08 December 2010

Iniesta, Xavi, Messi kuwania tuzo ya FIFA

 Hispania

WACHEZAJI watatu wa Barcelona, Andres Iniesta, Xavi Hernandez na Lionel Messi wametajwa kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka, inayotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA), ijulikanayo kama 'Ballon d’Or'.

Viungo Iniesta na Xavi, ndiyo waliyoisaidia Hispania kutwaa taji lake la kwanza la Kombe la Dunia mwaka huu, wakati mshambuliaji wa Argentina Messi ndiye aliyeiongoza Barcelona kutwaa ubingwa mwingine wa Hispania.

Kwa sasa Messi, ndiye anashikilia taji hilo la Ballon d’Or, ama mpira wa dhahabu baada ya kulitwaa mwaka jana ambaye kuteuliwa na jarida la michezo la nchini Ufaransa.Lakini mwaka huu, tuzo hiyo ya mchezaji bora imeunganishwa na FIFA ili kuweza kutoa tuzo moja.

“Ni heshima kuwa miongoni mwa wanafainali watatu wanaowania tuzo ya Ballon d’Or na kizuri zaidi ni  kuwania tuzo hiyo sambamba na Xavi na Leo,” Iniesta aliandika katika tovuti yake ya Facebook. “Tuzo hii ni kubwa mno katika fani yetu,” aliongeza.

Wakati wachezaji hao wakiwania tuzo hiyo, mchuano wa kuwania nafasi ya kocha bora upo kati ya Jose Mourinho ambaye amewahi kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa na vikombe vya ligi ya ndani na ubingwa mara mbili, akiwa na timu ya Inter Milan, Mhispania Vicente del Bosque na kocha wa  Barcelona, Pep Guardiola.

1 comment:

  1. H\Kama hata sisi waTZ tungetakiwa kutoa maoni ni nani hasa anastahili tuzo hiyo, basi chagua langu mimi lingekuwa Iniesta. Katika kombe la dunia alicheza ile inayoitwa "JIHADI" hadi alipofanikiwa kuwatwaa mashabiki na dunia nzima kimasomaso kwa kulichukua kombe! Kila la heri kijana wa watu huyu. Kuna siku na sisi tutakuwa na Iniesta wa Bongo. Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete