17 December 2010

Makanisa yataka katiba mpya

  •Yasema wakati wa NEC kuvunjwa umefika
•Yataja dosari zilizojitokeza Uchaguzi Mkuu
•Yaonya wanasiasa kuchanganya ahadi na haki
•Yakosoa CCM kuingiza Kadhi kwenye Ilani


Na John Daniel
JUMUIYA ya Kikristo Tanzania (CCT) imeitaka Serikali kuhakikisha inakamilisha haraka utaratibu wa kuandikwa Katiba mpya ili kukidhi mazingira yaliyopo ndani ya nchi.Akisoma tamko la Jumuiya hiyo Dar es Salaam jana, kuhusu  kasoro zilizojitokeza
wakati wa Uchaguzi Mkuu, Mwenyekiti wa CCT, Askofu Peter Kitula, alisema wamejiridhisha kuwa kulikuwa upungufu mkubwa unaohitaji marekebisha ya haraka kwa maslahi ya Taifa.
“Ni nia yetu ya dhati kuona tunakuwa na Katiba mpya haraka iwezekanavyo itakayotungwa baada ya tafiti za kina kufanywa kwa umakini....” Kwa kusikiliza na kuzingatia sauti na utashi wa watu na uzingativu wa kutosha wa dalili za nyakati na mazingira ya nchi pamoja na kuheshimu maono na falsafa za waasisi wa Taifa letu,”alisema Askofu Kitula.
Alitaja kasoro hizo kuwa ni pamoja na udini, matusi, kejeli, vitisho na rushwa kwamba ni mambo ya hatari yalijitokeza katika mchakato huo.
“Jumuiya ya Kikristo ilipeleka waangalizi wa uchaguzi 28 kutoka ndani na nje ya nchi, tunachukua fursa hii kusema tumesikitishwa na mambo yalijitokeza kama vile rushwa ya uchaguzi iliyokithiri hata baada ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi kupitishwa.
Matamshi na malalamiko yaliyotolewa na wanasiasa kuhusu udini bila kuthibitisha au kuwachukulia hatua za kisheria waliotumia udini kuvuruga amani ya nchi au kuingilia kwa makusudi ya kuchafua mchakato wa uchaguzi ama kutumia udini kama farasi au njia ya kuwaingiza madarakani ama dini kutumika kisiasa kwa nia ya kuwalaumu, kuwachafua na kuwadhalilisha wanadini walio safi,”alisema Askofu Kitula.
Alisema matumizi mabaya ya lugha za kejeli baina ya wanasiasa, vyama, viongozi na dini baina ya wafuasi, matusi ya wazi na maneno ya udhalilishaji pamoja na vitisho kwa baadhi ya maeneo kuwa dosari zinazopaswa kufanyia kazi haraka.
Alisema mchakato wa uchaguzi wa demokrasia ni njia sahihi ya kutoa fursa kwa Taifa kupata viongozi bora na waadilifu bila vurugu, uvunjifu wa amani wala kudhalilishana.
Alisema licha ya mapungufu hayo, CCT inawapongeza Watanzania kwa kuonesha m w a m k o n a m a b a d i l i k o , kutambua haki zao na kutokubali kuyumbishwa na wanasiasa.
“ Tu n a w a p o n g e z a s a n a watanzania kwa mwamko wao kisiasa, kuzijua haki zao, kujitambua haki zao na kuonesha kwa vitendo dalili za wazi kutopenda kuyumbishwa na misukumo ya kisiasa isiyo endelevu,”alisema Askofu huyo.
Alisema CCT inawapongeza Watanzania kwa utulivu na uungwana wa hali ya juu katika mazingira ambayo yangevuruga nchi.
“Tunaamini kuwa wakati umefika wa kuwa na Tume huru na mpya ya uchaguzi itayokuwa imeundwa kwa kuvishirikisha vyama vyote vya siasa, wasomi, watafiti na wadau mbalimbali. Tunaamini elimu ya kutosha kwa wapiga kura na wananchi kwa ujumla pamoja na taratibu huru na wazi zitakazowakilisha ari za vyama, makundi yote ya kijamii zitakazolenga kuboresha mahusiano mema ni njia pekee ya kuondokana na kero na machungu ambayo tumeyaona katika uchaguzi mwaka 2010,”alisisitiza Askofu Kitula.
Aliendelea; “vinginevyo tumeanza kuhofia kuwa chaguzi zinazopaswa kuwa huru, haki na amani sasa zinatishiwa kuwa za vurugu,uvunjifu wa amani, vitisho na mabezano, matusi na kejeli zisizotujenga kama nchi.
“Vyama viache, viepuke na vikwepe ushawishi wowote wa kutumia njia iwayo yote ya kampeni zenye ahadi za uwongo na zisizotekelezeka”alisema na kuongeza vyama vijifunze kutofautisha ahadi na haki, mfano upatikanaji wa maji, elimu, afya, na utabibu,miundo mbinu na haja nyingine ya msingi ni haki na havihitaji kuwa sehemu za ahadi kwa wanaoomba kura,”alisema.
Alisema CCT inataka vyama vya siasa kutambua kuwa uboreshaji wa njia za uchumi kwa wananchi ni wajibu wa kiongozi yeyote na siyo hisani. Alisema Jumuiya hiyo inavitaka vyama vya siasa kuwaonesha wananchi njia za kupatikana kwa mahitaji ya haki na ya msingi na kwamba watahukumiwa kwa uwajibikaji wao na siyo takrima au rushwa zinazotolewa wakati wa kampeni.
Udini
Alisema tatizo hilo lilianza mwaka 1986 na hakuna kiongozi w a S e r i k a l i a l i y e j i t o k e z a kulikemea badala yake Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilizidi kufanya makosa kwa kuingiza suala hilo katika Ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2005.
Alisema kwa mujibu wa Katiba ni kosa kuhusisha dini katika siasa na kwamba waasisi wa Taifa letu waliona hilo na kuweka bayana mahusiano kati ya dini na Katiba.
“Kazi ya kutangaza dini,kufanya ibada na kueneza dini itakuwa ni huru na jambo la hiari ya mtu binafsi, na shughuli na uendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi,”alisema Askofu Kitula akinukuu Sheria ya mabadiliko ya kumi na nne katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania namba moja ya mwaka 2005.
“Kuanzia miaka 1986 kulianza kujitokeza mihadhara ya kidini na kidhehebu katika jamii lakini jambo hili halikukemewa wala kuchukuliwa hatua za kisheria.
Ilani ya uchaguzi ya CCM 2005 ilitamka bayana kuwa suala la Mahakama ya Kadhi litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi, ikumbukwe kuwa mahakama ya kadhi ni jambo la kidini na kiibada katika dini ya kisilamu, jambo hili ni kinyume cha Katiba ya nchi na sheria ya vyama vya siasa hakuna aliyeona hatari yake na kwamba litakuwa chanzo cha udini ndani ya siasa za Tanzania, “alisema.
“Tafsiri yetu ni kwamba chama chochote cha siasa hakitakubaliwa usajili wa muda endapo kwa kufuatana na Katiba yake au sera ya chama hicho kinalenga kutetea au kuendeleza maslahi ya imani au kikundi chochote cha kidini.
pamoja na kwamba CCM iliondoa kifungu hiki katika Ilani ya 2010 bado mbegu ya udini haikuondoka kwani baadhi ya viongozi wa kisiasa na dini bado wanaendelea kulizungumzia,”alisema.
Kejeli na matusi
Lugha za kejeli na matusi vilitumika bila aibu na kwa makusudi kabisa, mbaya zaidi ni pale ambapo mgombea wa ubunge wa CHADEMA alipomtukana mgombea urais wa CCM, jambo hili lilishtua na kusikitisha Taifa zima,”alisema Askofu Kitule.
Alisema CCT inalaani vitisho vilivyotolewa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na kwamba vilichangia wapiga kura wengi kushindwa kujitokeza kwa hofu ya kushughulikiwa na chombo hicho kikubwa zaidi cha dola.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu watanzania watatu waliuawa kikatili wakati wa kampeni huko Musoma, Maswa na Kibakwe, jambo la kusikitisha hadi leo hakuna kiongozi wa chama chochote anayesema wala kemeo,”alisema.
Alisema licha ya uchaguzi na kazi ya kuhesabu kura kufanyika kwa amani, dosari kubwa ilijitokeza baada ya vyombo vya dola kuingilia mchakato huo wakati wa kusafirisha masanduku ta kura huku baadhi ya mawakala wakifichwa.
“Tunaona kuwa ni ishara ya kujenga mazingira yanayoweza kuendeleza uvunjaji wa amani, hali hii ikiachwa itakuwa donda ndugu katika nchi nzima,”alionya.
Alisema CCT inatoa wito kwa vyombo vya usalama kubaki na wajibu wa kulinda wananchi na mali zao, vyama vyote bila upendeleo wala vitisho.
“Vyombo vya ulinzi na usalama vione kuwa ulimwengu tunaoishi ni wa mabadiliko, ni wajibu wa vyombo hivyo kwenda na kulinda michakato ya mabadiliko bila kuathiri uhuru na haki ya watu kuchagua viongozi wao kidemokrasia,”alisisitiza.
Wakijibu maswali ya waandishi wa habari Makamu Mwenyekiti wa CCT Askofu Dkt. Valentino Mokiwa, alisema hakuna sababu ya Taifa kwenda kama kipofu kwa kupapasa. Alitoa wito kwa viongozi wa kisiasa kufuata Katiba na maelekezo ya kisheria na kuachana na udini ili kunusuru amani na utulivu wa nchi.
“Suala la Mahakama ya Kadhi inapaswa kuzikwa kabisa na wala lisiwepo tena midomoni mwa wanasiasa, nisingependa kodi yangu itumike kujadili mahakama ya kadhi, hakuna kitu kitakachojadiliwa Bungeni bila kodi ya mwananchi kutumika."Ningepende kodi itumike kupeleka dawa hospitali, suala hili life kabisa, libaki la kidini kama Mokiwa anavyoweza kuwa na idara yake ya maendeleo ndani ya Kanisa bila kutegemea kodi ya wananchi,”alisema.
Viongozi hawa pia waliipongeza Serikali hatua ya kuundwa kwa Serikali ya umoja kati ya CCM na Chama cha Wananchi (CUF) na kuwataka wanaopinga suala hilo kufunga midomo.
Hata hivyo viongozi hao walikosoa Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa kuwataja mawaziri na viongozi kadhaa wa Serikali ya Kenya kuhusika na mauaji ya watu baada ya uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo na kuhoji kwanini wahusika wa mauaji ya Iraki wasitajwe wala kushitakiwa? .

