jawabu mnayo nyie.So maandamano ni njia pekee ya kudai haki na kutuma msg ndani na nje kwa mda wa haraka sana. hii inatumika duniani kote mapka kule tunakoamini wametuzidi kwa kila jambo.

    Mwisho Cuf kujitoa katika Serekali ya umoja wa kitaifa si sahihi kwa sababu mtazamo wa Cuf ni kujenga njia bora na uwazi zaidi katika uchaguzi na maandeleo kwa ujumla sasa ukiwacha ccm wafanye peke yao watakuliza badae na utajuta,lkn ukiwepo utaweza kuona na kusema NO hapo si sahihi kufanya hivi.

    Naomba tujenge hoja ili wanaosoma wafaidike na mawazo yetu na sio jazba .

    Thanks

    ReplyDelete