20 December 2010

Mashabiki wa TP Mazembe wazua vurugu

LUBUMBASHI, DRC

GHASIA zimezuka katika mji wa Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), baada ya timu ya TP Mazembe kushindwa katika fainali ya kuwania Kombe la Dunia kwa klabu mjini, Abu Dhabi, usiku wa kuamkia jana
.

TP Mazembe ilikuwa klabu ya kwanza kutoka barani Afrika kuwahi kufuzu fainali za mashindano hayo, ilifungwa mabao 3-0 na Inter Milan ya Italia.

Habari zinasema kuwa, mashabiki ambao walikuwa na matumaini makubwa kwamba, TP Mazembe ingeshinda mchezo huo, waliingia katika barabara za mji wa Lubumbashi na kuvamia biashara zinazomilikiwa na kampuni ya China.Inaaminika kuwa, mashabiki hao walidhani kuwa, refa aliyesimamia mchuano huo raia wa Japan, alikuwa Mchina, na walikuwa wamekasirishwa na hatua alizochukuwa mwamuzi huyo dhidi ya TP Mazembe ,wakati wa mechi hiyo.

Ilielezwa kuwa, wakati wa ghasia hizo, mali ziliporwa, lakini polisi waliweza kuwatawanya mashabiki hao kwa kufyatua risasi hewani.Kampuni nyingnei ya China zinaendesha biashara katika mji wa Lubumbashi ambao ni kitovu cha uchimbaji madini ya shaba nyekundu.

No comments:

Post a Comment