28 comments:

  1. BABA ASKOFU SUALA LA MAHAKAMA YA KADHI HALIFI WALA HALITAKUFA,TUTAPAMBANA HADI KIELEWEKE. UMETOA MFANO MZURI SANA KUHUSIANA NA MAHAKAMA YA KITAIFA KUHOJI MAUAJI YALIYOFANYIKA KENYA BADALA YA KUHOJI MAUAJI YANAYOFANYIKA IRAK, NA SISI TUNAHOJI VIPI NCHI ZA KENYA,UGANDA,RUANDA,BURUNDI NA NYINGINEZO ZENYE WAKIRISTO WENGI HATA KULIKO WAISLAM LAKINI ZINA MAHAKAMA YA KADHI? NINI HOFU YENU KWENYE HILI? TUNATAKA PIA NCHI IWEPO KWENYE OIC KWANI BALOZI WA VATICAN HAPA NCHINI ANAFANYA SHUGHULI GANI NA PALE VATICAN SI NCHI ILA PANA UTAWALA WA KIDINI NDANI YA NCHI YA ITALIA. JAMANI TULIWAAMBIA MAPEMA KWELI KATIBA MPYA INAHITAJIKA KWENYE NCHI YETU LAKINI TUELIMISHANE NA TUWE TAYARI KUMEZA MACHUNGU MENGINE AMBAYO HATUYAPENDI KAMA HAYO,SISI WAISLAM TUMETAKA SIKU NYINGI KATIBA IANDIKWE UPYA ILI NASI MAMBO YETU YA MSINGI YAWEPO KATIKA KATIBA MPYA LIKIWEMO MAHAKAMA YA KADHI,SASA TAYARI MMEANZA KUCHAGUA YALE YANAYOKIDHI MAHITAJI YENU,MSIYOYAPENDA MNAANZA KUYATENGA,HIYO SI KATIBA JAMANI. BAKWATA TUNAKUOMBA SHEIKH MKUU TUPISHE VIJANA TUPAMBANE NA HAYA.TUNALISIHI KANISA LISIANZE KUCHAGUA YAPI YAWEPO NA YAPI YASIWEPO

    ReplyDelete
  2. Viongozi wa dini mnaposhabikia siasa lazima mtakutana na mengi,hivyo wakuu wa kanisa na misikiti chungeni kauli zenu sana,kwani wanasiasa wa kiafrika ni wezi,wabadhirifu na wanakwenda kwenye siasa kuganga njaa na sio kuwatumikia wananchi. Askofu kuhusu mauaji ya wakenya waliouwawa katika uchaguzi hapo umechemsha,mimi naishi Nairobi hali ilikuwa mbaya sana,sasa waliochochea hali hii ni wanasiasa ambao wanatakiwa kwenye mahakama ya kimataifa na watapewa fursa ya kujitetea,sasa hapo kuna ubaya gani? kuhusu Irak pia pia umechemsha maana nchi hii ilikuwa haiko hivyo ila Rais Bush ndie chanzo,nilifikiri pia utasema pia kwa nini rais mstaafu Bush asifikishwe kwenye mahakama hiyo kujibu tuhuma za mauaji ya kinyama yaliyofanywa na askari wake na uharibifu wa mali na kuacha vilema wengi nchini humo,au kwa sababu Busha alitamka kamaliza URUSI sasa adui mkubwa aliyebaki ni Muislamu? wakuu wa dini siasa si kitu chema kukihusisha na kanisa au dini,siasa ni kitu hatari sana hivyo hamna budi kutahadhari sana na matamshi yenu.

    ReplyDelete
  3. JIADHARINI NA WAANDISHI,KAZI YAO NI KUANDIKA,ILI KUPATA RIZIKI YAO,HIVYO TUSIWE WATU WA HARAKA TU KUTOA MAONI YA YALE YALIYOANDIKWA BILA KUFANYA UTAFITI WA KINA.TAASISI YEYOTE INAPOTOA TAMKO HUWA WANASEMA WAZI KWENYE VYOMBO VYA HABARI KAMA RADIO NA TV,WAANDISHI WA HABARI NDIO WALIOSABABISHA MACHAFUKO MENGI KATIKA NCHI NYINGI DUNIANI,KAMA KENYA,BURUNDI NA RWANDA.HATA KAMA WATANDIKA TUTOE MAONI BAADA YA KUDHIBITISHA KWELI WALICHOANDIKA NI SAWA,NA HAPA TUZUNGUMZIE UMUHIMU WA KILA JAMBO KWA WANANCHI.KWA MAANA KATIBA ITAKUWA YA WANANCHI WOTE TUZUNGUMZIE KATIBA AMBAYO ITATUWEZESHA TUISHI KWA AMANI NAUTULIVU,SIYO KWAMBA HUYU AMEPEWA HIKI NA MIMI NIPEWE,WAKATI KUMBE UNAWEZA KUPEWA KIZURI ZAIDI YA KILE AMBACHO MWENZAKO AMEPEWA,TUACHE HOJA ZA KUDANDIA HAZITATUFIKISHA MBALI.TUWE NA KATIBA INAYOZUNGUMZIA TANZANIA NA MTANZANIA NA SIYO MAKUNDI YA WATANZANIA,MKIANZA KUJADILI HOJA YA KATIBA KWA MISINGI YA DINI,TUTAFIKIA MAHALI TUTASEMA UKANDA,HATIMAYE KABILA NA MWISHOWE KOO,VITA YA SOMALIA NI YA KOO.TUCHUNGE NDIMI ZETU.

    ReplyDelete
  4. Kama masuala ya uendeshaji wa masuala ya dini haupaswi kugharamiwa na serikali askofu atuambie kwa nini kodi zetu zinatumika kusaidia hospitali na shule za kanisa? Je hajui kuna kodi zetu zinatumika kugharamia balozi za nje zilizopo hapa nchini ukiwapo ubalozi wa Vatican ambao hauwakilishi nchi ya Italy? Askofu hajui kwamba badala ya kutulipa ushuru unaostahili kanisa linapata msamaha wa ushuru unaotokana na vifaa (mfano magari ya maaskofu) vinavyonunuliwa nje kwa kodi zetu? Hebu viongozi wa kanisa acheni unafiki. Hakika nyie kwa udini ni hatari kuliko wana siasa! Suala la mahakama ya kadhi ni imani ya watu wengine, nyie mnaingiaje humo tena kwa hoja dhaifu? Acheni kuingilia ibada za wenzenu. Hakika msipoacha hii nchi itaingia kwenye machafuko ya kidini na hakutakuwa cha kwenda kanisani au msikitini. Inapaswa sote, waislamu na wakristo tukemee tabia hii hata ikitolewa na viongozi wetu wa kiimani. hata kwa upande wa waislamu mkisikia viongozi wa dini yenu wanaingilia mambo ya wakristu muwakemee maana wanatupeleka pabaya huko.

    ReplyDelete
  5. Mimi ninashangaa sana Waislam kila wanapotaka mambo yao ya Uislam yaingizwe kwenye Katiba wanatutajia nchi zingine. Jamani sisi hatutaki kuiga nchi zingine. Wakiuana na sisi tuuane. Kila nchi inaangaliwa kwa historia yake! Na ninajua mbinu wanazofanya waislam kutaka wapewe upendeleo haitawezekana kwa nchi kama Tanzania. Wewe unayesema unataka shehe wenu mkuu akae pembeni muingie ninyi vijana na sisi wakristo tunasema wakina Pengo na wakina Kikura wakae pembeni ili tupambane sisi vijana wa kikristo na waislamu. Wakristo siyo waoga kama unavyofikiri tupo tayari kwa lolote na sisi. Juu ya kuwataja wanasiasa wa Kenya hapo maaskofu wanachotaka kuamanisha ni kwamba hiyo mahakama inawataja hao wakenya kwa vile ni wa waafrica lakini wazungu wanapofanya makosa hatuoni wakishitakiwa mahakama ya Kimataifa isiwe ya wahalifu wa kiafrica tu. Ni kweli walikosa lakini na wanasitahili kuadhibiwa ila tunataka wanaofanya makosa wote washitakiwa bila kujali langi zao au mahali wanapotoka.

    Tunataka katiba mpya lakini isiyo na udini wala upendeleo kwa CCM. Tunataka katiba ya maendeleo siyo ya kuendeleza dini moja. Waislamu waanzishe mahakama yao nje ya mfumo wa serikali kama sisi tulivyo na mahakama zetu za kanisa zinafika mpaka synodi za juu lakini hatujawahi kusema hizo mahakama ziandikwe kwenye katiba yetu.

    ReplyDelete
  6. Ndugu Mhariri wa majira, mimi naona hii nchi sasa inakwenda pabaya. Kama masuala ambayo ni muhimu kwa utawala wa nchi hii yanaleta migongano ya kidini sasa basi. Nani asiyejua kuwa mtu awe muislamu au mkristu suala la kuwa na katiba mpya ni lazima kwa sasa? Hao wanaotaka kuchanganya masuala ya katiba mpya na dini si wananchi wa kawaida. Hawa ni viongozi tu waliopo madarakani wanajifanya watu wa kawaida wanaotoa maoni yao lakini sio kweli lengo lao wanataka kupotosha haya mambo mazuri, siyo vinginevyo. MWISHO NASEMA SUALA LA KATIBA MPYA NI LAZIMA. HATA WEWE UNAYEJIITA MUISLAMU AU MKRISTU UTAKUJA KUJUTA BAADAYE ENDAO SUALA HILI HALITAFANYIWA KAZI SASA!!!!

    ReplyDelete
  7. Katiba mpya ni lazima na makundi yote yahusishwe,hoja ya mahakama ya kadhi haizikwi ila tutazikwa mimi na maaskofu waliotoa tamko hilo.tutaidai hata katika mfumo wa nje ya mfumo wa mahakama. uliyetoa hoja kwamba mahakama ya kimataifa inawashtaki waafrika wa kenya tu si kweli kule wapo wengi tu hata wazungu wapo ila la kutia shaka ni mfano wa Baba Askofu kwa Iraq ambaye amesahau nchi hii imevurugwa na Bush,wahanga wa vifo huko si Wakristo pekee,wapo Mashia,Masunni mpaka Mapagan na raia wa kawaida. kwa hivyo kwa Iraq bora angetuambia Bush naye afikishwe huko tungemuelewa. Tujadili katiba yenye manufaa kwa Mtanzania tuache kuchaguliana mambo,tuache yawe wazi halafu tuangalie athari na faida zake.

    ReplyDelete
  8. Ninamuunga mkono yule aliyesema kwamba awe mkristo au Muislamu ana hitaji katiba mpya. Katiba mpya ni mhimu sana kwa sasa kwa ajili ya usitawi wa taifa letu. Ila baadhi ya watu wanataka kutuvuruga kwa kulichanganya na swala la mahakama ya kadhi. Nijuavyo wakristo hawapingi mahakama ya kadhi ila ianzishwe nje ya mfumo wa serikali. Mahakama zote ziwe za jadi, za maabalaza ya dini ikiwemo ya kadhi zinaweza zikatambuliwa na kuheshimiwa ndani ya katiba yetu. Ila zisighalimiwe na serikali kwani zitakuwa ni mzigo. Serikali yenyewe ishughulike na maendeleo ya watu na isijihusishe kwenye kuendesha tasisi za dini. Yupo anayesema ubalozi wa Vatikani, huo ni sawa na ubalozi wa Irani, Saudi Arabi ni za Kislamu zinazoendeshwa kwa mjibu wa sheria za dini ya kislamu lakini kwa mfumo wao hawatulazimishi sisi wote kuwa wafuasi wa dini za kiislamu. Lakini OIC iko wazi katika katiba yake naomba watu wasome malengo ya OIC kama yataruhu nchi kama Tanzania na mfumo wake kujiunga nayo.

    Nasisitiza kwamba katiba yetu itakayoundwa izingatie mazingira, mila na utamaduni wa nchi yetu Tanzania. Isiwe katiba ya kuiga nchi fulani. Nchi ambazo zinaudhoefu wa kupigana vita.

    Ebu tujikumbushe wimbo wetu wa Tanzania, Tanzania ninakupenda kwa moyo wote. Ninaendapo nakuota wewe. Tuangalie sana kweli tutaendelea kuipenda nchi yetu ambayo tunatembea tunaiota au tuichukia kwa ajili ya ujinga wa watu wachache ambao sasa wanatuingizia malumbano ya udini ambayo hatukuyazoea? Eti tu ili tuwaunge mkono na wapate sababu ya kututawala kwa mgongo wa dini?

    ReplyDelete
  9. Baba Askofu umenena, na umekuwa muwazi kwa kuliweka mezani hili na lijulikane.

    Hawa wenzetu tuendelee kuwaelimisha kwa sababu walisha potoshwa na viongozi wao. Wanapoongelea suala la Vaticani ni lini walisikia hata siku moja limeongelewa katika bunge. Au ni kifungu gani katika katiba kinasungumzia haya mambo ya vaticani. Au bageti ikisomwa ni kiasi gani basi kinaingia kwa hawa watu wa Vaticani. Utaona hakuna wao wanaendesha kama taasisi ya dini. Na hawa ndugu zangu waislamu kama wanataka mahakama ya kadhi basi waanzishie huko vichochoroni na waombe kibali serikalini lakini sio kuingizwa kwenye katiba ya Tanzania hilo haliwezekani kamwe.

    Wao wanaendelea kudanganyana na kujipa matumaini kuwa litawezekana haliwezekani hizo ni ndoto za abunuasi. Sisi tunajua serikali inajitosheleza kwa mahakama ilizo nazo haiitaji kuongezewa mzigo mwingine. Huo ni mzigo wenu waislamu na mkaongelee hayo makesi yenu huko kwa sababu mnajua inavyoendeshwa. Chaajabu ukimuuliza huyu muislamu eeh hii mahakama itasaidia nini wanakuambia hata wao hawajui.

    Mtu mmoja asipende kuyumbisha Tanzania,Serikali muwe makini kwa haya mambo na hiki kimbelembele cha mahakamaya kadhi kife tuongelee mambo ya maendeleo. Katiba ikianza litawekwa mezani lichambuli upungufu na faida zake sio kukurupuka tu na kuiweka. Kwanza ninafikiri hata lisiwepo kabisa linaweza kuvuruga mawazo ya watu na kuhatarisha amani.
    Sisi tunajua tunataka KATIBA kutokana na mwenendo wa sasa hapa Tanzania sio kwenda kuiga mambo ya kadhi.

    Sisi tunaikataa katiba ya sasa kwa sababu iliachwa na mkoloni wao wanatuletea mambo ya mahakama ya kadhi ina maana bado tuendelee kuiga, kuweni wastaarabu na mjiamini hata sisi tunaweza kujitungia sheria zetu na kuzifuata.

    ReplyDelete
  10. Sioni sababu ya kuhoji balozi wa vatican ndo kigezo cha tanzania kiunga na OIC. tukumbuke vatcan sio jumuia ni nchi kamili ambayo inamipaka yake, taratibu zake (katiba) na kiongozi wake, sio kweli vatcan ni himaya ya italy. kwa maelozo zaidi vatcan ina sifa kamili ya kuwa mwanachama wa UN sema wao hawataki kujihusisha na mambo ya jumuia za kimataifa. tuelezane ukweli OIC inaweza kuwa mwanachama wa UN?
    jaman hii nchi imejengwa kwa misingi ya kuheshimiana haina sababu kila kitu wanachokifanya wenzetu ni sahihi, tujijengee uwezo wa kupambanua mambo kabla ya kuyatekeleza, haiana sababu eti kwakuwa kenya, uganda majirani zute wanafanya hivi na sisi lalima tufanye hivyo
    mbona hamtaki kushabikia udikteta wa mseven kuitawala uganda milele, eti kwa kuwa m7 hataki kuwaachia waganda wengine waongoze gurudumu la maendeloe ya inchi yao, basi na si kikwete nae ang'ang'anie ikulu
    suala la kadhi, OIC libaki mikononi mwa waislam litatuletea matatizo, likiwa ndani ya katiba hii si nchi ya kiislam wala kikristo jamani, interest za kikundi fulan hazipashwi kuwa kipaumbele cha katiba
    hata bakwata ingetawaliwa na vijana wa namna gani hatutakubali kubuluzwa na wachache

    ReplyDelete
  11. Tunasema tunapojadili katiba kila kitu kiwe mezani kichambuliwe kwa kina pamoja na faida na hasara zake kwa wananchi,hatutaki taasisi fulani iseme hili liwepo hili lisiwepo. Tatizo ni kwamba wengi wengu wanaimba tunataka mabadiliko ya katiba lakini ukimuuliza hii iliyopo ina kasoro gani,hajui kwa sababu hajawahi kuisoma au atakuambia katiba haifai kwa sababu imemuibia kura Slaa au muislam atakuambia katiba inaonea Waislam.OIC ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine za jumuia ya kimataifa na Waislam walipodai Tanzania ijiunge nayo wakaambiwa ni uvunjaji wa katiba ndio maana wanataka kama hoja ni hiyo basi iingizwe kwenye katiba.hata mwalimu nyerere aliwahi kusema hilo si tatizo ila nchi ifate taratibu za kujiunga uanachama katika taasisi hii,na mwenyewe Nyerere alisema mbona nchi kama Uganda na msumbiji ni wanachama na akatamka wazi taratibu zilikosewa. sasa mnatuambia nini? hebu tuiwekeni katiba wazi,tusichaguliane

    ReplyDelete
  12. UDINI NI WA KIKWETE NA WENZIWE WACHACHE. KIKWETE HATA WIMBO WA MATAIFA WA AFRIKA MASHARIKI ALIUKATAA KWA MAELEZO KWAMBA "IT SOUNDS TOO CHRISTIAN". WAKATI MMOJA LISEMA ISINGEKUWA WAKRISTO, YEYE (KIKWETE) ASINGESOMA. LAKINI ANAWACHUKIA WAKRISTO SANA. KWA KIKWETE AKIKUAMBIA TWENDE KUSINI, UJUE ANAWAZA KWENDA KASKAZINI. AKISEMA ANACHUKIA RUSHWA, UJUE ANAIKUMBATIA. AKISEMA AMANI NA UTULIVU, UJUE ANAONGEA VITA. AKISEMA TUNATOA MAMBO YA KADHI KWENYE ILANI YA CCM 2010, UJUE ANAITAFUTIA KASI ZAIDI. ATAISHIA BABAYA. NAWAUNGA MOJA KWA MOJA MAASKOFU KWA KAULI YAO ISIYOKUWA YA KINAFIKI WALA KUJIKOMBA. WAME ACT RESPONSIBLY. WASIDANGANYWE ATI WAO WHUBURI TU DINI HUKU SHERIA NA HAKI ZA WANANCHI ZINAKANYAGWA WA WATAWALA WA CCM NA SERIKALI YAKE, YUMKINI PIA INA WAKRISTO VIONGOZI WANAFIKI WAKUBWA. OLE WENU NA VIZAZI VYENU..ASEMA BWANA!

    ReplyDelete
  13. MIMI SIOGOPI MAHAKAMA YA KADHI ILA NINAOGOPA MAMBO HAYA HAPA. MIMI NI MWISLAM LAKINI YANANITISHA KWA KUIPENDA TANZANIA KISIWA CHA AMANI. IMETOKA GAZETI LA MZALENDO.

    Tangu Askofu Mkuu Toto alipofariki shughuli za kanisa hilo zilikuwa zikiongozwa na Askofu Mkuu mstaafu wa Anglikana Tanzania, Askofu Mtetemela na baada ya kustaafu hivi sasa kanisa hilo linaendesha shughuli za kiroho chini ya usimamizi wa Askofu Mkuu wa Tanzania, Valentine Mokiwa.
    Sambaza chapisho hili!
    Ingizo hili limetumwa na makame silima tarehe 12/12/2010 nyakati za 9:24 mu, na limehifadhiwa katikaHabari. Fuatilia majibu yoyote katika chapisho hili kwa RSS 2.0. Unaweza kuruka hadi mwisho na kutoa majibu.Pingi hairuhusiwi kwa sasa.
    • MAONI (27)
    • #1 andikwa na Hassan10
    takriban siku 1 iliopita
    Jee wz’bar mupoooo? huyu Agustino Ramadhani jaji mkuu wa Tanganyika juzi aliulizwa kuhusu katiba ya Zanzibar kuandikwa upya alisema haijuwi maana hajapelekewa akaisoma?. lakini ya Tanzania anaijuwa maana kaisoma? na mimi nilikuwa sijuwi kuwa Popo wa Z’bar kumbe na yeye huchaguliwa Dodoma tena wa mara hii asitoke zanzibar atoke vatican Rome Itali?
    • #2 andikwa na sale
    takriban siku 1 iliopita
    Jamani hizi sura za kikafiri zipo Zanzibar ama hii picha imechukuliwa toka Tanganyika? na kama zanzibar basi kumbe kuna makafiri wengi,,,
    Msalieni mtume janiiiiiiiiiiii,,,,,
    Hongera Komando Salmin Amour na Bilali matunda yenu tumeyaona,,,,,,,,,,,,
    • #3 andikwa na Mrfroasty (Ufundi)
    takriban siku 1 iliopita
    Hadi viongozi wa dini pia wanachaguliwa Dodoma, nilidhani ni viongozi wa kisiasa pekee!
    • #4 andikwa na salix2020
    takriban masaa 23 yaliopita
    ah hawa wengine kujipachika majina ya kiisilamu na wakati ni makafiri sijui wanahisi wanamzuga nani kwa sababu nakumbuka miaka ya iliyopita wakati wa utawala wa mkapa aliwahi kupelekewa barua kutoka jumuia moja ya kiislamu tanzania ya kutaka usawa katika nyanja mbali mbali ndani ya serikali ya tanganyika baina ya waislamu na wengineoe kutokana na kuonekana serikali ya tanganyika kulibeba kanisa na waumini wake na kuwabana waislamu wasipate haki zao inavyostahiki basi miongoni mwa majibu yake alisema hamuoni katika serikali kuna viongozi kibao wana majina ya kiislamu mimi nilidhani atasema huoni kuwa kuna viongozi kibao wakiislamu wamo katika serikali yake lakini akasema viongozi wenye majina ya kiislamu sasa ninachokusudia hapa inaonekana hawa makafiri wa tanganyika kujipachika majina ya kiislamu ndio kujipatia kibali cha kuaminiwa na waislamu ama nini? au wenzangu mna maoni gani?
    • #5 andikwa na salix2020
    takriban masaa 22 yaliopita
    na jengine ndugu zangu wazanzibari nawausia jamani hata kama kwetu kuna dhiki vipi basi kama una viwanja basi ni bora kumuuzia ndugu yako yoyote wa kizanzibari na sio kafiri yoyote wakitanganyika hata akikwambia anataka kufanya jambo gani basi ni kheri usiuze kwa sababu miongoni mwa ajenda kuu za ukoloni wa kitanganyika kwa zanzibar ni kuifanya zanzibar kuwa haina tofauti na dar-es-salaam kwa makanisa kwa hiyo jamani mujue ukimuuzia mgeni yoyote kiwanja na ikathibiti kuwa simuislamu hasara yake ni kwa kizazi kijacho kama tuna uchungu na uzalendo na nchi yetu basi suala hili ni la kulizingatia ahsanteni
    • #6 andikwa na Manyamba
    takriban masaa 21 yaliopita
    acheni chuki za kidini, nyinyi wenyewe mmejazana ktk nchi za watu huko ulaya mbona hamjafukuzwa? wakristo wana haki km walivyo waislam zanzibar, hata Mtume SAW aliishi na wakristo kwa wema tu ktk kipind chake, hakuwatukana wala kuwanyanyasa, someni dini vizuri msijitie waislam kumbe hamna lolote mnalolijua, kwanza Zanzibar sio nchi ya kiislam bali ni nchi ya waislam, tena nn kupiga kelele zilokuwa hazina maana? hata km ingekuwa ya kiislam basi bado wakristo wana haki ya kuishi zanzibar, hakuna baya lolote kuchagua viongozi wao, na nyinyi chaguen wenu msiwatukane wakristo bureeee…


    ENDELEA HAPO CHINI..........

    ReplyDelete
  14. Maoni mengi ni mazuri na wote mna kitu kimoja cha msingi mnaonekana mnaipenda kweli Tanzania kwa wote kuunganishwa na kitu kimoja nacho ni KUTAKA KATIBA MPYA.
    Endeleeni kuiombea nchi yenu maana inapita ktk kipindi kigumu sana cha kiuchumi.

    ReplyDelete
  15. Huyo anayemuhusisha Kikwete na katiba mpya hana budi akapimwe akili maana hata alilozungungumza hajui,ameona tu bora aandike. Huyo Mr President ni mstaarabu sana na mnapaswa kuiga ustaarabu wake,ni mvumilivu sana wa matusi yenu,hapa tunajadili katiba hatumjadili mtu,hizo hasira zenu hata mkifanyaje uchaguzi umepita na yeye ndiye Rais wa Jamhuri ya Tanzania,tunajua kwa nini hapendezi kwenu lakini matatizo ya nchi hii kayakuta yametengezwa na Mkristo mwenzenu Mkapa,sina haja ya kuendeleza haya yameisha pita,nazungumzia au nachangia mawazo ya katiba yetu mpya. Nasema kuwa tunaptaka katiba mpya lazima uwanja uwe mpana,kanisa lisiipangie nchi lipi lijadiliwe na lipi lisijadiliwe hapana haya ni makosa makubwa sana,katiba ni meza ya majadiliano na katika mkusanyiko wa jamii mbalimbali kila mtu ana wazo lake,tuache kuwaunder rate wengine,huu ni mfumo dume mlioachiwa na mkoloni wa Kiingereza ambao kwa sasa haufanyi kazi. tupiganie katiba mpya na tuangalie hiyo katiba mpya haimkandamizi yoyote,hapa pataeleweka,msimsakame Kikwete kwani yeye ni Mwenyekiti wa CCM na si M,kiti wa Islamic CCM,na hata angetaka asingeweza kwani ndani ya CCM kuna waumini wazuri sana wa dini ya Kikristo ambao hawawezi kukubali Ukristo udhalilishwe,hayo yanayotokea huko kwingine si mwongozo wa dini bali utashi wa vikundi vya watu vinavyotumia kivuli cha dini.

    ReplyDelete
  16. mahakama ya kadhi ni suala la kidini. suala la balozi wa vatican c kiashiria kwa sababu mbona balozi za nchi za kislam zipo nchini! Tz kuna watu wameoana mume mslam na mke mkristo watoto nao wafamilia hiyo wako waslam na wakristo.Mahakama ya kazi kuwekwa kwenye katiba ni ndoto. hilo ni suala la binafsi, yaani kodi yangu itumike kwa kitu hakina masiahi kwangu bali kwa kinkudi fulani? Nchi zilizo na mahakama ya kazi si kigezo cha cc kufuata mkumbo, nchi zenyewe zilikuwa na machafuko. pia badhi ya nchi hizo zinataka kuondoa kwenye katiba zao. cha msingi mahakama ya kadhi iwe kama NGO, mtafute hele wenyewe kwa michango acheni kutaka dezo. baada ya kuangaikia elimu na mko nyuma sana. mahakama ya kadhi haina tija. bado itakuwa inashughulikia masuala ya ardhi,ndoa na miradhi tu masuala ya jinai hayapo. na cc tz mchanganyiko wa dini zetu zimeingiliana sana, mnataka kuleta vita vya kijamii. hakitakubalika na damu itamwagika!

    ReplyDelete
  17. Hakuna anayetaka pesa za serikali,tutatafuta za kwetu wenyewe,hakuna vita ya kijamii hapa ila kanisa linataka kuwa linatoa mwongozo wa uendeshaji nchi hasa kanisa la catholic,hili ni jambo lisilokubalika,kwanza tunawaambia nyie kuwa suala la mahakama ya kadhi ni la waislamu haliwahusu,linahusiana na waislamu wenyewe. hapo zamani kulikuwepo na MALIWALI lakini kwa bahati mbaya hamsomi historia ya nchi yenu,mnakurupuka tu,hawa walikuwa ni kwa ajili ya mambo yanayowahusu Waislam tu,iliondolewa hii na skuli za misheni ambazo zilikuwa zinachukua Wakristo tu kwa ajili ya elimu,mwalimu aliziondoa kwa sababu za msingi,lakini kama serikali imerudisha skuli hizo kwa kanisa mbona waislam hawalilalamikii hili,pili usidanganye walioliweka kwenye katiba zao wanataka kuliondoa wewe ni muongo na mnafiki mkubwa,hapo jirani zetu Kenya kuna watu bila shaka walitumwa na makanisa kujaribu hilo na walionja joto ya jiwe,walijaribu kufungua kesi ya kikatiba na walishindwa,hatuna haja ya pesa zenu na si zenu ni za kwetu sote na wote tunatakiwa tuwe na maamuzi ya jinsi ya kutumia. Mahakama ya kadhi inahusiana na sheria za Kiislamu tena ni katika mambo ya ndoa,mirathi na haimlazimishi hata muislamu mwenyewe kwenda huko,msiitafsiri vibaya kwa makusudi ya kupotosha watu.na wala hauvurugi mfumo wa sheria yoyote ya nchi. HIVYO TUNASEMA KATIBA NI UWANJA MPANA WA HAKI MBALIMBALI ZA KIJAMII NAZO LAZIMA ZIWE NA MAPANA NA MAREFU YA MJADALA,SASA HAIWEZEKANI ASKOFU ASEME SUALA HILI LIZIKWE KABISA,HAIWEZEKANI HATA KIDOGO KANISA LISEME HILI LIJADILIWE HILI LISIJADILIWE,WACHA HATA MAPAGAN WALETE YAO,KUTAKUWA NA JOPO LA WATAALAM KUTOKA KADA MBALIMBALI WATACHAMBUA NA WATATOA MAPENDEKEZO YAO NA KUTAKUWA MFUMO WA KUJADILI.ACHENI MFUMO DUNI HUO NA HII DUNIA IMEBADILIKA WATU HAWADANGANYIKI.IACHENI KATIBA IJADILIWE KAMA KATIBA NA INA TARATIBU ZAKE TUSIANZE KUCHAGULIANA NA KUTAFUTA VURUGU,LILE LILILO JEMA KWA NCHI YETU NDIO LITAPEWA KIPAUMBELE NA HATA HUO MFUMO WA MAHAKAMA YA KADHI KAMA WATU WANA NIA YA DHATI BASI HAUNA TATIZO UTATAFUTIWA NJIA MBADALA.TUSIANZE KUUTAFSIRI KWA NJIA POTOFU

    ReplyDelete
  18. Nashangaa hawa wanaosema ubalozi wa vatican hapa. Hawajui ya kuwa vatican ni nchi? Hii ndio nchi yenye eneo dogo kuliko zote duniani na haiko chini ya Italy. Someni muelewae kabla ya kusema. Balaozi wa Vatican nchini ni kama alivyo balozi wa Iran ambayo ni nchi ya kiislamu. Mbona hiyo hamsemi? Ni siyo Iran peke yake nchi zote za Mashariki ya kati ambazo ni za kiislamu zina balozi zake hapa Tanzania mbona hizo hamsemi? Mahakama ya kadhi ni suala lenu waislamu kwa nini mnataka kuliingiza kwenye katiba inayohusu Wakristo, wapagani, Wahindu, Wabuda na dini nyinginezo?. In maana sasa kila dini itataka kuwa na mahakama yake. Sijui hiyo itakuwa nchi ya aina gani. Kuna mambo mengi yenye kero kwa watanzinia kwa ujumla hayo ndiyo yanayotakiwa kujadiliwa ni sio hili la kuangalia dini moja.

    ReplyDelete
  19. Juzi ubalozi wa Vatican ulitoa agizo la pope kuhusiana na mapadri. JE ULIWAHI KUSIKIA UBALOZI WA SAUDI ARABIA UKITOA AGIZO KWA WAISLAMU? BALOZI YA VATICAN IKO HAPA KWA AJILI YA KANISA LA KATOLIKI NA HAIKO KISIASA NA BALOZI WA SAUDI ARABIA AU IRAN NI BALOZI ZA KISIASA KAMA ZILIVYO BALOZI ZA MAREKANI,UK,FRANCE NA ZINGINEZO AMBAZO HAZITOI AGIZO KWA WAKIRISTO BALI KWA AJILI YA NCHI ZAO. TUZUNGUMZIE KATIBA YA NCHI YETU HAYO YA UDINI TUWEKE MBALI,KILA DINI KAMA INATAKA MAHAKAMA YAKE IWEKE JUU YA MEZA PANA YA KATIBA ICHAMBULIWE INATAKA ISIMAMIE NINI KATIKA MAHAKAMA YAKE,WAISLAMU WAMEISHAELEZA NA INAFAHAMIKA MAHAKAMA YA KADHI INASIMAMIA NINI NA HILO LINAFANYIKA KATIKA NCHI ZA JIRANI ZETU BILA ZOGO.

    ReplyDelete
  20. Huyu jamaa alieandika mambo ya maliwali hapo juu acha kupotosha jamii. Nenda shule ukasome Historia vizuri. Mimi simwelewi kama hawa liwali ndio walikuwa wanafanya kazi mahakama ya kadhi. Au walikuwa wanafanya kazi kutokana na mazingira yao na ujiulize kazi ya maliwali ilikuwa nini.

    Sasa kama ni mambo ya ndoa na mirathi Tanzania haina chombo cha kushughulikia hizo haki. Yaani watu wanaombea kuishi kwa amani wewe unatafuta mahakama za kusuluhisha ndoa.

    Na kama sio pesa za uma zitakazotumika sasa unawasumbulia nini uma kuhusu haya mahakama ya kadhi. Tumesha waambia tena hilo ni lenu mtajua wenyewe waislamu mtakako malizia nalo. Mkifuata sheria hakuna mtu atakae wazuia kama mnavyowajua wakristo hawachongi sana.

    Labda Mh makamu wa rais kwa sababu alisha toa hiyo ahadi tumsubirie atawaeleza nini wananchi kwa sababu wakristo wakiendelea na malumbano na waislam kwa maneno ya chini chini hivi ndio uhasama unazidi kujijenga. Waislamu wataona wakristo wanatunyima haki kumbe sio kweli.

    Mimi siwezi kukueleza labda utafute mtu alieenda shule umuombe akusaidie zaidi kuhusu mambo ya dini yanahusiana vipi na mambo ya serikali kwa muundo wa Tanzania yetu. Sio kwenye vibaraza vya kahawa. Vibaraza vya kahawa na darasa ni tofauti. AHSANTE.

    ReplyDelete
  21. Tatizo kubwa la ndugu zetu waislam ni shule. Ukitazama mawazo ya muislam aliyeenda shule utaona mtazamo wake ni tofauti kabisa na wenzake. Ndugu zangu waislamu musikazanie elimu ya Madrasa ndiyo maana hamna hoja za msingi. Hata Kikwete wenu hawezi kuwasaidia maana anaona hamna hoja za kwenda shule. Ni hoja za madrasa na mistahafu ya quoran. Zama hizi ni za kutaka mtu awe amesoma social science vizuri kabisa. Ukiwa na social science education utakuwa na uwezo wa kutofautisha mazingira ya Kenya, Uganda, Burundi na mazingira ya Tanzania yetu. Sina mda wa kujadili kwa kina kwanini wakenya waliichagua katiba mpya pamoja na kwamba ilikuwa na mahakama ndani yake. Sisi tulioishi Kenya tunajua vizuri mazingira yaliyofanya katiba ya Kenya ipite pamoja na uwepo wa mahakama ya Kadhi. Na kwa taarifa yako si kwamba wakenya wanapenda mahakama ya kadhi iwepo ila mazingira ya nchi yao yaliwalazimisha waikubali katiba jinsi ilivyo. Maana ilikuwa ni bora waikubali ile katiba jinsi ilivyokuwa kuliko kama wangeikataa. Wangeliikataa wangeliendelea kushuhudia mauaji ya kila wakati kuliko kwa hiyo ilikuwa ni lazima waikubali katiba mpya pamoja na mapungufu yaliyokuwa ndani yake kama mahakama ya kadhi.

    Ni lazima ndugu zangu waislamu muelewe kwamba waasisi wetu hawakukosea kutenganisha mambo ya dini na kazi za serikali huo ndio umekuwa msingi wa amani yetu. Mahakama ya kadhi ni kutangaza dini ya kiislamu maana waislamu wenyewe wanasema ni sehemu ya ibada kwenye dini yao. Kikwete hawezi kuwapendelea ninyi eti tu kwa kuwa ni muislamu kwani yeye anafuata katiba ya nchi yetu na ameapa kuilinda. La kufanya nini mngelipigania serikali iingize kwenye katiba kwamba mambo ya serikali ya Tanzania ikubali kuzigharami tasisi za dini. Hii itakuwa rahisi sana kwenu kupata mahakama ya kadhi ili igharamiwe na serikali. Na kwa kweli hata mabaraza ya mahakama za wakristo za mabo yahusuyo dini yao yatagharamiwa na serikali. Serikali yenyewe itaona kama ina uwezo wa kugharamia mahakama zote hizo. Ila kwa busara za muasisi wa taifa letu aliona hakuna uwezekano huo.

    Wapo watu wanaosemea mahospital ya mission kugharamiwa na serikali. Ninadhani hakuna mahali popote kwenye katiba inaposema mahospital ya mission za kikristo pekee yake yatagharamiwa na serikali! Hakuna kitu kama hicho. Ila nijuavyo hata hospital za mission yaani za kikristo na za kiislamu na hata za kihindi kama zitatoa huduma bure kwa wananchi bila ubaguzi wala upendeleo wowote zina haki ya kupewa ruzuku na serikali kwani hayo ni moja ya majukumu ya serikali. Ipokuwa kama zinafanya biashara zinalipa kodi. Sasa hapo kama kweli una akiri unaweza kufikiri kwamba hayo si mambo ya ibada hata kidogo. Ni mambo ya huduma za jamii.

    Kwa muislamu mwenye akiri aliyeenda shule kama bwana moja hapo juu alivyotoa maoni yake naamini anaelewa ikiwa atakuwa hana ushabiki wa kidini. Tuache mambo ya ushabiki wa kidini tuangalie maslahi ya taifa letu. Kama kweli tunaipenda Tanzania na tungelipenda iendelee kuwa kisiwa cha amani. Wapo wahuni wengi wanatoa mawazo yao humu. Kama mwingine ambaye hawataki kabisa wakristo wawepo Zanzibar ila waislamu waendelee kuishi Tanganyika. Tanzania ni yetu wote. Wazanzibar wakiachwa watauana tu. Angalia jinsi wapemba walivyoikataa CCM Zanzibar na wanaendelea kufaidi matunda ya muungano kwa kuweza kujenga mahekalu yao Tanganyika. Muungano ukivunjika watapoteza kila kitu walichonacho Bara pamoja na mahekalu yao.

    Kwa wapenda amani wote tukatae kuingiza mambo ya udini kwenye nchi yetu.

    ReplyDelete
  22. waislam wapo wengi mashuleni na vyuoni wewe una mawazo mgando,hayo yalikuwa huko nyuma na yalifanywa kwa makusudi. hilo ndilo linalowasumbua mpaka mnakuwa woga. hamjibu hoja mnaishia waislam hawakwenda shule huwa ni ujinga na upumbavu,karne hii nani asiyempeleka mwanae shuleni

    ReplyDelete
  23. Kwa kweli sisi wengine wasomaji tunashangazwa sana na baadhi ya waandishi wa maoni. Ah! Hivi, kumbe watu wengi ni wajinga sana nchini kwetu Tanzania. Mbona watu wengi wanapenda kujizonga zonga. Haya mambo ya kidini sio ya kupewa kipaumbele kwenye mabadiliko ya katiba. Ikiwa ni hivo, basi kila mtu atoe wapi iko shida yake iingizwe katika katiba. Wacheni wazimu na ujinga. Cha muhimu ni maendeleo ya nchi kiuchumi, kwa hio mambo ya rushwa, na yote yanayorudisha nyuma taifa na (hasa viongozi waroho sana) ni ya kuangaliwa sana.

    Mara nyingi hawa viongozi wanakuwa wameshashiba hela ya rushwa na sasa wanajidai kuzidisha ufisadi, uchochezi mara wa dini, mara ethnicity,kwa interests zao kibinafsi. Na kukoroga akili za umma ili yao ya wizi wa hela yasionekane. Hawana lolote..... Na wanawatumia waandishi wa habari, wanawapa hela za kutosha, ili kutupa chambo kwenye nyanja za maoni ya wengine. Mungu awalani na familia zao.

    ReplyDelete
  24. Sioni sababu ya huu muungano kutokana na maoni ya hapo juu sijui ardhi, sijui mkapa kafanyaje, sijui waislam tanganyika wanafki wanajipachika mjina, haieleweki.

    Tujenge tanganyika yetu tuache malumbano tumewabeba vya kutosha.
    HASHIM.

    ReplyDelete
  25. Sijui Askofu Kitula una rejea gani mkononi mwako, lakini suala la udini Tanzania halikuanza mwaka 1986. (Hili sio kama hujui lakini unakwepa kulizungumzia) Nenda ukasome (hivi vichahe), Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara, 1953 hadi 1985 (John C. Civalon, 1992), Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968): Historia iliyofichwa kuhusu Harakati za Waislamu dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika ( Mohamed said na Ali Salum Mkangwa, 2002)na Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania (Hamza Njozi, 2000) kwa uzuri na hapo utagundua kuwa Utawala wa kikoloni wa kingereza ndani ya Tanganyika,na pia utawala wa Kambarage ulijenga msingi wa hilo hata raia wengine wasiokuwa wakristo walijiona kuwa kama raia wa daraja la pili ndani ya nchi yao waliyoipigania katika kudai uhuru wake. Unaona mwaka 1986 kwa sababu katika kipindi hicho ndio kiongozi muislamu aliingia madarakani na kwamba hata hizi harakati za kudai katiba mpya zinashika kasi wakati huu kwa msingi huu huu. Ninamshangaa Mkapa kwamba naye anataka katiba mpya wakati ambapo miaka michache aliiongoza Tanzania kwa katiba hiyo. Jee hakuliona hilo? Alifika hadi kumdhalilisha jaji Kisanga mbele ya umma wa Watanzania pale alipokuja na mawazo kama hayo katika kazi aliyomtuma yeye mwenyewe. Tatizo hapa ni kuwa kuna kundi la raia wa nchi hii limezoea kupendelewa na kwamba anapokuja mtawala na kujaribu kuweka sawa hapo ndio sauti za kuwepo udini utazisikia. Hivyo Askofu Kitula anataka tuamini kuwa kabla ya mwaka 1986 hakukuwa na udini?

    ReplyDelete
  26. Anonymous wa Dec 22, 7@:14 AM umewapa vidonge vyao. Lau Mkapa angekubali mabadiliko ya katiba katika kipindi chake cha uongozi asingelijukulia mali za taifa na kusaidiana na kina Chenge, Balali na mnafiki Hosea kuifisadi hii nchi. Maana katiba inawalinda wasishtakiwe kisha leo wasema urongo kwa wazungu kuwa eti kikwazo ni JK, hapana kikwazo ni katiba inayowapa kinga! Na Chenge kwa kuwa alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali analijua hilo na hao wa makanisa wanalijua hilo. Subirini mwaka 2015 akija rais mkristo ndio mbadili katiba kama hamtasema ooh katiba hii haina makosa iko sawa.

    ReplyDelete
  27. HAKUNA MSHINDI KATIKA MASUALA YA DINI.
    Waislamu na Wakristo tu Wana wa Mungu; kwa hili hakuna anayepinga kama yupo huyo ni hatari!!!!!
    La msingi hapa tunachojali kwa ustawi wetu SOTE ni kuwa na KATIBA itakayotokana na sisi wenyewe na siyo KAMATI fulani kutengeneza katiba.
    Ustawi hatutauona kama tutaingiza mambo ya DINI katika kutengeneza katiba.Jamii yetu tupo mchanganyiko wa watu mbalimbali na dini tofauti tena sasa hivi yako Madhehebu mengi ya Wakristo zaidi ya 400 sijui ya wenzetu Waislamu!Kwa sasa kuna familia ambazo ni mchanganyiko wa Waislamu na Wakristo,hebu fikiria hao tutawafanyaje? Au kuna malengo fulani???

    ReplyDelete
  28. tatizo nilionalo mimi ni kuwa, wengi miomgoni mwa ndugu zetu wakristo, wamewakabidhi vichwa vyao Maaskofu wafikirie kwa niaba yao, kila tamko linalotolewa na Maaskofu kwao wao ni amri ya Mungu, jambo hilo limewanyima uhuru w\a kufikiri, aidha wanashindwa kutofautisha baina ya kusoma na kuelimika, suala la mahakama ya kadhi ni suala dogo sana, wala halistahili hofu hii kwa wakristo, kuwenu huru kufikiri na kujadili, hizi si zama za ukasuku.

    ReplyDelete